Tetesi: Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CHADEMA kuhusu kuacha kuhudhuria vikao vya Bunge. Kuna fukuto la chini kwa chini

Tetesi: Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CHADEMA kuhusu kuacha kuhudhuria vikao vya Bunge. Kuna fukuto la chini kwa chini

Mbowe akiunguruma pale ufipa wafuasi wa Chadema hujificha chini ya meza
Naamini kuna tatizo katika vichwa/akili za viongozi wa juu wa CHADEMA. Wanachama na Wafuasi wao, ndani na nje ya chama. Siamini kama Mbowe tu ndiye anayewaburuza labda hata viongozi wenzake ni walemavu wa akili. Mifano iko mingi kutetea hoja hii.
1) Bunge la Katiba, walisusa vikao na kuunda UKAWA ambao umesaidia tu kukijenga CHADEMA.
2) Bunge la kwanza, kwenye utawala wa Rais Magufuli, walisusia kusikiliza hotuba yake. Kwa mtu mzima, makini, mwenye hekima na busara, kiongozi aliyechaguliwa na watu kuwawakilisha kwenye chombo kimojawapo cha juu katika Dola, na anaheshimu dhamana hiyo, asingefanya hivyo. Japo walitoka bungeni ni wazi waliendelea kusikiliza hotuba hiyo nje ya bunge na ndiyo maana wamekuwa wakirejea baadhi ya hotuba hiyo kwenye mijadala yao ya madai mbalimbali yenye msingi wa ubinafsi na siyo Taifa. Wanayaimba kila siku kama ndege kasuku.
3) Mara nyingi wamekuwa wakisusia vikao vya bunge vya bajeti ili hali wakidai majimbo yao yapate maendeleo. Pamoja na kususia vikao hivyo bado Serikali huwalipa mishahara, posho na pesa ya mfuko wa jimbo ambayo baadhi ya wabunge huitumia kwa maslahi binafsi.
4) Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mtukufu Mbowe aliwaagiza wagombea wote kususia na wakatii bila kuuliza kulikoni na madhara yatokanayo na kufanya hivyo.
5) Jana, M/Kiti wao, Mtukufu Mbowe, tena kawaagiza kususia kikao cha bajeti wakajifungie kwenye makazi yao hapo Dodoma, na wala wasiende kwenye majimbo yao, ati kwa kuogopa kuambukizwa COVID-19 kana kwamba hao wabunge wana akili za kitoto zisizojua athari za kutojikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko na usalama wa maisha ukibaki mikononi mwa wazazi.
6) Bila kusahau wanaCHADEMA, wakati wa Uchaguzi Mkuu, 2015, walivyokuwa wanazungusha mikono (ati ndiyo mabadiliko) na kupiga deki barabara ili Mabwana zao wapite.

Ni wazi kabisa, pasipo na shaka Mbowe ni BABA LAO. Na viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wamebaki kulamba na kumeza kila linalosemwa na kutendwa na Mtukufu wao Mbowe.
 
Kweli Mkuu Chadema wasingekimbia bunge ila wangepiga nyungu
Kama Kujiweka Quarantene ni kukurupuka ,Kuazimisha NYUNGU ambapo hakuna mchanganyo( Ingridients) maalumu, Kila mtu anajichagulia majani yake na kuchanganya atakavyo,Hali kadhalika NYUNGU pia jichagulie saizi yako bila kujali chochote mwengine la kilo 2,3,5, Haina fomula .....
Kwenye hili hujaona UJUHA wala UKURUPUKAJI?,
Ushauri :-
Tuyape yote Nafasi na baadae tufanye Tathmini lipi ni la KIBWEGE na Lisilo na MAARIFA.
 
Tusubiri bomu kulipuka
Kama wabunge hawakushirikishwa hata mimi nakubaliana na wewe siyo sawa ila pamoja na hayo ushahidi ni muhimu kutuletea hapa ku validate HOJA yako
 
Umeona wabunge waliofariki ni watatu na hao wengine watakuwa kumi na tatu, ilà wabunge wametajwa kwa sababu ni wabunge. Hao kumi na tatu kiuhalisia wanaweza kuwa wengi zaidi, sina facts hivyo nasema HUENDA!!
Simple logic ni kuwa mkusanyiko wowote wa watu huwa ni kichocheo kwa covid 19 na hivyo huendea kwa haraka zaidi.

Hivyo hivyo kama vifo bungeni ni 3 kati ya wabunge 300 na nje ya bunge ni 13 kati ya watu 50,000,000 utaona hapo ratio iliopo. Uraiani kila watu wastani wa 4,000,000 kukpmetokea marehemu 1. Na bungeni kila kwenye wabunge 100 kumetokea marehemu 1
 
Kwa hili Chadema wametusaliti Watanzania Lazima tuwanyooshe October
Hata kama wangekuwa wengi kiasi gani Mbunge ni Mwakilishi wa Wananchi sasa kama yeye anakimbia vita sasa nani ataongoza mapigano kwa wapigakura wao??
 
Zingatia makosa ya kimtandao Tumechoka kuchangia watu na mnampa shida Melo kuitwa mahakamani Kwasababu ya uzushi wenu
Umeona wabunge waliofariki ni watatu na hao wengine watakuwa kumi na tatu, ilà wabunge wametajwa kwa sababu ni wabunge. Hao kumi na tatu kiuhalisia wanaweza kuwa wengi zaidi, sina facts hivyo nasema HUENDA!!
 
Hawa Chadema wanafikiria Rais wa Nchi ni sawa na kuwa meya wa ubungo
Wewe acha ukichaa Rais huwezi mlinganisha na Mbunge!! Rais ni nembo ya nchi analindwa sana tu kama kuna tatizo lolote nchini yeye anakuwa wa mwisho kuumizwa unafikiri Rais anatakiwa kuwa mbele? Haijawahi tokea duniani labda kwenye Saccos ya Chadema!
 
Kwanini Mbowe awalazimishe wabunge kujitenga ? Huu Sio udkteta ?
Hata kama wabunge wa CHADEMA wasingeamua kuchukua hatua ya kujitenga na vikao vya bunge, bado ingebaki kuwa uamuzi sahihi bunge kubadili namna ya kuendesha vikao.

Hivi unahitaji ishara gani kuamini kuwa ndani ya bunge kutakuwa na maambukizi ya kutosha tu!

Nina mashaka Tanzania tuna tatizo la kimsingi tusilolijua na kwamba utatuzi wake ni mgumu au sintofahamu isiyo mithilika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mpumbavu sio kila kitu ulete siasa.
Wabunge ni binadamu kama ulivyo wewe,wana haki ya kuishi na usalama wa afya zao.
Hivi Nkamia nae ni Chadema?Au hukusikia maoni yake?
Ndassa na Mahiga ni Chadema?Au hukusikia vifo vyao?
Bado huelewi?Au kwakuwa wewe kazi yako ni kujificha nyuma ya keyboard ukiwa na mumeo anakutomasatomasa hapo kitandani kwenu basi ile raha ya kuguswaguswa unapost chochote tu kulingana na mihemko unayopata hapo?
Binadamu wenzio wako hatarini pale bungeni,sio Chadema sio CCM,ni binadamu wale wote,so acha kuandika upumbavu humu,shenzy type!
 
Mbowe ni mtu hatari sana ukimpinga rejea sumaye alivyotishiwa
Wabunge ni watu wazima, viongozi walioaminiwa na wananchi, wakapewa dhamana ya kuwawakilisha kwenye chombo cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali, wanapaswa kuwa na maamuzi binafsi ya mfano wa kuigwa walio wachaguwa.

Mbowe, kama Mbunge na KUB, na M/Kiti wa Chama Kikuu cha Upinzani, angepaswa kutumia madaraka hayo kuwasilisha hoja yake hiyo bungeni, badala ya kutoa maagizo kupitia vyombo vya habari.

Kwa agizo hilo na njia aliyoitumia, Mtukufu Mbowe ameonesha dharau ya wazi kwa viongozi wenzake, Bunge, Wanachama wa CHADEMA, wapiga kura, na Watanzania wote kwa ujumla. Mbowe, pia ameonesha makucha yake ya udikteta. Yumkini ndiyo maana viongozi wanahama chama CHAKE.

Mtukufu Mbowe, anathibitisha kuwa mtu hatari kwa amani katika Taifa. Kauli na matendo yake ni wazi yanahusika, pasipo shaka sasa, na matukio mbalimbali ya uhalifu ndani ya chama CHAKE km kupotea, kupigwa risasi na hata la maandamano haramu yaliyosababisha kifo cha Akwilina.

Selasini, Mb, wakati akitangaza kukihama chama cha Mtukufu Mbowe amedokeza machache tu ya kumhusu. Tutegemee mengi machafu na maovu ya kutisha kutokea ndani ya CHADEMA na jamii, kwenye uenyekiti wa Mtukufu Mbowe.
 
Back
Top Bottom