Ukiwa na akili zako timamu hauwezi kuamini maneno hayo mbele ya hadhara,je,huyo Mpinzani akishapata Uongozi anapigana na nani?Ukitazama kwa jicho pevu,atakayeleta vita ni yule aliyeshindwa na mpinzani kwa kung'ang'ani madarakani.Tunaposikiliza kauli kama hizi,tupate fursa ya kuhoji,kulikoni wagombea wanaruhusiwa kuwatishia wananchi vita?
Tumechoka kukumbushwa vita vya Libya,Lebanon,Syria au Iraq.Mazingira ya nchi hizo hayashabihiani na yetu hata kidogo.Ukweli usemwe na tuache vitisho.Nani aanzishe vita katika mazingira ya utendaji unaozingatia haki?Watanzania tunafahamika kwa kupenda Amani pale wanapohakikishiwa haki.