Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
Sababu za tishio la kufunga biashara kwa makampuni haya sio sababu halisi kama wengi wanavyozipokea. Ukisoma statements zao, zimeandikwa kimkakati kwamba LATRA wameongeza new charges ya 15%. Seriously?!.
Sio kweli kwamba Serikali imeweka kodi mpya ya 15%. Uhalisia ni kuwa LATRA wamewataka Uber na Bolt wa-charge 15% commision kwa kila trip na sio 20 au 25% kama walivyokua wanafanya.
Kimsingi, madereva wa hizi huduma wamekuwa wakilalamika kukatwa hela nyingi kwa trip (20-25%) na hizi kampuni, hivyo LATRA imeingilia Kati kushusha hizo rates ili madereva wanufaike.
Labda niulize.. Kwani ni mara ngapi abiria ukitumia BOLT/UBER umekuwa ukimsikia dereva analalamika kuhusu malipo? Mara ngapi wamekuwa wakikataa kwenda baadhi ya trips kwa sababu hailipi? Mpaka imekuwa kawaida.
Zinachofanya hizi kampuni ni kuibua taharuki ili Serikali iufyate ziendelee kutengeneza faida kubwa na kuwabana madereva. Ujanja ujanja tu wa kibiashara.
Media zetu nazo..... Au basi!!