Kuna 'misinformation' inaendelea kuhusu Uber/Bolt kufunga biashara Tanzania..

Mkuu naomba kujua hiyo 25% ya bolt au uber nao wanalipa 18% vat ?
 
Mkuu naomba kujua hiyo 25% ya bolt au uber nao wanalipa 18% vat ?
Kwa Uber/Bolt Corporate ambayo ni service wanatoa on credit kwa makampuni wakiwapeleka month invoice inakuwa na EFD yenye QRC c ikionyesha wamelipa 18% imelipwa kwenye total amount kama VAT.
Kwa individual customers ambao ndio wengi I hope TRA wana mifumo yao
 
Kodi wanayotoza TRA kwenye hayo makampuni analipa Dereva katika kila trip. Mfumo umechezewa sana. Na ndiyo maana ukifungua App ya dereva especially kipengele cha Mjumuisho na Mchanganuo wa Mapato, Matumizi na Makato ya Nauli/Malipo aliyopokea dereva kuna Makato ya kodi sehemu 3.
 
Una hasira nao!!!!
Wamenichukiza sana aisee. Hii inchi umasikini sio swala la asili ni swala la watu kutaka tubakie hapa. Tukibadilishana nchi na taifa moja la wazungu mika 10 tu Tanzania haitakuwa hii. Dubai watasubiri.
 
Kwan kuna sehemu wamesema ni lazima mtu kuweka gari katika system ya uber na bolt?! Kama kitu hakina faida achana nacho.
 
Punguza jazba na usiingize siasa,hii ni biashara km biashara zingine so issue ya kodi haikwepek
 
Exactly, hapo ndio uone jamaa Wana haki ya kushusha Hadi 15% kwa kweli.

Angalau makampuni yangekuwa yanatoza hiyo 25% per day. Sio per trip. Ni biashara kichaa.
Watoze per day on what?
 
Wamenichukiza sana aisee. Hii inchi umasikini sio swala la asili ni swala la watu kutaka tubakie hapa. Tukibadilishana nchi na taifa moja la wazungu mika 10 tu Tanzania haitakuwa hii. Dubai watasubiri.
Hiyo ni kweli. Nchi hii wapigaji wengi sana!!!
 
Ulianza vizuri post yako mpaka ulipoanza kutukana na ulivymsifia Magufuli aliyetuaminisha ujinga huku pesa zikipigwa tena sana nyuma ya pazia.
 
Unajua Uber wao wanalipa wafanyakazi wao Pesa ngapi?
 
Sijajua ila hiki nachokwambia ni uhakika
Nafaka hivi hakuna uwezekano wa say LATRA au madereva wakajiunga na kuwa application yao ambayo wataitumia eg hapa Tanzania tu? Kuna kampuni nyingi tu zinaweza ku-design na ku-code app za namna hii japo wakitaka app ya kiwango bora ni lazima waingie gharama na pengine wachukuwa programmers wa nje.
 
Kama app zinazofanya hivi TZ zipo nyingi tu mkuu. Kuwa na app jambo moja kuendesha hiyo biashara jambo lingine. Mkuu hebu fikiri kama mwendokasi tu watu wanalalamika we unadhani Latra ambao wameshindwa tatua matatizo mengi wataweza? Tanzania jambo likishaingia pesa wale mliowachagua kama viongozi nao wanageuka Mungu watu.
 
Ni kweli. Uendeshaji Tanzania ndiyo janga.
 
Masikini siku zote tunanyonywa... tunapenda Cheap sana..

Hizo kampuni pia zinalipa Jengo la Ofisi, Matangazo, Wafanyakazi, Kodi TRA, Leseni, internet services, Servers, Maintenance n.k. ambazo wengi gharama zake hatuzijui.

Huu mzani hauangaliwi kabisa,, tunakomaa kuwaita Wanyonyaji utafikiri hatujawai fanya biashara.
 
Makampuni gani wanatumia Uber/Corporate? Nimeulizwa swali la interview ya kazi. Unaweza ukawa na idea na makampuni yanayotumia Uber/Bolt corporate?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…