covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,355
- 20,792
Kuna mpasuko wa kidini unaanza kunukia Tanzania na ukifuatilia kwa makini utagundua mgogoro huu unaongezeka kila siku.
Cha kusikitisha Chanzo kikubwa ni wanasiasa, wale wale waliofanya makosa miaka ya nyuma hadi tukafika hapa tulipo. Badala ya kujifunza, speed ya makosa imeongezeka maradufu.
Kwa sasa viongozi wa dini wamegawanyika vibaya kila upande unavuta kwake, kila mmoja anapigania ajenda yake, na hakuna sauti ya pamoja kama zamani. Na tukiamua kuyapuuzia haya, muelekeo wa nchi hauko pazuri kabisa. Tusishangae kuona mgogoro mkubwa wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu ukianza kuota mizizi na ukapelekea umwagaji mkubwa wa damu hapa nchini.
Wakati hayo yote yanatokea, wanasiasa wako bize kupigania nafasi, mamlaka na maslahi yao. Kwao, hali ni mbaya kisiasa, hivyo hawana muda wala nguvu ya kusimamia utulivu wa nchi. Kwao mivutano ya dini kwa sasa They take kama advantage kwao ili waendelee kuaminika kwa jamii.
Matokeo yake sasa Viongozi wa dini wameachwa wajitume kivyao bila mwongozo, bila mwelekeo, bila utulivu.
Ninachojiuliza kwanini Serikali imeshindwa kabisa kutuliza hali hii? Joto linapanda kila siku, presha mtaani imefika mbali, na watu wanaanza kugawanyika waziwszi kwa misingi ya kidini na kimadhehebu.
Kwa mwendo huu, taifa linaelekea kugawanyika vipande vipande muda si mrefu, na kama kawaida,wataoumia ni wale wale Masikini, Wasio na mtetezi, Wale wanaotaka tu kuishi kwa amani
Nina wasiwasi sana na hali ya usalama kuanzia sasa na siku za baadae hapa Tanzania.