chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nasikia kuna mradi mkubwa unaofadhiliwa na mataifa ya nje ili kukarabati Shule Kongwe hapa nchini. Mradi huu hutoa pesa kwa ajili ya shughuli hii.
Shule ya Sekondari Nyakato pamoja na Ihungo ni moja ya shule kongwe na hivi karibuni zimezua mjadala. Shule hizi zilipigwa na tetemeko lililoikumba mkoa wa Kagera.
Kuna hoja kwamba pesa za kukarabati shule hizi zilitokana na michango ya rambirambi na pole kwa waathirika, na wakati huohuo mradi wa kukarabati shule kongwe ulikuwa unaanza.
Swali fikirishi:
Je, pesa za kukarabati shule hizi zilitoka wapi? Kwenye mradi wa kukarabati shule kongwe au ni michango ya waathirika wa tetemeko? Kama ni pesa za mradi, za tetemeko zilipelekwa wapi?