Mkuu Kuna swali nataka kuku uliza nilipata ugonjwa peripheral neuropathy wakanipatia nat B pale muhimbili na dawa za kupaka ila mpaka sasa Hali bado 😢😭 naskia ganzi kalii mguuni nipate dawa Gani mbadala wa hiyo nat b
Dawa hua zipo na utameza sana tu. ila changamoto ni kwenye kubaini
chanzo cha tatizo ilo kwanini miguu inakufa ganzi au kuchomachoma mithili ya sindano na kuwaka moto..
Hizo Nat B zinapunguza ukali wa hizo dalili ila sio kutibu chanzo.
chanzo cha tatizo kinaweza kua ni umri wako
Kazi unayo jishugulisha nayo ( usikute wewe n dereva wa malori muda mwingi upo barabarani )
Chakula unachokula na digestion yake kiujumla.
Kupatwa na jeraha linaloweza kusababisha hali hio
Kuugua Magonjwa ya muda mrefu
Unywaji wa pombe kupita kiasi.
Matibabu hua ni kubaini chanzo na kutibu tatizo. Kubadilisha mfumo wa maisha na ulaji wa chakula. Pia wasiliana na wataalamu wa tiba asili pamoja na tiba ya chakula (nutirition) huenda nao wakawa na tiba nzuri kuliko madawa ya kiwandani.piga mazoezi ya mwili kusisimua misuli
#Angle yangu ilikua ni kubaini chanzo cha tatizo hilo na kulitaftia ufumbuzi