Kuna mtu amekutana na issue yoyote ya malipo huko UTT?

Kuna mtu amekutana na issue yoyote ya malipo huko UTT?

SHIGOTTO

Senior Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
156
Reaction score
282
Ndugu zangu nawasalimu kwa jina la serikali ya muungano Tanzania. Nipo kwenye mjadala mzito na mke wangu kuhusu hii mifuko ya UTT.

Tumepata pesakiasi Fulani baada ya KULIPWA fidia na Sasa nimemshauri tuwekeze kwenye bond ya utt, tatizo anatishika kuwa huko ukiweka fedha siku ukizitaka kupata kwako ni mtihani mkubwa naomba kufahamishwa.

Kama Kuna mtu amekutana na issue yeyote ya aina hii huko UTT, msaada tafadhali
 
Mkuu naomba kuuliza niliomba ku repurchase na hela yangu ikakatwa kwenye mfuko toka alhamisi iliyopita ila mpk now bado kwenye account haijaingia,
Kwa uzoefu wako inachukua siku ngapi mpaka hela iingie kwenye acc ya bank? Zimepita siku 3 sasa siioni hiyo hela.
Ni siku tatu za kazi. Ijumaa, jumatatu na jumanne kwahiyo leo jioni au kesho asubuhi itaingia.
 
Ni siku tatu za kazi. Ijumaa, jumatatu na jumanne kwahiyo leo jioni au kesho asubuhi itaingia.
Kwa hiyo mkuu siku 3 za kazi ni tofauti na siku 10 za kusubiria? Niko mfuko wa bond nilituma maombi nikaambiwa nasubiria siku 10 za kazi, siku 10 zikaisha ndio nikakatwa hizo hela kwenye acc yangu ya utt
Kumbe tena kuna kusubiria siku 3 ili hela iingie kwenye bank?
 
Back
Top Bottom