Mkuu bank tunakopa vizuri ila sio kwa Riba wanazotaka wao,mfanyabiashara kama Bakhresa bank zote wanatamani wamkopeshe tena riba ajipangie mwenyewe.
Ukiwa mfanyabiashara level hizo wewe ndio unapanga riba unawambia,mnakaa mezani wanakubembeleza tuongeze kidogo kuna 1 2 3,nk unajifkiria kisha unawambia sawa ntawapa % flani..
wanakupa mkopo maisha yanaendelea,ila level tulizopo sasa hivi RIBA tunapangiwa na bank,yani wao ndio wanakwambia tunataka riba kias flan,unataka wanakupa hutaki pita vile..
Mimi sijafikia level za kuwaendesha mabank,najua Muda utafika nitaweza waendesha hapo ndio nitaanza kukopa sasa,Kina MO kina Bakhresa na wengine uwajuao hawaendeshwi na mabank wao ndio wanayaendesha hayo mabank, ndio mana wengi wao hawatumii bank za TZ wanaweka pesa bank za nnje huko,bongo wanaweka za miradi tu.
Kuna utofauti mkubwa ukikopa wewe bank na akikopa MO, ukiwa ktk level za MO mkopo n mzuri sana maana haukuendeshi bali unauendesha wewe,Bank si kwa kila mtu mkuu, dagaa wote wanaoweka pesa bank ndio wanaofanya bank zina run higher.
Kina Bakhresa wanapewa mikopo bila hata RIBA mzee wanaombwa tu waweke pesa bank,wakitaka mkopo hata wa bilions wanapewa Free, wewe JE umefika huko walipo wao?