Kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana kwa kutumia waganga wa jadi?

Kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana kwa kutumia waganga wa jadi?

Kuna Wakati Maisha yanakua Magumu, Yaani Mpaka Unawaza ata Kwenda kwa Waganga. Hivi Njia Sahihi Nikufanya Nini Maana Hata Mimi Apa Nahitaji Kazi Sana. Ila Namuamini MUNGU Sija Mkatia Tamaa. Msaada jamani Nipo Serious kwa kweli.
 
Achana na hizi kazi za kwenye vijikampuni uchwara vya wachina au wahindi.

Nauliza kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana either serikalini au kwenye makampuni ya kimagharibi na NGO kwa nguvu za witch doctors a.k.a waganga wa jadi?

Kama yupo ebu aje hapa atoe ushuhuda wake ili na sisi tukajaribu bahati zetu huko.

Asante
100% na unaweza kuingia hata bila oral. Nina watu wawili nawajua wametoboa kwenye ile interview yenu ya ......M.O, trust me.
 
Njia Rahisi ya kupata mganga wa kweli
Nenda kijijini huko mbali, ukishuka mwambie dereva bodaboda yoyote akupeleke kwa mtaalamu maarufu. Utafika.

Fika Kijiji chochote mbali huko sumbawanga au mbaya na kigoma fikia Guest kaa siku mbili zoeana na muhudumu muulize mganga maarufu yupo wapi utapata

Achana na waganga wa dar es salaam

Sent from my itel S32LTE using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo ya ulozi yapo wakuu, kuna msukuma mmoja nilikuwa nafanya naye kazi yy Kila ikifika mwezi wa 12 anasingizia miguu inamuuma anaomba ruhusu kazin anaenda kwao huko shinyanga akirud anakuja na midawa tele mingine unakuta ikifika usiku anachanganya kwenye ndoo ya maji Lita 20 anaogea, huwez amin Sasa hivi ndio bosi pale eneo wakat anakuja alikuwa kapuku tu
 
Mawezaje kwenda kwa mganga alfu babdae Tena niende kanisani Tena nakula sacramentari
 
Mawezaje kwenda kwa mganga alfu babdae Tena niende kanisani Tena nakula sacramentari
Mkuu ndo maisha yalivyo hata huyo anayekuongoza kanisani unaweza kutana naye huko kwa maganga ,haya mambo hayana formula
 
Haya mambo ya ulozi yapo wakuu, kuna msukuma mmoja nilikuwa nafanya naye kazi yy Kila ikifika mwezi wa 12 anasingizia miguu inamuuma anaomba ruhusu kazin anaenda kwao huko shinyanga akirud anakuja na midawa tele mingine unakuta ikifika usiku anachanganya kwenye ndoo ya maji Lita 20 anaogea, huwez amin Sasa hivi ndio bosi pale eneo wakat anakuja alikuwa kapuku tu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]noma sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAMNUKUU MWANA JF MMOJA
Nyumba ya mganga na nyumba ya Chifu haipungukiwi ni msemo wa wazee huo. Umemtibu mtu analeta shukrani kwa alichofanikiwa.
Sifa za Mganga wa kweli.
Mganga wa kweli hakutozi hela nyingi kuliko alivyopangiwa na mizimu iliyompa uganga maana uganga wa kweli lengo lake ni kusaidia jamii, unganga ni jadi na lengo lake ni kuisaidia jamii toka enzi na enzi ni bahati mbaya sana kuufanya uganga kuwa dili la kuwaibia watu, hii sio lengo la uganga kwa asili yake.

Uganga wa kweli mara nyingi ni ule unaotokana na kurithi toka kizazi mpaka kizazi sio ule wa kujifunza,ukanjanja, udii na ulozi wa kuwatupia watu mabalaa kwa lengo la waje uwatibu.

Mganga wa kweli lazima atakukurahishishia shida ulionayo na kama imemzidi uganga atakwambia au atakuposti kwa wajuaji zaidi wa shida yako (Waganga wanafahamiana kwa uwezo na nyanja kama walivyo walozi).

Mganga wa kweli atakutibu ili upone ndo akufaidi zaidi kwa shukrani na zawadi na uaminifu wako kwake na ndio faida ya uganga wa kweli. Huyu mganga hutamwacha kamwe kwenye kulingana na alivyotatua shida yako. Kuna jangiri alijeruhiwa na nyati porini nyati alivunja vunja miguu, yule mwamba wenzie walimbeba mpaka kijiji cha jirani huko Katavi kwa mganga. Mganga akawaambia wale wenzake mje mumchukue baada ya wiki tatu muache debe moja la unga. Wenzie waliporudi baada ya wiki 3 walikuta anatembelea fimbo na akapona mifupa na akarudi kwenye ujangiri wake na akipata mnyama lazima apeleke nyama kwa Mganga.

Onyo: Nazungumzia waganga wa kweli sio matapeli wa mjini na mapropesa.

Watu wanaibiwa na wanachanganya sana kati ya Ulozi, Ugagula, Uganga na Mazingaombwe, kiini macho.

MIMI NAANDIKA NA NINA MGANGA WA UHAKIKA
Kama mtu anataka mganga wa uhakika mganga wa Tanga aje pm ilaa aandae kunitumia 5000 Kwa akili ya connection.
Alisikika m Tanzania mmoja akisema Vibora vinagharama Quality is Expensive kama hutaki unataka cheap chukua ya kwenye nguzo utapeliwe.
Nikimtapeli mtu anireport nipigie life ban
Karibuni PM/DM
watu wanaamini uganga hausaidii watu asikudanganye mtu waganga uzunguni ni matajiri sana kama unataka uamini
Ingia TikTok Kuna jamaaa anaitwa DANIEL MACDONALD anaulizaga wazungu matajiri what do you do for a living wengi ni waganga na wale dream tellers watafsiri wa ndoto na conclude
Kwenye maisha kama wewe ni wa kiume usipende sana mtelemko utaponza sehemu zako za kukalia sababu ya njaa.
 
Back
Top Bottom