changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Yaani unanionekana jinsi gani ulivyokuwa unafuata imani ya dini sababu ya uoga. Kwahiyo kwavile naishi ndio kithibitisho cha Mungu kuwa huruma? Kwahiyo ndugu zangu na marafiki zangu waliokufa, na watu wengine waliokufa ni matokeo ya Mungu kutowaonea huruma? Kiumbe yupi ambaye atapata huruma ya milele ya Mungu, maana sifa ya kiumbe hai yeyote ni pamoja na kufa. Kuna watoto wanazaliwa na pia wanakufa, huruma ya Mungu inakuwaga wapi?Shauri yako, MUNGU anakusikia,na kuna siku atakuuliza.Kama kweli MUNGU wetu angekuwa katili kadiri ya maneno yako mimi na wewe tusingekuwepo hadi sasa hivi tukiwa tunachati; MUNGU wetu ni mwenye huruma na upendo mwingi ndio maana anatusamehe pamoja na kwamba tunamkosea sana na mara nyingi.