Kuna mtu anaweza asikupe pesa kwa sababu hana kwa wakati huo lakini akakupa ushauri wenye thamani kuliko pesa uliomuomba

Kuna mtu anaweza asikupe pesa kwa sababu hana kwa wakati huo lakini akakupa ushauri wenye thamani kuliko pesa uliomuomba

Sasa hii comment yako umenifanya nijiulize labda mi na deal with petty issues ndio maana am doing on my own?!!
Hapana mkuu, unaweza kuwa naye mtu mzima mmoja hata kama ni mjomba akawa ni mshauri wako mzuri sana
 
Ni kweli ushauri unasaidia sana, kuna muda unaweza kuwa na jambo linakuumiza kichwa hupati solution kumbe ukishirikisha watu wanakupa ushauri mpaka unajilaumu ulikuwa wapi muda wote kusema yanayokusibu.

Picha linaanza,, kipindi niko shule ya msingi kuna jirani yetu alikuwa na mtoto mdogo wa kike miaka kama mitano hivi lakini pia jirani yule alikuwa na gari (pick up) na shughuli zake zilikuwa za garage.
Jamaa alishamzoesha mwanae mara nyingi akirudi na ile gari nyumbani anampakia anazunguka nae mita mbili tatu then anamrudisha,basi mwanae akazoea hivyo.

Kwa bahati mbaya ile gari ilipata ajali kiasi kwamba ilikuwa haitengenezeki tena, katika kusimulia watu walioenda kumpa pole jamaa yule mwanae akasikia wanavyosimuliana kuwa hana gari tena,,mtoto alimuuliza baba yake yake swali moja tu " baba kwahiyo gari letu sitaliona tena" baba mtu akajibu ndio mwanangu,,,, aisee yule mtoto kuanzia pale akawa mnyonge sana,akawa hali chakula, haongei, haendi kucheza ,yaani yupo tu kama sanamu hafanyi chochote.
Wale wazazi wakajua masihara bwana siku ya kwanza ikapita, Kesho yake dogo alipoamka yakawa yaleyale, hakula chochote wakaleta vyakula vyote pendwa dogo alikuwa anaangalia tu,,soda soda sijui juice dogo hakurespond, mpaka inafika jioni mtoto yuko vile vile ,wakaona watampoteza mtoto kizembe, sasa wakawa wameamua waende hospitali, swali likawa je hospitali wataenda kusema mtoto anasumbuliwa na nini?

Kama bahati kuna jirani mwingine akawa anapita akakutana nao ndio wanatoka ila waende hospitali ,katika salamu na story story wakamsimulia jirani kuwa mtoto ana tatizo, yule jirani akashangaa sanaa na akamvuta baba wa mtoto pembeni akamuuliza unasemaje hili ni tatizo wakati wewe unashinda garage na una marafiki kibao wana magari unashindwa kuazima hata kwa nusu saa umdanganyishie mwanao kweli?
Yaani jamaa alivyopewa tu lile wazo alitoka nduki kwenda kuazima gari, hata nusu haikuisha akawa amepata kufika nalo nyumbani akamwambia mwanae nimenunua gari lingine mwanangu,,,muda huoo huo mtoto akachangamka,akasikia njaa wakampa msosi akala, jamaa akampakia kwenye gari akazunguka nae kidogo mtoto akaridhika kwa 100% akiamini baba amenunua gari nyingine,mpaka leo binti yuko darasa la tano anaamini wana gari hata kama halioni home. Tatizo likawa limetatuliwa namna hiyo ilihali wao kama wazazi hawakufikiria hivyo.

Samahani kwa maandishi mengi ila nimejaribu kugusia tu unaloona kwako ni tatizo kumbe kwa mwingine si tatizo kabisaa.
 
Ni kweli ushauri unasaidia sana, kuna muda unaweza kuwa na jambo linakuumiza kichwa hupati solution kumbe ukishirikisha watu wanakupa ushauri mpaka unajilaumu ulikuwa wapi muda wote kusema yanayokusibu.
Absolutely right...
 
Kuna uzi ulisema unapambana na shida zako then hapa tunaona ulienda kuomba kwa jamaa.
Nilisema ninapambana na shida zangu lakini maji yakizidi shingoni ndio ninaomba msaada tofauti na yule ambaye kila siku kazi yake ni kuomba omba tu mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom