Kuna muda lafudhi zinakuwa zinakata vibe

Kuna muda lafudhi zinakuwa zinakata vibe

Unakutana na mwanamke au mwanaume amevaa kapendeza ananukia marashi kwa mtazamo unakubali kuwa ni full package.

Shida inaanza pale anapoongea unakuta na ile lafudhi yenyewe ya kikabila mpaka unaweza pata wenge kuwa upo kijijini.

Kuongea lafudhi za kikabila doesn't mean kuwa wewe ni mshamba ila kuna kavibe unakuwa umekaondoa just imagine pisi iwe kali afu iongee ile lafudhi ya ebitoke.
Nakuelewa kamanda, nakuelewa. Niliwahi kwenda kufanya kazi flani kwenye mgodi wa makaa ya mawe Tancoal pale Ruanda Songea. Jioni moja nikawa loose kwenye kisenta cha Ruanda pale ikapita pisi... pisi ya kwenda. Nikasema haya si ndo mambo yangu sasa.

Pisi nikaisemesha, ile kujibu kiswahili kimetafunwa na lafudhi ya Kingoni aisee...kuna vibe flani ilipotea ghafla.

Ila kuna lafudhi zingine zinanipaga vibe. Kama manzi za chuga daaaa! Ile lafudhi ya mademu wa chuga inanipaga vibe moja ya hatari.
 
Back
Top Bottom