Kuna muda lafudhi zinakuwa zinakata vibe

Kuna muda lafudhi zinakuwa zinakata vibe

Manyara hapana kwakweli upande wangu.Wote tulioanza kuongea lugha zetu za asili ndiyo tukaja kufahamu kiswahili,tuna mtihani mkubwa upande wa lafudhi.
Manyara wengi wao Kiswahili awajui
Wakubwa lkn kuongea Kiswahili chenga
Kule ni kiiraq tu Sio shulen co mtaan co bar..
 
Sana kuna na wahaya ila nililiona hili kwa wachache. Huyo jamaa anapenda masifa yeye mda wote ni kuongea na kujisifia na ile lafudhi yake
Kwakweli Kagera kwa lafudhi nibaya na inakera zaidi ukikutana na much know halafu aongee kiswanglish, inatia hasira sana
 
Hata wachagga sijui wa wapi wale,huwa wanaongea kwa speed na wakiwa serious,kwa usiye elewa wanachoongea unajua hapa zitapigwa muda si mrefu,gafla unawaona wanaangua kicheko.Kumbe wanapiga story tu.
😂 hao watakua warombo, ukikutana na wale wa ndani ndani huko alafu awe muongeaji sana unaweza ukacheka.
Leo kuna madogo waha walikuja dukani walivyokua wanaongea kiswahili na lafudhi yao nusura nicheke.
 
Du hii ilishawahi kunitokea advance bukoba kwenye ile shule maarufu pisi zilikuwa zinanikubali kimuonekano ila kiswahili kilikuwa cha kisukuma kilinikosesha credit kwa watoto wazuri ,kutokana na unfair comparison kati ya apearance yangu na kiswahili changu ikabidi nichange character nikaacha kuongea sana, kuna siku nilichaguliwa kipindi cha dini nikatoe ushuhuda wangu nikafikiri kuhusu acent yangu ikabidi niseme sina ushuhuda ili nisiongee sana nikajishusha credit
 
Back
Top Bottom