Kuna muda lafudhi zinakuwa zinakata vibe

Nakuelewa kamanda, nakuelewa. Niliwahi kwenda kufanya kazi flani kwenye mgodi wa makaa ya mawe Tancoal pale Ruanda Songea. Jioni moja nikawa loose kwenye kisenta cha Ruanda pale ikapita pisi... pisi ya kwenda. Nikasema haya si ndo mambo yangu sasa.

Pisi nikaisemesha, ile kujibu kiswahili kimetafunwa na lafudhi ya Kingoni aisee...kuna vibe flani ilipotea ghafla.

Ila kuna lafudhi zingine zinanipaga vibe. Kama manzi za chuga daaaa! Ile lafudhi ya mademu wa chuga inanipaga vibe moja ya hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…