Kuna mwalimu mkuu mmoja yupo njiani muda huu, anaenda kwa bosi kujieleza kwanini hawakufundisha Jumamosi hii

Kuna mwalimu mkuu mmoja yupo njiani muda huu, anaenda kwa bosi kujieleza kwanini hawakufundisha Jumamosi hii

Mtumie meseji,kamishna wa elimu,Dr.Lyabwene Mtahabwa.Ilishakatazwa hiyo hali,itakua afisa elimu,alikua kafuata mchepuko wake(ambaye ni mwalimu),eneo hilo,na anataka kulipwa posho.Hapo afisa elimu kafoji tripu,ale posho.Rejea waraka uliosainiwa na Dr.Mtahabwa,ulikataza kabisa.
 
huo ni ujinga,upumbavu,kwa nini muende jumamosi?Je Kuna posho hiyo juma mosi?Sheria za kazi zinakataa !!!mwambie mwalimu wako afanyeujasiriamali ziku za juma mosi
wanaojitambua hawafanyi huo ujinga wa kufanya KAZI NJE na mda wa KAZI,piga KAZI mda wa kazia tu ukiisha kapige mishe zingine,Kwa hali hii lini walimu tutaendesha. Subaru Forester!????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajira ni utumwa
Kuzaliwa duniani ni utumwa, haijalishi umejiajili au umeajiliwa. Kuns mtu kaandika hapa, kuna kituo cha mafuta kimefungiwa, kwa kuto uza mafuta kwa siku tatu, wanatakiwa wajieleze, kwa EWURA wasipoeleweka wanafungiwa mazima.
Nadhani pia unaona akina Mwijaku, Baba Levo, Dotto magari kazi wanazofanya kwa wanaume wenzao, muhimu jali unachoingiza.
 
Wakati naleta mada hii nilijua kuwa mahanithi wapo tu hivyo hujanisumbua bado.

Wasikupe pressure hao mkuu. Hao ndiyo wale nyani wanaoshangilia bandari kuuzwa kama wale washangiliao kuchomwa kwa miti porini.
 
Huruma sana.
Bora hawa wa mjini wazazi tunawapiga kampani kwa mtindo wa pesa ya tution na mitihani.
Au na wizara ya elimu na TAMISEMI tuwape DP WORLD
 
Ndo hivyo jamani!

Hilo ndilo linalotokea sasa hivi tunavyoongea huku mkoani kunakolimwa ufuta na korosho kwa wingi.

Ipo hivi, Ijumaa ya tarehe 01.09.2023 shule zilifungwa kwa mapumziko mafupi ya wiki mbili. Sasa katika shule hiyo walimu walikubaliana kuwa wawapumzishe watoto wote (yaani pamoja na darasa la nne na la saba (ambao wanasoma sana kutokana na kukabiliwa na mitihani) kwa siku mbili (Jumamosi na Jumapili) hadi Jumatatu ili mafunzo yaendelee, wakafunga shule jioni na kutawanyika.

Kumbe Jumamosi afisa elimu msingi kutoka halmashauri (manispaa) alifanya ziara ya ufuatiliaji na kufika shuleni hapo bila kuwakuta wanafunzi wala walimu akafura si mchezo. Akamuagiza chawa wake (afisa elimu kata) amuambie huyo mwalimu mkuu afike ofisini kwake saa mbili kamili siku ya Jumatatu (leo) akiwa na maelezo kamili ya kwanini watoto hawakuwepo shule siku hiyo. Maagizo yakaendelea kuwa kabla ya kwenda huko Jumapili afike kwanza kwa afisa elimu kata nako ate maelezo. La jumapili limepita na sasa mwalimu yupo ofisini kwa afisa elimu anatoa maelezo, imelazimu aache kufundisha kwa leo.

Jinsi anavyosafiri:
Kwa kutumia kamshahara kake

Status ya shule:
1. Wanafunzi 700+ (kuna awali na maalum)
2. Walimu 7 tu
3. Ebm kwa mwezi 300,000

Hali halisi ya maandalizi ya mitihani:
Drs la 4 na 7 wanasoma hadi saa 12 kila siku tangu mwaka huu uanze (nina mtoto darasa la saba hapo). Hakuna mchango, walimu wanajitolea tu.

Inavyokuwa misafara ya maafisa elimu:
1. Wanawekewa mafuta (ufuatiliaji)
2. Wanalipwa posho (ufuatiliaji)

😡😡😡
Hivi kitatokea nini ikiwa siku moja kuna mwalimu akatoa somo kwa kumchaanga makofi afisa elimu fulani kisha kumfungia store ya shule hadi atakapofuatwa na mkurugenzi wake au vyombo vya usalama? Inakera sana.

Muwe na asubuhi njema!
Ualimu na waalimu waheshimiwe. Hata Dkt Magunguli alikuwa mwl ila hata hakuwasaidia kabisa hata kidogo, na sasa top 5 wawili ni waalimu ila ndiyo hivyo
 
Kuzaliwa duniani ni utumwa, haijalishi umejiajili au umeajiliwa. Kuns mtu kaandika hapa, kuna kituo cha mafuta kimefungiwa, kwa kuto uza mafuta kwa siku tatu, wanatakiwa wajieleze, kwa EWURA wasipoeleweka wanafungiwa mazima.
Nadhani pia unaona akina Mwijaku, Baba Levo, Dotto magari kazi wanazofanya kwa wanaume wenzao, muhimu jali unachoingiza.

Ujaelewa, na wala huwezi elewa, hivi unafikiri mimi ningejieleza? Kwani Mwalimu mkuu hana observation ya hali ya wanafunzi wake akaamua wapumzike?
 
Ujaelewa, na wala huwezi elewa, hivi unafikiri mimi ningejieleza? Kwani Mwalimu mkuu hana observation ya hali ya wanafunzi wake akaamua wapumzike?
NImejibu neno, kuajiliwa ni utumwa, utumwa unaanza tu ukizaliwa na kuanza kujitegemea, hivyo hata kwenye sekta binafsi utumwa upo, ndiyo maana mtu unasikia anajieleza, mimi sikupenda kufanya hivi, ila Serikali, watu ama shida imenilazimu kufanya hivi.
 
Sawa. Ni maoni yako lazima yaheshimiwe
 
Binafsi sijawahi kuielewa elimu ya Tanzania kuanzia mifumo yake ya utendaji pamoja na uongozi.

Huwa naona matamko mengi lakini utekelezaji ni ziro kabisa, Kwa mfano huu utaratibu wa kusoma siku za weekend na siku za likizo umetoka wapi?

Kwanini kalenda ya masomo isizingatiwe? Kama kwa mwaka siku za masomo ni 194 kwanini zisifuatwe? Shida ni nini hasa???

Tunatengezeza taifa la hovyo kupita kiasi lililojaa uoga wa kila aina, Yaani viongozi , wazazi na wanafunzi wameshajiaminisha kuwa lazima kusoma muda mwingi eti ndio watafaulu, Huu ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu.

Tuache elimu ya kukariri, tujifunze stadi na ufundi ili tuwe na kizazi imara.

Hii nchi upumbavu ni mwingi sana kwa kweli.
 
Walimu wengine ni sifuri kabisa. Mwalimu mkuu/mkuu wa shule atanipangiaje kazi nje ya siku za kawaida? Nasema atafundisha yeye. Sifanyi kazi ambazo hazipo kwenye azimio la kazi na kwenye andalio la somo, hata akishitaki kwa muajiri huwa sitishiki kwa kuwa nazijua sheria za kazi kulingana na mkataba wa ajira. Sitaki kufanyishwa kazi kiholela na hakuna binadamu mwenzangu wa kuitumia akili yangu vibaya apendavyo. Kama ni kusoma wote tumesoma kila mtu awajibike kwenye kazi zake tuheshimiane.
 
Si walimu wakuu mkiwa kwenye vikao vyenu vya kujipendekeza Kwa Maafisa elimu ndio huwa mnapropose kufundisha hadi Jumapili ili kuongeza ufaulu?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hahaha ili Kulinda ukuu uendelee kubaki na posho ya madaraka iendelee.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi sijawahi kuielewa elimu ya Tanzania kuanzia mifumo yake ya utendaji pamoja na uongozi.

Huwa naona matamko mengi lakini utekelezaji ni ziro kabisa, Kwa mfano huu utaratibu wa kusoma siku za weekend na siku za likizo umetoka wapi?

Kwanini kalenda ya masomo isizingatiwe? Kama kwa mwaka siku za masomo ni 194 kwanini zisifuatwe? Shida ni nini hasa???

Tunatengezeza taifa la hovyo kupita kiasi lililojaa uoga wa kila aina, Yaani viongozi , wazazi na wanafunzi wameshajiaminisha kuwa lazima kusoma muda mwingi eti ndio watafaulu, Huu ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu.

Tuache elimu ya kukariri, tujifunze stadi na ufundi ili tuwe na kizazi imara.

Hii nchi upumbavu ni mwingi sana kwa kweli.
Yaani ni shida mkuu, masomo ya ziada au tuition zinatakiwa kuwa initiative za mwanafunzi mwenyewe kujua kama anayahitaji na atamwomba mzazi amlipie, sasa hii ya kuswaga kila mtoto abaki shule likizo au asome tuition ni kuwanyanyasa hao watoto.​
 
Back
Top Bottom