Kuna mwana CCM atagombea Urais mwaka 2025 dhidi ya Samia Suluhu?

Kuna mwana CCM atagombea Urais mwaka 2025 dhidi ya Samia Suluhu?

Huu uzi ni miongoni mwa athari za miaka 10 ya Kikwete ya kuendekeza usiasa badala ya kujikita kwenye kazi na uzalishaji mali halisi. Wao waliita kukua kwa demokrasia ila uhalisia ilikuwa ongezeko la vurugu, propaganda na ongezeko la vijana wavivu wanaowaza madaraka ya haraka kupitia uanaharakati. K
Ulimsikia Profesa Issa Shivji alivyosema kuhusu tatizo la elimu kwenye nchi yetu? Alisema kuwa tatizo letu kubwa ni watu kuogopa mijadala!!
 
CCM huwa wanachapisha form moja ya urais halafu wanasema wajumbe wamemkubali na kapita bila kupingwa huku wajumbe wanaokitolea mate kiti wanapigwa mkwara mkali.

Rejea kilichofanyika 2020.
 
Uwezo wenu ni mdogo sana kiakili. Mbona swali rahisi sana ila la muhimu? Hajauliza kugombea uenyekiti wa chama chenu chakavu kazungumzia u Rais jee mnaona anatosha? Wewe unakuja na ya Mbowe! Kwani Mbowe ni Rais?
Urais ni wa nchi na kila mtu anaweza kuhoji lakini kwenye chama kama hukubaliani na ukionacho unaachana nacho.
Acheni kutumia vichwa kufugia nywele kijana!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Akiguswa Mbowe unakuwa mkalii wewe uchwara.
 
Njoo tulime huku. Kilimo kinalipa mno, Mhe. Rais kafungua masoko watu wanachangamkia fursa. Hizi hoja zako hazina maana.🙏🙏🙏
Nani kakwambia kuwa kila mtu anatakiwa kuwa mkulima?
 
CCM inasema ina wanachama zaidi ya milioni kumi (10,000,000) nchi nzima. Kati ya hayo mamilioni ya wanachama yupo ambaye anaona Samia Suluhu hatoshi kwenye Urais, hivyo mwaka 2025 atachukua fomu kuchuana naye ndani ya CCM?

Au watu wote hao ndani ya CCM wanaona Samia Suluhu amekamilika kwenye urais wake alioupata kwa mujibu wa Katiba na si kwa kugombea??

Jee asingeupata Urais wake kwa mujibu wa Katiba, Mwaka 2025 wangemuacha agombee peke yake ili arithi nafasi ya Mwendazake John Magufuli au wangempinga?
Mimi nitampinga ndani ya chama.
 
Hakuna shaka samia hatogombea. Achana na chawa kibao hao kina shaka.
Samia hatoshi na yeye analifahamu hilo. Ikiwa watataka kumuweka kama mgombea wa ccm bila kuwapa nafasi wana ccm wengine bila shaka chama kitagawika. Samia hakupita tanuru la mchujo kua mgombea wa ccm kwa hivyo hilo lazima kuzingatiwa.
Hata kiitikadi samia hayuko vizuri. Sio mjamaa na anasujudu wamagharibi kitu hakitaweza kutuletea uwezo wa kujitegemea na maendeleo kwa watu wetu.
 
Jee asingeupata Urais wake kwa mujibu wa Katiba, Mwaka 2025 wangemuacha agombee peke yake ili arithi nafasi ya Mwendazake John Magufuli au wangempinga?
- Jibu ni hapana, kungekuwa na mchakato kama ule wa 2015, uliopelekea kubakiwa na majina matano (5)
'Majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ni Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria) January Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Balozi Amina Salum Ali (Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani)'

Chanzo: BBC
1666095658525.png
 
Back
Top Bottom