Kuna mwanasimba aliyemuelewa huyu Sadio Kanoute?

Kuna mwanasimba aliyemuelewa huyu Sadio Kanoute?

Ni kweli Simba hatuna uvumilivu kwa mambo ambayo ni wazi yanaenda ndivyo sivyo.
Bado sijapata wasaa wa kutosha kumuangalia huyu mchezaji,, hata wachezaji wengine wapya.

Kwasasa siwezi sema chochote.
Mchezaji mzuri haitakiwi umuangalie mpaka mechi kumi. Angalia Samatta EPL walimpa mechi ngapi wakaamua kusema hawana nia naye.
 
Ni kweli Simba hatuna uvumilivu kwa mambo ambayo ni wazi yanaenda ndivyo sivyo.
Bado sijapata wasaa wa kutosha kumuangalia huyu mchezaji,, hata wachezaji wengine wapya.

Kwasasa siwezi sema chochote.
Hi ndilo la msingi kuliko yote.

Watu wanataka mabadiliko ya ghafla...

Yaani mashabiki uvumilivu unawshinda.
 
Sijui kigezo kilichotumika kumleta huyu jamaa Sadio Kanoute.

Wengine watasema alikuwa kiungo bora kwenye mashindano ya CHAN 2019. Lakini huyu jamaa kifupi anachangia kuzamisha sana mtumbwi wa Simba ana bado wanalazamisha kumchezesha. Ni kiungo aiye na kasi na mpira, kumbuka kiungo mkabaji muhimu uwe na kasi kwa mpira wa kisasa.

Haya ndiyo niliyoyaina kwa Sadio Kanoute.
1. Yupo slow sana
2. Sio mzuri kwa mipira mirefu yaani kuhamisha timu.
3. Hana dribbling hawezi kuhold mpira hasa timu ikishambulia au kushambuliwa.
4. Hana commanding power kwa wachezaji wenzake , sio mtu anayeongea ni muda wote yupo kimyaa tu.
5. Passing accuracy yake ni mbovu, nilishuhudia kwenye mechi moja akipoteza pasi zaidi ya tano mfululizo.

Naombeni mnishawishi nimuelewe, mimi binafsi namuona ni mchezaji wa daraja la kawaida sana.
Mchezaji wa ndondo alisajiriwa kwa faida zao akina momomo.
 
Wanasimba tulieni achane pupa...

Wachezaji wote ni wazuri...

Mnaona mabaya tu kwasabu team haiparform...

Mwakajana hakuna aliye ona udhaifu wa Mugaru ila now kila mnaona...so kuweni na subira..

Mambo yanakuja...

Yanga isiwape presha ni team ya kawaida sana.
Upepo umepita sasa nyeti za bata zinaonekana.
 
1. Emmanuel Okwi
2. Onyango
3. Amisi Tambwe
4. Manula
5.Mafisango (RIP)
nk kibaoo
Umeanza kufatilia simba mwaka gani?
Acha uongo mkuu Emanuel Okwi msimu wake wa kwanza alistruggle sana.

Okwi alianza kuonyesha makali msimu wa pili na msimu wa tatu ndiyo akawa wa moto zaidi.

Unazungumzia Mutesa Mafisango katika usajili wake Mafisango alisajiliwa na Mumba Sunzu ulikuwa usajili wa kuziba magepu katika timu ambayo ilikuwa na playing style bila kuondokewa na mchezaji muhimu hata mmoja.

Aishi Manula msimu wa kwanza lawama zetu zote ilikuwa kufungwa long balls japokuwa tulimaliza msimu bila kufungwa lakini alifungwa goli 12 na mbili karibu zote ni long range goals tatizo ambalo ni msimu uliopita ndiyo halikuwepo.

Mchezaji ambaye alikuja kufit kwenye squad from day one mpaka leo ni Sergej Paschal Wawa peke yake.
 
Hivi huwa unaangalia mpira?
Mechi inachezwa unaona ni kanuote na Inonga tu ndio wanaocheza mpira ( mfano dhidi ya polisi).
Kiungo kwenye double pivot unataka awe na kasi aipeleke wapi ya kazi gani?
Huoni kuwa ikitakiwa kudribble anafanya hivyo vizuri kabisa?
Eti mkimya, ulitaka awaje sasa? Awe anapayuka kifaransa humo si watu watamuona chizi.
Alafu unajipambanua kama shabiki wa Simba, Simba ipi unayoshabikia wewe?
 
Kuna mashabiki wa Simba mna mawenge yaani ligi hata mechi kumi hazijafika kila mtu anajidai mchambuzi wa mpira. Kama unahsi kwenye mpira unatakiwa kila siku ucheze vizuri wewe na ushinde basi umepotea. Wapeni wachezaji muda wa kuonesha viwango vyao, mechi nne tuu uvumilivu umewashinda, wenzenu walikaa miaka minne wanataabika lakini bado walishikamana mpaka leo angalau wameanza kuona mwanga.
Mpira una kupanda na kushuka, hauwezi kuwa kwenye peak muda wote.
 
Hivi huwa unaangalia mpira?
Mechi inachezwa unaona ni kanuote na Inonga tu ndio wanaocheza mpira ( mfano dhidi ya polisi).
Kiungo kwenye double pivot unataka awe na kasi aipeleke wapi ya kazi gani?
Huoni kuwa ikitakiwa kudribble anafanya hivyo vizuri kabisa?
Eti mkimya, ulitaka awaje sasa? Awe anapayuka kifaransa humo si watu watamuona chizi.
Alafu unajipambanua kama shabiki wa Simba, Simba ipi unayoshabikia wewe?
Mkuu usiniambie kuwa shabiki wa Simba lazima usifie hii migara iliyoletwa na akina Magori. Haya nimabie huyu jamaa ni mzuri kwa kitu gani? Au unadhani kiungo kazi yake ni kuzuia na mirafuu tu.
 
Mkuu usiniambie kuwa shabiki wa Simba lazima usifie hii migara iliyoletwa na akina Magori. Haya nimabie huyu jamaa ni mzuri kwa kitu gani? Au unadhani kiungo kazi yake ni kuzuia na mirafuu tu.
Mkuu....
Kwa ulivyo ntatutumia nguvu nyingi kukuelewesha.
Naomba ni kuache hivyo hivyo huku nikipendekeza ukajifunze zaidi kuhusu viungo wa kati na majukumu yao.
 
Back
Top Bottom