Kuna namna nyingine ya kupunguza komwe?

Tafuta hela,ukishazipata watu watakuja humu kutuuliza wafanye nini ili wawe na komwe.Mshukuru Mungu kwa kila jambo,alikuumba hivyo kwa sababu na hakuna anachokosea....
Hela ninazo mkuu ila haya mambo ya kuitana komwe wakati nina jina langu ndio yananichukiza mkuu
 
Daah! inaonekana unajichukia sana jinsi ulivyo anyway
vipi ulipata dawa ya kuzuia ile ishu?
 
Komwe, kipara sio kovu wala ugonjwa,, Kuna watu wanakomwe kias kwamba unaweza Sema sola ipo juani! Usiishi kwa kuogopa maneno ya watu, acha Waite watakavyo na jinsi ilivyo siku Zote Jina linalokataliwa zaidi ndio linalotumika zaidi,, jina lisikunyime Amani mzee wangu
 
Ishi Maisha Yako Jikubali
Najikubari mkuu sema kuna watu hawaachi yaan mfano juzi mtu anaongea mimi nasikia anamwambia mwenzie upande wa pili kwamba nakwamba ila usimwambie yule komwe kumbe mimi nawasikia,

Mfano mwingine jana kuna mgeni mmoja alinitembelea sasa kwenye kuulizia ulizia jina watu wakawa wanachanganya akawaambia mtu ninaemtafuta ana komwe hivi ndio wakajua maana mtaa huo mwenye komwe ni mimi wakamwambia aaah yule mwenye komwe ebu nenda nyumba ile pale alipofika kwenye story za hapa na pale anasema alipotea ila ndio ananiambia kwamba nilipowaambia hivyo wakanipa uelekeo nikafika mpaka hapa
 
Sawa asante sana mkuu
 
Jikubali aisee maisha ni yako mbona sisi tuna machogo ila hatuna stress za kipuuzi kama wewe!!
mungu hajakukosea

Sasa punguza hilo komwe uwe tahira
Najikubari mkuu ila kusemwa semwa sasa
 
Dawa ni moja tu.. kulikubali kuwa lipo hapo... Sio ugonjwa huo wala si kasoro
 
Wewe ni WA kike au kiume? Kama ni wakiume umepoteza sifa ya kuwa wakiume
 
Shida moja ambayo unayo, ni kuyapa ubize masikio yako kusikiliza yasemwayo na watu... Acha kuichosha akili... Kuna mambo mengi muhimu ya kusikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…