Kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Mkuu,

Hiyo habari ya Obama kupewa nyumba una source gani?

Wamarekani mambo yao wanaweka mtandaoni. Sheria yao ya mafao ya marais wastaafu hii hapa, haijataja nyumba.

 
Obama alipomaliza muda wake alipanga nyumba Washington ili awe karibu na mtoto wake ambae alikuwa bado yuko High School. Pension ya Rais wa Marekani inakatwa kodi ni sawa na mshahara wa Cabinet Secretary ( around 180000 Usd wakati wa Rais ni around 400000).

Amandla...
 
Hakuna nchi nyingine yenye upumbavu kama huu hapa duniani isipokuwa nchi hii tu ya kufikirika na yenye viongozi ambao vichwani mwao mmejaa konokono
 
Duh! Hata huko Kenya utaratibu wao ni kama wa kwetu kwenye kila kitu ulichotaja?
 
Kule hawana ujinga huo ni CCM pekee wameweka huu utaratibu wa kijinga
 
Jimmy Carter bado anaishi kwenye nyumba yake aliyoijenga mwaka 1960!

Yeye na mkewe walirudi Plains, Georgia, kwenye nyumba yao baada ya utumishi wao kumalizika.

Ni nyumba ya kawaida kabisa.



Na hivi mshahara wa Rais wa Tanzania ni kiasi gani?
 
Hawataki kusema. That is the crux of the issue. Sijui kwa nini wanaufanya siri unless mshahara ni so obscene kiasi kuwa wanaogopa reaction za watu. Haya mapesa tunayoambiwa anatoa kila siku inanifanya nihisi hivyo.
Mishahara ya watumishi wote wa umma inatakuwa iwe wazi with no exception. Pamoja na mapato na assets zao zote. Hii itaondoa hisia za conflict of interest na kuwa wanajitajirisha kutokana na nafasi zao.

Amandla...
 
Duh 🙄 !
 
Ukiingia Google mishahara ya wakubwa wote huko Duniani ipo wazi haifichwi !

Ukweli na Uwazi wa hayati Mkapa uliishia kwenye nini ??!!
Lakini sorry Tunasemaga kila Nchi na sheria zake 🙏🙏 !
 
Ukiingia Google mishahara ya wakubwa wote huko Duniani ipo wazi haifichwi !

Ukweli na Uwazi wa hayati Mkapa uliishia kwenye nini ??!!
Lakini sorry Tunasemaga kila Nchi na sheria zake 🙏🙏 !
Hata Mkapa hakuweka wazi mshahara wake na vyanzo vyake vingine vya fedha!

Amandla...
 
Tz tuna mungu, huyu mungu kitu pekee asichokuwa na access nacho ni kumrudishia mfu pumzi…….

Otherwise vitu vingine vyote anaviweza labda asitake mwenyewe. Turejee kauli ya Ridhiwani, “……isingekuwa busara za Baba yangu….”

Inabaki busara na hekima ya kiongozi husika ili mambo yaende sawa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…