Kuna nini kati ya CHADEMA, Marekani, Ujerumani, Ubelgiji, Amnesty International na Kenya dhidi ya Usalama wa Tanzania?

Kuna nini kati ya CHADEMA, Marekani, Ujerumani, Ubelgiji, Amnesty International na Kenya dhidi ya Usalama wa Tanzania?

Maneno demokrasia, haki na uhuru ni maneno yanayoweza kujenga au kuibomoa taifa. Kila tunapoyaongelea tutafakari maendeleo ya mtanzania na uzalendo kwa nchi yetu

Mungu ibariki Tanzania
Demokrasia kwao is just a word, a stepping-stone ya kutimizia malengo yao yeye tashwishwi. Kama ambavyo mtu anaweza kulebo package ya sumu with the word "asali tamu kutoka Tabora!" Halafu hawa jamaa ndio wametufundisha ule msemo Sumu haionjwi. Watanzania wametekeleza hicho kivitendo kwa kukataa kabisa kwenye ballot box kuonja sumu HIYO.
 
Historia ni mwalimu mzuri, viongozi wa Africa tangu Mkwawa,Mirambo nk had,Mugabe ,M7 na jiwe hawajawahi kujali wananchi wala maslahi ya wananchi wao.hua wanaangalia matumbo yao

Umepatia kwa kiasi kikubwa sana. Historia ya Afrika ikiandikwa upya kwa kuzingatia ukweli tu itashangaza wengi.

ISIPOKUWA ipo mifano ya waliotelekeza matumbo yao na kujitolea kwa ajili ya wananchi wao. Kwangu mimi, niliye na uhakika naye ni JK NYERERE. Huyu alijisahau kabisa na familia yake. Alitaka maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote
bila ubaguzi.

TATIZO lake kuu hakutaka kabisa mawazo mbadala. Alichukulia kama usaliti. Hakutaka kabisa upinzani akiona utamchelewesha kufanya mema aliyokusudia. Mambo yakawa: zidumu fikra sahihi za mwenyekiti! Makosa kibao ya kimkakati yakafanyika hadi aliponyosha mikono juu 1984 na kuachia ngazi.

Legacy aliyotuachia ndio hii ya jinamizi la chama dola minus nia ya dhati ya kujali wananchi. Alisema mwenyewe: wamechukua mabaya yetu yote na kuyaacha mazuri!
 
Wakuu,

Hili ni bandiko la swali ili kupata uelewa mpana kuhusiana na taswira mpya wanasiasa wa Tanzania na washirika wao wanavyoonesha katika siku za hivi karibuni.

Je, kuna uhusiano gani wa ziada nje ya utaratibu wa kawaida kwa nchi tajwa hapo juu na shirika mojawapo la haki za binadamu na chama kinzani chenye viongozi machachari zenye harakati hasi?

Je, sio muda muafaka kurejea mfumo wa usalama wa nchi na kurekebisha baadhi ya mambo ili kudhibiti mbinu chafu za kijasusi zinazoendelea hivi sasa kwa kutumia watu kutoka miongoni mwa waTanzania wenyewe ama kwa kujitambua au bila kuelewa kutokana na uerevu unaotumika kupandikiza hadaa kwa ulaghai uliobobea (mercenary hoodwink approach)?

Wajuvi wa masuala ya kijasusi tufumbueni macho tubaini mwelekeo ulio sahihi kwa mustakhbari wa Taifa.
Mataifa yanaonesha hasira za udharimu,
Bado Mungu tu kuonesha hasira zake kwa wadharimu. Tujipe muda!!!
 
Tanzania ni nchi ya ajabu. Ina watu wa ajabu wanaofanya mambo ya ajabu mno. Subiri siku moja utayaona maajabu yake mchana; kuzimu hakuna nyota.
Historia ni mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki wa Afrika
Zinanufaika Hadi Kesho kutwa na Africa kwa kuwaondoa viongozi wa kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao.
 
Haya mashirika ya umoja wa Mataifa yaliundwa kurudisha ukoloni Afrika. Ndio hivyo yanawatetea vibaraka wao wanaowasaidia kuurudisha ukoloni Afrika.

Hapa Tanzania wameshindwa kwa aibu kubwa sasa wanajaribu hii mbinu ya kuchutama kuficha aibu yao. Ila nayo itashindwa.
 
Umepatia kwa kiasi kikubwa sana. Historia ya Afrika ikiandikwa upya kwa kuzingatia ukweli tu itashangaza wengi.

ISIPOKUWA ipo mifano ya waliotelekeza matumbo yao na kujitolea kwa ajili ya wananchi wao. Kwangu mimi, niliye na uhakika naye ni JK NYERERE. Huyu alijisahau kabisa na familia yake. Alitaka maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote
bila ubaguzi.

TATIZO lake kuu hakutaka kabisa mawazo mbadala. Alichukulia kama usaliti. Hakutaka kabisa upinzani akiona utamchelewesha kufanya mema aliyokusudia. Mambo yakawa: zidumu fikra sahihi za mwenyekiti! Makosa kibao ya kimkakati yakafanyika hadi aliponyosha mikono juu 1984 na kuachia ngazi.

Legacy aliyotuachia ndio hii ya jinamizi la chama dola minus nia ya dhati ya kujali wananchi. Alisema mwenyewe: wamechukua mabaya yetu yote na kuyaacha mazuri!
Kuna mada naifanyia utafiti ntakuja nayo hapa kabla ya krismas itahusu kufeli kwa itikadi ya mwalimu na kubwa zaidi ndani yake ni kuwa nyerere hakuwahi kujua ukweli juu ya ujamaa badala yake alitaka kuufanya ujamaa ambapo hata wasoviet hawakuwahi kuupenda
 
Maneno demokrasia, haki na uhuru ni maneno yanayoweza kujenga au kuibomoa taifa. Kila tunapoyaongelea tutafakari maendeleo ya mtanzania na uzalendo kwa nchi yetu

Mungu ibariki Tanzania
Demokrasia= Uhuru +Haki ,je wewe hupendi haki?
Hupendi kuwa huru?
 
Historia ni mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki wa Afrika
Zinanufaika hadi Kesho kutwa na Afrika kwa kuwaondoa viongozi wa kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao.
Hongera kwa kuliona hilo, kwa mtu anaejua historia ya Wabeligiji walichokifanya Kongo hawezi hata kuwapa neno lolote la kuwakaribisha Wabeligiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mada naifanyia utafiti ntakuja nayo hapa kabla ya krismas itahusu kufeli kwa itikadi ya mwalimu na kubwa zaidi ndani yake ni kuwa nyerere hakuwahi kujua ukweli juu ya ujamaa badala yake alitaka kuufanya ujamaa ambapo hata wasoviet hawakuwahi kuupenda
Excellent. Fanya hivyo mkuu. Nilisoma kuwa Nyerere alihojiwa sana kuhusu huo "ujamaa" anaoutekeleza Tanzania ni nini hasa? Inasemekana mara zote alikuwa akikwepa kujibu kama ndio "socialism" au "communism" kwa kiingereza. Yeye alikuwa anachanganya vigezo vya democracy, socialism, communism na dictatorship kwa kadri inavyomkalia vyema na kudai "ujamaa ni ujamaa" tu; ni mfumo wa Kiafrika usio tafsiri kwa lugha nyingine!

Ili kumpa support, Warusi na Wachina walitaka awe wazi kuwa anajenga kitu kati ya ujamaa na ukomunisti hasa alipolazimisha uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa. Hivyo walimtahadharisha aache ndoto za kufikiri atajenga huo ujamaa kwa kutegemea "imani" ya wananchi. Sharti nguvu ya dola itumike full time. Lakini yeye aliamua kujificha kwa vile alikuwa pia anataka uhusiano mzuri na mataifa ya magharibi hasa nchi za scandinavia. Ubepari hakuutaka kabisa na kwenye socialism hakupenda demokrasia ya vyama vingi. Alipenda zaidi ukomunisti wa China lakini eti asijulikane dikteta! Ndio sababu ya kudai ujamaa ni wa kipekee! He was trying to be clever.
 
Fanyeni haki, otherwise ICC nako inaingilia game muda si mrefu
we nae huchoki tu
toka kampen upo na kusifu ni yeye ni yeyey haoo ulipo hata sera na ilan yako huijui umekalia kelele tu icc unapajua wewe au umekaalia kiibodi waria.tu
 
Swali: Kuna nini nyuma ya Pazia kati ya CHADEMA, Marekani, Ujerumani, Ubeligiji, Amnesty International na Kenya dhidi ya Usalama wa Tanzania?

Jibu: CHADEMA walikua wawakilishi wa Marekani, Ujerumani, Ubeligiji, Amnesty International na Kenya kwenye bunge la Tanzania sasa wawakilishwa wametaharuki kukosa uwakilishi waliouzoea
Umejitahidi mrembo angalau umepata ziro (0)
 
Historia ni mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki wa Afrika
Zinanufaika hadi Kesho kutwa na Afrika kwa kuwaondoa viongozi wa kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao.
Hayo ni mapambio ya kina Kwame Nkruma, kila zama na kitabu chake. Mhutu must go, wala hana uzalendo, zaidi Sana Ni muuaji, katili, asiyefuata katiba. Amegeuza ikulu kuwa pango la wanyang'anyi.
 
Historia ni mwalimu hizo Nchi zote zilizomsindikiza Lissu hazijawahi na hazitowahi kuwa Rafiki wa Afrika
Zinanufaika hadi Kesho kutwa na Afrika kwa kuwaondoa viongozi wa kiafrika wenye Uzalendo na waafrika
Kwa kuwatumia waafrika Kama Lissu kufanikisha matakwa yao.
Lissu hata wakimweka lazima ataondolewa tu kwa unaharakati wake ule!! Haweziongozi nchi hata miaka miwili! No way!
 
Back
Top Bottom