Kuna nini mpaka siku hizi ndugu hatutembeleani?

Kuna nini mpaka siku hizi ndugu hatutembeleani?

Na ajabu ya siku hizi Rafiki anaweza kuwa karibu yako kuliko ndugu yako...
Hili ni hakika 100%

Yaan siku hizi ule msemo wa undugu si kufanana ,ndio watu tunauelewa sasa.

Lkn sio kwamba, watu wengi tunapenda kujionyesha wenye upendo kwa watu wambali ??? Hali inayofanya tuwe mbali kiupendo nandugu ??
 
Siwezi kusema ndiyo au hapana...
Nadhani hata ndugu kuna baadhi siyo wote mnaweza kuelewana..

Maana yake ni nini? Marafiki tunaokuwa nao ni wale tumetokea kuelewana, wanatuonesha Upendo nasi tunawaonesha Upendo.. Mwisho wa siku kunakuwepo Ukaribu ambao hata kwa ndugu hauwezi kuwa hivyo.
 
Hili swala la mfumo wa maisha kubadilika kwenye hizi zama tayari zishaelezwa na mwandishi nguli mmoja anaitwa alvin toffler.
Screenshot_20210507-161720.jpg
 
Hivi wakuu nanyie mnaona kama mimi au?

Mbona kama ile Tamaduni yetu ya kutembeleana haipo tena.

Unajua ile tunakua, ilikua unasikia..Likizo hii tunaenda kwa Shangazi..kwa Baba mdogo. Kwa Mjomba... Kwa Bibi ...n.k

Lakini siku hizi hii kitu haipo

Au Mitandao yakijamii imechukua nafasi...yaan ukiona picha ya Ba mdogo kapost, unalike, unakoment.. Imeishaaa hiyooo

Au ukiona status yake wasap... Imeishaaaaaaa hiyo... Ndio salamu, ndio kujuliana hali?.
100%
 
Watu wa Dar ndio wamesababisha yote haya yaani ukienda unasimagwa na vimiogo vya mia mbili wakati huku mkoani tunakula ndoo nzima
 
Umenifumbua macho..hapa inshu ni Upendo yaan upendo umetwaliwa na Utandawazi.

Nikweli ijapokua tu bize na maisha, ila tungekua na upendo, ubize usingekua kitu.

Lkn ,si Simu zipo bana tunapigiana tu inaisha?

Yaan we ubebe familia yako nzima unitembelee??[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Moja kati ya matokeo mabaya ya utandawazi ni kutuondolea upendo ndugu yangu.

Zamani tulikuwa tunakula kwa pamoja,sahani moja bakuli moja.hamuwezi kuanza kula kama fulani hajafika mezani.lakini sasa hivi chakula kikitengwa mezani kila mtu anajikatia na kuondoka zake.ikitokea kama familia bado inaule utaratibu wa kusali pamoja wakati wa kula basi kwa kujivuta sana watakaa kwa pamoja kusali.Vinginevyo tumeletewa ubinafsi wa kiwango kikubwa mno..kila mtu anajikatia chakula chake kwenye sahani hazungumzi na mtu bali huzungumza na simu tu🥺🥺

Utandawazi umekuja sasa na sio kwamba hatutaki kula sahani moja na ndugu zetu..,hapana tunataka sana lakini ukifikiria mkononi mtu anakucha kama ngiri mikono yote na unawaza mikono hiyo hiyo inaenda chooni..🥺🥺ni huzuni kwakweli.

Tukija kwenye simu..bado mwisho wa siku nitazunguka kuelezea weeee lakini nitarudi pale pale..utandawazi ni mzuri lakini matokeo yake ni kutulete ubanafsi na kutuondolea upendo.🥺🥺
 
Hakuna cha ubusy wala nn.
Mtindo wa maisha wa sahv ndio chanzo watu tumeelekeza ukaribu wetu kwenye social networks kuliko mawasiliano ya ana kwa ana tukiisi vimepitwa na wakati
Nikweli mkuuu..nahii imefanya watu mahusiano ya karibu kupungua kabisaaa

Kila mtu anabeba matatizo yake
 
ukiumwa au kuuguzwa ndio umuhimu wa ndugu,hao marafiki watarara mbere. Shift za kuuguza.
Hapa sasa, ndo unauona umuhim wa Ndugu

Ndugu ataacha mambo yote...lkn kikwel ndugu mwenyewe ni Baba au Mama au dada au kaka yako.
 
Nimesikitishwa sana na hii mada.

Nami piaa nishawahi uliza mzee mbonq ndugu. Zetu saivi hawatutembeleii kama zamani.

Zamani nlikuwa naona ndugu wakitoka kijiji kimoja hadi kingine kwa baiskeli kuja kututembeleaa lakini saiv hapana.

Licha ya kuwa usafiri umekuwa nafuu na gharama nafuu lakini wapi.

Unaweza kuona unakaa na ndugu zako wa damu mji mmoja na hata msitembeleane.

Perhaps ndo unabii unatimia kuwa cku za mwisho upendo wa ndugu utapoaaa.
 
Siku hizi salamu ni kule status nitumie hiyo sister. Maisha yanaenda kasi mno likizo tulikuwa tunaenda kwa bibi, mjomba, mama mdogo. Lakin siku hizi watoto wanaenda tuition likizo. Udugu umebaki kama historia. Upendo wa kweli umepotea ndugu zako wamebaki wale unaokutana nao kila siku na mkajenga mazoea
 
Nimesikitishwa sana na hii mada.

Nami piaa nishawahi uliza mzee mbonq ndugu. Zetu saivi hawatutembeleii kama zamani.

Zamani nlikuwa naona ndugu wakitoka kijiji kimoja hadi kingine kwa baiskeli kuja kututembeleaa lakini saiv hapana.

Licha ya kuwa usafiri umekuwa nafuu na gharama nafuu lakini wapi.

Unaweza kuona unakaa na ndugu zako wa damu mji mmoja na hata msitembeleane.

Perhaps ndo unabii unatimia kuwa cku za mwisho upendo wa ndugu utapoaaa.
Kwa hakika mkuu nakubaliana nawee 100%
 
Short and clear na kwamba upendo umetoweka, na aliyebaki na upendo akitembelea wenzake huonekana anajipendekeza hivyo naye huamua kuacha ili kubalance shobo, mwisho wake kila mtu na lake.

Siku hizi hata majirani hawasalimiani wala hawafahamiani hasa mijini, kila mtu anatoka na kuingia kwake labda afe mmoja ndio watu hujitokeza baada ya kusikia kwaya inanguruma nyumba ya pili.
 
Back
Top Bottom