Kuna nini mpaka siku hizi ndugu hatutembeleani?

Wenzetu wamangi huwa wanasema kuwa usilalamike kuwa hautembelewi na ndugu Bali lalamika hauna hela. Wewe kuwa na hela ndugu zako watapishana nyumbani kwako Kama hospital.niliisikia kwa redio boma fm nikiwa naishi pale Dorcas kwa mama Macha
 
Hii haijakaa sawa kuna watu wana hela na hawatembelewi
 
Tutafute pesa mkuu ukiwa huna pesa hata hao ndugu ukienda kuwatembelea wataona kero.Na wengine wanapina undugu kwa kuangalia status yako ya kimaisha ukiwa huna kitu hata kukuuliza hali kwenye simu pengine watashindwa lakini ukiwa upo vizuri kiuuchumi huko si wa kuuuliza hali.
 
Ni kweli mfumo wa maisha umebadilika, kutokana mfumo wa kibepari, ila ukiwa tajiri hukosi ndugu masikini wa kuja kukutembelea mara kwa mara na kuomba waishi kwako
 
Jirani yako ndio rafiki na ndio ndugu yako. Maisha yanabana kwa ugumu na pia majukumu ya kazi nayo hayana mpangilio unaoeleweka. Walioajiriwa wako kazini hadi siku zinazotakiwa kuwa ni za mapumziko, inapotokea anapata mapumziko, basi hana nguvu na muda wa kwenda kwa mtu, bali kupumzika alipo au ni muda huo atautumia kufuatilia mambo yake binafsi na sio kutembelea ndugu na jamaa.
 
Wenzetu wamangi huwa wanasema kuwa usilalamike kuwa hautembelewi na ndugu Bali lalamika hauna hela. Wewe kuwa na hela ndugu zako watapishana nyumbani kwako Kama hospital.niliisikia kwa redio boma fm nikiwa naishi pale Dorcas kwa mama Macha
Hahah sawa mkuu wacha tuzichange.

Lkm sasa, mbona wenye hela hata wao hawatembelei ndugu zao?
 
Sawa sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…