KERO Kuna ongezeko kubwa la makato katika huduma ya fedha kwa simu

KERO Kuna ongezeko kubwa la makato katika huduma ya fedha kwa simu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nimefanya transaction kwa mobile phone. Nimetoa kwa wakala na hichi ndicho kilichonistua....
Salio lako jipya ni TSh xxxx. Umetuma pesa kwa Wakala - xxxxxxx xxxxxx kiasi TSh 20,000. Jumla ya Makato TSh 2,156. (Ada TSh 1,850, Tozo TSh 306), VAT TSh 329. Kumbukumbu No.: xxxxxxxxxxx. 13/08/25 19:58. Furahia Punguzo kubwa la bei unapofanya miamala....

Hivi TRA wanatuona sisi raia kama mazuzu au nini hiki wanachokitafuta kwetu?

Wizara ya Fedha, huu mchezo ni wizi na siyo haki
Mkuu unawalaumu TRA buuuure na sio sawa!! Waziri wa fedha - mbunge wa CCM ndiye aliyependekeza kichomi hiko kwenye Bajeti na bunge lenye wabunge wa CCM asilimia 99.9 likapitisha unanimously!!! Hapa, alaumiwe waziri, spika na Bunge!!!
 
Kujenga nchi ama kulipa madeni ya Hela ambazo CAG anasema zaidi ya Trilioni 1.8 zilipotelea kusikojulikana?

Kama Hela za Kodi ndizo zinajenga nchi haya madeni yanaongezeka kwa sababu gani?
Kukopa ni suspended tax, badala ulipishwe kodi leo ikulemee, serikali inakopa unakuwa unalipa kodi kidogo kidogo
 
Nimefanya transaction kwa mobile phone. Nimetoa kwa wakala na hichi ndicho kilichonistua....
Salio lako jipya ni TSh xxxx. Umetuma pesa kwa Wakala - xxxxxxx xxxxxx kiasi TSh 20,000. Jumla ya Makato TSh 2,156. (Ada TSh 1,850, Tozo TSh 306), VAT TSh 329. Kumbukumbu No.: xxxxxxxxxxx. 13/08/25 19:58. Furahia Punguzo kubwa la bei unapofanya miamala....

Hivi TRA wanatuona sisi raia kama mazuzu au nini hiki wanachokitafuta kwetu?

Wizara ya Fedha, huu mchezo ni wizi na siyo haki
Chadema ni kama hamuaminiki Kwa uzushi Kwa sababu Toka July 2025 Serikali imeshusha makato haya ya kwako umeyatoa wapi?

Zamani ukitoa Laki lazima buku 5 ibakie lini Kwa Sasa ni chini ya buku 3

Kwenye ATM ndio kabisaa makato ni kiduchu.

Mwisho Serikali imeshusha VAT kutoka 18% to 16% Kwa miamala ya simu Sasa wewe huu utapeli umeutoa wapi?
 
We punguani kweli,kodi inatosheleza bajeti!?.. halafu mapunguani ndiyo mna kelele
Kama haitoshelezi bajeti kwa nini Kodi inayopatikana inafujwa kila mwaka kwa matumizi ya hovyo?

Halafu umetoa mfano wa Kenya. Leo CCM mnaona Kenya ni ya kutolea mfano😳

Kenya na Tanzania umeangalia Demografia Yao, umeangalia mfumo wao wa uzalishaji na ajira, umeangalia jinsi walivyoshajiisha (Modernized) biashara ya Kilimo na kuwa ajira rasmi?

Unajua Tanzania watu walio kwenye ajira rasmi ni kama 5% tu ya watu wote? Sasa utakusanyaje Kodi kama hujarasmisha ajira?

Au umesahau/hujui kama MKURABITA lengo lake lilikuwa ni hilo la kurasmisha biashara ili kuongeza wigo wa kodi lakini kama kawaida ya CCM mradi ukaishia kwenye semina na warsha bila ya utekelezaji?

Unajua "vitambulisho vya wamachinga" lilikuwa ni wazo la TRA kurasmisha wajasiriamali wadogo ili walipe Kodi lakini vikageuzwa jambo la kisiasa na Magufuli hatimaye likafia njiani na kujaza watu mabarabarani nchi nzima?

CCM acheni kufanya watanzania ni wajinga.
 
Back
Top Bottom