Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk

Haya mapepo hutembea na vizazi mpaka cha tatu ama cha nne.. Unapoona kwenye familia yako kuna dalili za mojawapo kati ya hayo fanya hima lisisambae na kuathiri wengine.

Kuna ujumbe uliotoka Twitter unaoutaarifu uma kuhusu binti mmoja aliyefariki Morogoro na mwili wake uko mochwari. Hana ndugu ama kwa lugha nyingine ndugu zake hawajulikani ni akina nani.

Kilichonifanya niandike mada hii ni marehemu wakati wa ugonjwa wake akiwa kalazwa hospital kusema hana wazazi (haikufafanuliwa kama ni marehemu ama hajawahi kuwajua ama vinginevyo)

Cha kuumiza zaidi ni kwamba naye kafa kaacha watoto wadogo wawili.. Ni wazi hao watoto wana baba zao/yao lakini hawajulikani walipo. Inaumiza mno kwamba nao watakua katika mkondo wa mama yao.. Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!

Ni maisha ya namna gani yanawasubiri hawa malaika? Mama kabla ya kifo kasema hana wazazi japo kataja alikotokea! Vipi kuhusu ndugu? Vipi kuhusu baba wa watoto?

Itakuwa faraja kubwa kama nduguze watajitokeza na kumchukua marehemu wakamzike na kuwachukua watoto wakawalee. Upendo hawatapata kama wa mama lakini at least watajulikana asili yao ili nao wasijekuja kusema huko ukubwani kwamba hawana wazazi wala ndugu[emoji25]

Kuna familia zina laana ya asili

Upungufu wa kinga za kiroho

IMG-20230416-WA0070.jpg

So tufanyeje Mkuu Ili tufukuze hayo Mapepo?
Ni muhimu sana kufanya vetting ya kutosha kwenye kutafuta mwenza mwenye background yenye afya kiroho kwenye familia atokayo ili kuweza ku dissolve hiyo hali.. Lakini hii ni njia mojawapo tu
Hujawahi kuona kwenye familia yenye shida tangu kwa mababu, baba anachepuka na kuzaa mtoto anayekuwa tofauti na wengine na kuja kuwa mkombozi wa familia ama akawa kimeo
 
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk

Haya mapepo hutembea na vizazi mpaka cha tatu ama cha nne.. Unapoona kwenye familia yako kuna dalili za mojawapo kati ya hayo fanya hima lisisambae na kuathiri wengine.

Kuna ujumbe uliotoka Twitter unaoutaarifu uma kuhusu binti mmoja aliyefariki Morogoro na mwili wake uko mochwari. Hana ndugu ama kwa lugha nyingine ndugu zake hawajulikani ni akina nani.

Kilichonifanya niandike mada hii ni marehemu wakati wa ugonjwa wake akiwa kalazwa hospital kusema hana wazazi (haikufafanuliwa kama ni marehemu ama hajawahi kuwajua ama vinginevyo)

Cha kuumiza zaidi ni kwamba naye kafa kaacha watoto wadogo wawili.. Ni wazi hao watoto wana baba zao/yao lakini hawajulikani walipo. Inaumiza mno kwamba nao watakua katika mkondo wa mama yao.. Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!

Ni maisha ya namna gani yanawasubiri hawa malaika? Mama kabla ya kifo kasema hana wazazi japo kataja alikotokea! Vipi kuhusu ndugu? Vipi kuhusu baba wa watoto?

Itakuwa faraja kubwa kama nduguze watajitokeza na kumchukua marehemu wakamzike na kuwachukua watoto wakawalee. Upendo hawatapata kama wa mama lakini at least watajulikana asili yao ili nao wasijekuja kusema huko ukubwani kwamba hawana wazazi wala ndugu[emoji25]

View attachment 2590664
Thanks bro well composed with sustainable family reconstruction 🙏🙏🙏 societal revitalization is very important amidst such recurring fishy scenarios.
 
Kuna vetting huwa inafanyika kwa mtu anayetaka au anayeteuliwa kwenye nafasi nyeti serikalini.

Kuna baadhi ya familia ukitaka kuingia lazima ufanyiwe vetting ya kutosha, usipokidhi vigezo huingii kwenye hiyo familia ama kwa kuoa au kuolewa....

Na wakuu wa koo/familia wako makini na hilo lengo ni kutopoteza mali na kuingiza mipenyo itayowatafuna kama magonjwa nyemelezi, umaskini, laana, ukichaa/kurukwa na akili, ulevi n.k.
 
Hiki ndicho walichokuwa wanakifanya mababu zetu zamani.. Unaweza kukataliwa ndoa kwasababu ya background ya familia
 
Yeah, kuna kila sababu na haki kwa watu kulinda watu wao kutokana na wasiojulikana na wakijulikana wana mawaa shurti kuwaweka mbali na watu wako wa karibu.

Kujichanganya na kama mbalimbali kumeharibu na kuvuruga mipango ya wengi ya maendeleo.

Unatafutiwa mke/mume unachaguliwa ujuzi wa kuwa nao kujkendesha kimaisha, unaandaliwa kujitegemea na kuinua wengine .......
 
Back
Top Bottom