Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk

Haya mapepo hutembea na vizazi mpaka cha tatu ama cha nne.. Unapoona kwenye familia yako kuna dalili za mojawapo kati ya hayo fanya hima lisisambae na kuathiri wengine.

Kuna ujumbe uliotoka Twitter unaoutaarifu uma kuhusu binti mmoja aliyefariki Morogoro na mwili wake uko mochwari. Hana ndugu ama kwa lugha nyingine ndugu zake hawajulikani ni akina nani.

Kilichonifanya niandike mada hii ni marehemu wakati wa ugonjwa wake akiwa kalazwa hospital kusema hana wazazi (haikufafanuliwa kama ni marehemu ama hajawahi kuwajua ama vinginevyo)

Cha kuumiza zaidi ni kwamba naye kafa kaacha watoto wadogo wawili.. Ni wazi hao watoto wana baba zao/yao lakini hawajulikani walipo. Inaumiza mno kwamba nao watakua katika mkondo wa mama yao.. Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!

Ni maisha ya namna gani yanawasubiri hawa malaika? Mama kabla ya kifo kasema hana wazazi japo kataja alikotokea! Vipi kuhusu ndugu? Vipi kuhusu baba wa watoto?

Itakuwa faraja kubwa kama nduguze watajitokeza na kumchukua marehemu wakamzike na kuwachukua watoto wakawalee. Upendo hawatapata kama wa mama lakini at least watajulikana asili yao ili nao wasijekuja kusema huko ukubwani kwamba hawana wazazi wala ndugu[emoji25]

Kongole mkuu.
Kuna pepo limoja sijui hata liitweje; labda liitwe pepo la kiburi na dharau.
Unaweza kumkuta mtu anazo changamoto nyingi lakini hubahatika kupata Ushauri, Maoni/Maonyo kutoka kwa Jamii na watu mbalimbali wanaomzunguka; lakini kutokana na pepo lililotamalaki kwake yy hupuuzia, hubeza na kudharau hadi iwe yamemfika kama yote.
 
Hilo ni pepo majnuni.. Shida kama zote lakini kiburi na dharau asilimia 100
 
Unapopata mchumba usiharakie ndoa chukua muda wa kutosha kuichunguza familia yake mpaka huko kijijini.. Maana unaweza kuikuta hapa mjini mambo safi kumbe huko kijijini kwenye mashina na mizizi hakufai
Na ukifanikiwa kupata mwenza sahihi.. JICHUNGE NA NGONO zembe.. Ngono imeharibu mengi

Kingine ni mahusiano ya kifamilia, ndugu na ukoo.. Jihadhari mno na mafarakano.. Kuna majanga huanzia huko.. Upendo na kusamehe huokoa mengi, visasi na mifarakano huzalisha mengi
Yan tufanye ngono lakin siyo zembe na wenza sahihi.
 
Ni muhimu sana kufanya vetting ya kutosha kwenye kutafuta mwenza mwenye background yenye afya kiroho kwenye familia atokayo ili kuweza ku dissolve hiyo hali.. Lakini hii ni njia mojawapo tu
Hujawahi kuona kwenye familia yenye shida tangu kwa mababu, baba anachepuka na kuzaa mtoto anayekuwa tofauti na wengine na kuja kuwa mkombozi wa familia ama akawa kimeo
Vipi ikitokea Kama wewe/ Mimi ndiyo Nina shida,na siyo huyo mwenza. Najinasuaje mkuu?
 
Unapopata mchumba usiharakie ndoa chukua muda wa kutosha kuichunguza familia yake mpaka huko kijijini.. Maana unaweza kuikuta hapa mjini mambo safi kumbe huko kijijini kwenye mashina na mizizi hakufai
Na ukifanikiwa kupata mwenza sahihi.. JICHUNGE NA NGONO zembe.. Ngono imeharibu mengi

Kingine ni mahusiano ya kifamilia, ndugu na ukoo.. Jihadhari mno na mafarakano.. Kuna majanga huanzia huko.. Upendo na kusamehe huokoa mengi, visasi na mifarakano huzalisha mengi
Kuna shida gan ukifanya ngono na mtu sahihi??
 
Hiki ndicho walichokuwa wanakifanya mababu zetu zamani.. Unaweza kukataliwa ndoa kwasababu ya background ya familia
Ashakum si matusi. Siku hizi vetting hufanywa kibinafsi zaidi na kwa ushabiki (mtu anayeoa/olewa)na hufanyika mtu akiwa amelamba kilaji maeneo ya bar/kilabuni au sehemu za starehe na kinachotazamwa ni Umbile/Muonekano wa nje e.g. "figure eight", Tako, Uwezo wa kifedha n.k. Tunakoelekea ni kubaya zaidi hadi Me anatamani Me. Aibu kubwa mno.
 
Mkuu,bado umeniweka katika mabano.

Naomba ufafanuzi wa kina tafadhali.
Kwa tafsiri nyepesi ni mambo ya nyota na afya ya kiroho.. Ukikutana na mtu wa hivyo na mkatengeneza familia automatically kama wewe ni dhaifu kiroho na una hayo majanga yeye ndio atakubeba
 
Unapopata mchumba usiharakie ndoa chukua muda wa kutosha kuichunguza familia yake mpaka huko kijijini.. Maana unaweza kuikuta hapa mjini mambo safi kumbe huko kijijini kwenye mashina na mizizi hakufai
Na ukifanikiwa kupata mwenza sahihi.. JICHUNGE NA NGONO zembe.. Ngono imeharibu mengi

Kingine ni mahusiano ya kifamilia, ndugu na ukoo.. Jihadhari mno na mafarakano.. Kuna majanga huanzia huko.. Upendo na kusamehe huokoa mengi, visasi na mifarakano huzalisha mengi
Leo unaongea kama mtumishi.

Ubarikiwe.
 
Kwa tafsiri nyepesi ni mambo ya nyota na afya ya kiroho.. Ukikutana na mtu wa hivyo na mkatengeneza familia automatically kama wewe ni dhaifu kiroho na una hayo majanga yeye ndio atakubeba
Asante Sana.

Hapa inabidi kutafakari Sana.
 
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk

Haya mapepo hutembea na vizazi mpaka cha tatu ama cha nne.. Unapoona kwenye familia yako kuna dalili za mojawapo kati ya hayo fanya hima lisisambae na kuathiri wengine.

Kuna ujumbe uliotoka Twitter unaoutaarifu uma kuhusu binti mmoja aliyefariki Morogoro na mwili wake uko mochwari. Hana ndugu ama kwa lugha nyingine ndugu zake hawajulikani ni akina nani.

Kilichonifanya niandike mada hii ni marehemu wakati wa ugonjwa wake akiwa kalazwa hospital kusema hana wazazi (haikufafanuliwa kama ni marehemu ama hajawahi kuwajua ama vinginevyo)

Cha kuumiza zaidi ni kwamba naye kafa kaacha watoto wadogo wawili.. Ni wazi hao watoto wana baba zao/yao lakini hawajulikani walipo. Inaumiza mno kwamba nao watakua katika mkondo wa mama yao.. Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!

Ni maisha ya namna gani yanawasubiri hawa malaika? Mama kabla ya kifo kasema hana wazazi japo kataja alikotokea! Vipi kuhusu ndugu? Vipi kuhusu baba wa watoto?

Itakuwa faraja kubwa kama nduguze watajitokeza na kumchukua marehemu wakamzike na kuwachukua watoto wakawalee. Upendo hawatapata kama wa mama lakini at least watajulikana asili yao ili nao wasijekuja kusema huko ukubwani kwamba hawana wazazi wala ndugu[emoji25]

Kuna familia zina laana ya asili

Painful and touching post
 
Back
Top Bottom