Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Ahsante mkuu.. bahati nzuri wewe umesoma yoga na meditation mkuu.
Tunaamini mtu yoyote anazaliwa akiwa na pure Consciousness,baada ya muda huanza kuwa contaminated na mambo ya kidunia.

Ndipo tunapo rudi kufanya Yoga,ili kurelease karmic energy zote ambazo mtu amekuwa contaminated nazo. Ambapo unarud tena upya ukiwa pure.
[emoji1545][emoji817] umeongea kiroho zaidi.. I wish haya masomo ya utambuzi wa kiroho yangekuwa yanafundishwa kwenye taasisi zetu za elimu
 
Broo Mshana,,naomba usitutishe walamba asali!!!
 
Kinachowaponza wengi ni tamaa na kupenda short cut.. Yaani mtu humfahamu vizuri tayari ushamparamia.. Iwe hiyo moja basi.. Unanogewa na kuendelea halafu taratibu kuna vitu unaanza kuviona ambavyo si vya kawaida sana lakini unapuuzia
Kuna ndoto unaoteshwa lakini unapuuzia
Marafiki wanakuonya lakini unadhani wanakuonea gere
Ndugu wanakuhadharisha lakini unawaona hawapendi maendeleo yako

Haya mambo huwa hayaji kwa bahati mbaya, huwa na background
Hapa nimekuelewa vizuri sana mzee. Asante kwa kutuelimisha maana elimu ni pana mno. Je wale wanaonunua wanawake wanaojiuza madhara yake yapoje ukilinganisha na hawa wanao amua kudumu kwa muda mrefu na aina hii ya watu?
 
[emoji3] trust me nimeacha ulozi na kumrudia Mungu mazima.. Si unajua kiza na nuru havikai pamoja? Niliamua kuchagua nuru na niko nuruni sasa[emoji173]
Ni kweli MshanaJr: uliwahi kuwa mganga/mtoa tiba za kiasili au ni kwa sababu tu ya kujua elimu ya mambo haya?
 
Hapo kwenye dilution sasa ndo unatoka njiani.

Ni hivi.

Kila mtoto anapoingia duniani, mtoto ambaye ni pure human hajachanganya uzao na mapepo, hatma ya maisha yake Huwa Inajulikana, NDOA pia Huwa Inajulikana. Tena NDOA yenyewe ni ya mke mmoja na mme mmoja.

Wapo watakaohoji iweje wanawake wawe wengi Duniani kuliko wanaume, kwamba hao waliozidi wataolewa na nani?

Jibu ni Rahisi. Uzao wa WANADAMU wasiochanganya uzao na mapepo ni Wachache kuliko uzao wa mapepo ktk mwili wa mwanadamu.

Na wanawake nusu mtu nusu Pepo ndo wengi kuliko wanaume nusu mtu nusu Pepo.

Waliookoka Wana solution ya kudumu.

Waliookoka tuna uwezo wa kujua nani Hasa ni ubavu wa mtu mume au mtu mke kupitia maombi.

Binti mmoja aliyeokoka alikuwa katika maombi, alimuuliza Mungu amuonyeshe Mume wake aliyeumbiwa Yuko wapi na alijibiwa.

Jibu lilikuja katika maono, aliambiwa mumuwe yupo Mkoa mwingine tena watakuja kukutanishwa baada ya miaka miwili ijayo.

Binti yule baada ya hapo hakujisumbua kutafuta au kusikia offer za wachumba wengine Hadi mumewe alipoletwa baada ya muda huo kufika na wakaoana sawa na Neno la BWANA.

Binti mwingine alichumbiwa na mchumba tajiri, bt alipoingia ktk maombi, Mungu alimwambia huyo Si ubavu wako, na Hana maisha marefu sababu atafariki baada ya miezi kadhaa sababu ndiyo hatma yake, so what if angekubali kuolewa, angekuwa mjane baada ya muda mfupi.

Ushauri.

Kama wewe ni Mwana wa Mungu,Usitende kuuliza Kwa mganga akusomee nyota,

Waislamu wanaAMINI katika Mungu lakini wanafail Kwa kuamini Waganga pia.

Mganga ni agent wa Ufalme wa chini, kama mtu ni uzao wa kipepo,ruksa kwenda Kwa mganga kuuliza mkewe kinyota kama wanaendana.

Bt kama ni uzao Kutoka juu, Mungu ana majibu yote.

Nawasihi Binti za Mungu, msikate tamaa mnapoona ubavu wenu hatokei Kwa wakati, yaezakuwa mumeo ameenda kuoa Pepo bila kujua, hivyo UKIOMBA Mungu, Mungu ataingilia kati na kuvunja NDOA ya kipepo Ili mtu sahihi arudi kufunga NDOA ilokusudiwa tangu Kuzaliwa.

Ameen
Nimejufunza kitu kikubwa hapaa.Asante sana
 
Hapa nimekuelewa vizuri sana mzee. Asante kwa kutuelimisha maana elimu ni pana mno. Je wale wanaonunua wanawake wanaojiuza madhara yake yapoje ukilinganisha na hawa wanao amua kudumu kwa muda mrefu na aina hii ya watu?

Lile nalo ni pepo baya sana hasa kama una familia
Imagine mwanamke unayemnunua ana joto na vinasaba vya wanaume wangapi aliolala nao? Kwahiyo unaingizwa kwenye mnyororo bila kujua
Mbaya zaidi sio wanaojiuza wote ni kwa ajili ya umasikini na kipato wengine ni ma agent wapo kuvuna manii kwa matumizi ya kishirikina

Kudumu na huyo mwenye hizo changamoto pia ni tatizo kwakuwa kuna mambo utafanya hayaendi na yakienda ni kwa msuli mkubwa sana

Unapata kipato kizuri lakini huna cha maana ulichonacho
Una kazi nzuri lakini hali yako na familia yako havilingani na hadhi ya kazi yako
Ni rahisi kutengeneza michongo ya pesa lakini pesa ukiitia tu mkononi kuna kitu cha dharura kinahitaji pesa kinatokea na kinakuhusu asilimia 100
Una pesa, una maisha mazuri lakini ndani ya familia kila siku ni changamoto haziishi nknk
 
Hiki ndicho walichokuwa wanakifanya mababu zetu zamani.. Unaweza kukataliwa ndoa kwasababu ya background ya familia
Hili lilikuwa jepesi kwakuwa sehemu kubwa ya jamii ilikuwa inakaa pamoja. Siku hizi miingiliano mingi, kumtrace mtu historia inakuwa ngumu. Tunaoana juu Kwa juu mno. Wazazi wakikataa, tunasema tunaingiliwa.

Hatari sana.
 
[emoji3]kidogo nilijaribu kufanya kwa vitendo.. Kidogo sana lakini
Hongera pia kwa kujifunza maisha, kila mtu anapitia mambo kadhaa katika maisha. Zote ni njia ila kujua njia sahihi ni neema tu na kila jambo linayo makusudi.
 
Umeiweka vizuri sana na umeongezea na mengine ya kujenga hasa hapo kwenye kuisikiliza sauti ya Mungu.. Na hili ni lazima litambulike kwamba sauti ya Mungu ni kati ya mhitaji na Mungu wake na si kupitia kwa madalali wa kiimani waitwao mitume na manabii

La pili ni hili ulilonipinga lakini kumbuka kuna hiki kitu kinaitwa kizalia (DNA) hiki ndio kiunganishi cha familia mpaka ukoo, ni mnyororo usiokatika mpaka upate kiunganishi na kutengeneza mwingine
Kuhusu DNA na mnyororo unaouongelea ni Kweli kabisa. Hiyo Iko kibinadamu.

Shetani alifanikiwa kuingiza DNA yake Kwa WANADAMU baada ya Hawa kula tunda alilokatazwa na ndo mlango shetani alitumia kutesa WANADAMU.

Wamwaminio Mungu hubadilishiwa DNA za Kuzaliwa.

Mtu anaweza Toka kwenye uzao ambao ni MASKINI Kwa kurithi, wauaji Kwa kurithi, au wenye magonjwa ya kurithi nk nk.

Bt aaminipo anabadilishiwa DNA, mababu na mizimu ikimtafuta ktk frequency zao wanamkosa.

Sisi Wana wa Mungu Kutoka juu, tukimpokea mtu aliyetoka kwenye vifungo vya kiukoo, Huwa tunamtenganisha na ukoo wake na tunamsajili ktk ukoo wa Wana wa Mungu.

Mtu mmoja alikuja kuomba msaada baada ya kustukia jambo Fulani baya lililokuwa linafuata familia Yao,

Walizaliwa watoto 6, Yeye alikuwa mtoto wa mwisho, waliandamwa na vifo vilivyofuatana ktk tarehe, na mwezi.

Ilikuwa Kila ilifika tarehe hiyo na Mwizi huo atafariki mmoja wa wanafamilia, aliuzika baba, mama, kaka zake wote, na alipobaki Yeye alistuka na akaja Kwa watumishi wa Mungu.

Alikatiwa connection hiyo, akabatizwa na kubadilishwa Jina. Ilipofika tarehe na mwezi husika hakufariki.



MANABII wa Kweli na UWONGO.

Mungu husema na Kila mtu, awe mwovu au mwema, tunatofaitiana tu jinsi ya kuelewa sauti hiyo sababu husema Kwa mafumbo ktk ndoto, maono au ktk Ulimwengu wa Roho.

Mtu anaweza kujisaidia Yeye mwenyewe bila kwenda Kwa manabii wa uongo kama tu atamkiri Yesu, ataacha dhambi na kuishi maisha ya usafi wa mwili na NAFSI.

Mungu hasemi na manabii pekee, anasema na watu wote, waislamu, wapagani nk nk Sema tu hawajui kusikia asemavyo.

Kama Kuna NABII wa Kweli, basi na Nabii wa UONGO yupo,

Kama Kuna mitume wa uongo, basi jua mitume wa Kweli wapo.

Hapa Tanzania Kwa mfano, Kuna madhabahu kubwa sana ya masonry inayowameza watumishi wa Mungu kuwatoa Kwa Mungu na kuwasajili huko.

Wanaanza vizuri, baada ya muda Fulani wanatekwa na kuingia huko.

Anayejiita Mzee wa.....na buldo... , Mwingiraaar,suguyuye,nk Walianza ktk Mungu bt nw ni manabii wa uongo.

Mwl Mwakasege,Mch Eliud misholi, Mch MBARIKIWA,Shehe Umar, Mchungaji Katunzi, Amiel Katekela ni baadhi ya Manabii wa KWELI wa Mungu.

So kama Bado ni mchanga kiimani Si vibaya kutafuta manabii wa Kweli wa Mungu ambao ni Wachache sana wenye kuihubiri Kweli ya Mungu.

Aamen
 
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk

Haya mapepo hutembea na vizazi mpaka cha tatu ama cha nne.. Unapoona kwenye familia yako kuna dalili za mojawapo kati ya hayo fanya hima lisisambae na kuathiri wengine.

Kuna ujumbe uliotoka Twitter unaoutaarifu uma kuhusu binti mmoja aliyefariki Morogoro na mwili wake uko mochwari. Hana ndugu ama kwa lugha nyingine ndugu zake hawajulikani ni akina nani.

Kilichonifanya niandike mada hii ni marehemu wakati wa ugonjwa wake akiwa kalazwa hospital kusema hana wazazi (haikufafanuliwa kama ni marehemu ama hajawahi kuwajua ama vinginevyo)

Cha kuumiza zaidi ni kwamba naye kafa kaacha watoto wadogo wawili.. Ni wazi hao watoto wana baba zao/yao lakini hawajulikani walipo. Inaumiza mno kwamba nao watakua katika mkondo wa mama yao.. Malezi na makuzi bila wazazi wote wawili. Mama akiwa marehemu lakini asiyejulikana! Inauma sana!

Ni maisha ya namna gani yanawasubiri hawa malaika? Mama kabla ya kifo kasema hana wazazi japo kataja alikotokea! Vipi kuhusu ndugu? Vipi kuhusu baba wa watoto?

Itakuwa faraja kubwa kama nduguze watajitokeza na kumchukua marehemu wakamzike na kuwachukua watoto wakawalee. Upendo hawatapata kama wa mama lakini at least watajulikana asili yao ili nao wasijekuja kusema huko ukubwani kwamba hawana wazazi wala ndugu[emoji25]


Kuna familia zina laana ya asili



Upungufu wa kinga za kiroho


Vyombo vya habari visaidie kutoa taarifa ndugu/watu wa karibu wapatikane
 
Kinachowaponza wengi ni tamaa na kupenda short cut.. Yaani mtu humfahamu vizuri tayari ushamparamia.. Iwe hiyo moja basi.. Unanogewa na kuendelea halafu taratibu kuna vitu unaanza kuviona ambavyo si vya kawaida sana lakini unapuuzia
Kuna ndoto unaoteshwa lakini unapuuzia
Marafiki wanakuonya lakini unadhani wanakuonea gere
Ndugu wanakuhadharisha lakini unawaona hawapendi maendeleo yako

Haya mambo huwa hayaji kwa bahati mbaya, huwa na background
Hii kitu unayoisema nimepata uzoefu nayo kwa sehemu. Miaka ya nyuma huko nilipata girlfriend mzuri, anaakili ya kimaisha na ya ziada. Ila hiyo ya ziada ni ya gizani. Pia nilikuja kugundua ni mtu mwenye muunganiko mkubwa sana na mapepo/majini. Sababu aliwahi kuniambia mwenyewe baadhi ya matukio ya ndoto na linalokuja kutukia physically. Tulikuwa tukivutana sana kama wote ni wanaume na Kuna wakati alikuwa na utisho. Alikuwa ni mwanamke anayetaka kuniinamisha kitu ambacho sijawahi kuota katika maisha ya mume na mke. Nikaachana naye maisha yakaendelea, lakini Kuna matukio kadhaa yalikuwa yakinitokea kwenye ndoto hata baada ya muda wa miaka zaidi ya mitano tuliyoachana! Tangu hapo naheshimu sana mambo ya uhusiano wa mwanamke na mwanaume na hata mwingiliano wa kawaida tu wa wanaume wenzangu kama marafiki. Bila shaka naeleweka vizuri na watu wenye upeo wa ziada.
 
Hii kitu unayoisema nimepata uzoefu nayo kwa sehemu. Miaka ya nyuma huko nilipata girlfriend mzuri, anaakili ya kimaisha na ya ziada. Ila hiyo ya ziada ni ya gizani. Pia nilikuja kugundua ni mtu mwenye muunganiko mkubwa sana na mapepo/majini. Sababu aliwahi kuniambia mwenyewe baadhi ya matukio ya ndoto na linalokuja kutukia physically. Tulikuwa tukivutana sana kama wote ni wanaume na Kuna wakati alikuwa na utisho. Alikuwa ni mwanamke anayetaka kuniinamisha kitu ambacho sijawahi kuota katika maisha ya mume na mke. Nikaachana naye maisha yakaendelea, lakini Kuna matukio kadhaa yalikuwa yakinitokea kwenye ndoto hata baada ya muda wa miaka zaidi ya mitano tuliyoachana! Tangu hapo naheshimu sana mambo ya uhusiano wa mwanamke na mwanaume na hata mwingiliano wa kawaida tu wa wanaume wenzangu kama marafiki. Bila shaka naeleweka vizuri na watu wenye upeo wa ziada.
Ndiyomaana huwa namwomba sana Mungu kuniepusha na majanga ya kuendekeza vimada kila kona ya nchi maana mengine ndiyo hayo mapepo yenyewe
 
Back
Top Bottom