Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Ipo hapa mtaani mzee ana watoto tisa, wakike ni saba wa kiume wawili. Wadada wote wamezalishwa tena sio mtoto m'moja wamezidiana idadi ila kila m'moja ana watoto zaidi ya wawili. Wamerudishwa nyumbani wote na watoto. Mzigo anabeba bibi yao.
Wanapaswa kumlilia Mungu aisee
 
Kuna familia acha tu na tatizo linakuwa kwa wakubwa kina mjomba na au babu hawawakusanyi ndugu na kukaa kila mara kufanya vikao vya ndugu na kutambulishana,kuna ndugu hawajaliani kabisa na hawana muda unakuta kila familia wamejitenga
 
"... Kama wewe ni Mwana wa Mungu,Usitende kuuliza Kwa mganga akusomee nyota,"

ANAYEULIZA KWA MGANGA BADO HAJAWA MWANA WA MUNGU!
 
"... Kama wewe ni Mwana wa Mungu,Usitende kuuliza Kwa mganga akusomee nyota,"

ANAYEULIZA KWA MGANGA BADO HAJAWA MWANA WA MUNGU!
Ndio Wana wa Mungu hawaendi kupata hatma ya maisha Yao Kwa Waganga ambao ni agent wa kuzimu.

Ni sawa na mtoto wa Kondoo apotee njia akakuta Simba ananyonyesha wanae, na Kondoo akajumuika na Wana wa Simba kunyonya Kwa mama Simba.


Hairuhusiwi, ni hatari.
 
Pepo la Umaskini
Pepo la mikosi
Pepo la kukosa ndoa
Pepo la kuzalia nyumbani
Pepo la ugumba
Pepo migogoro na mafarakano
Pepo la wizi, utapeli na udanganyifu
Pepo la madeni na mikopo isiyolipika nknk


Hivyo vitu hapo juu karibu vyote vinaanza katika ngazi za familia,koo,taifa na bara. Mimi nimejaribu kufikiri kama ifuatavyo hasa ngazi ya bara moja na bara lingine:

a) Umasikini:
Afrika inaongoza kwa umasikini mkubwa.

b)Migogoro na mifarakano: Afrika inaongoza.

c)Mikopo na madeni: Afrika inaongoza.

d)Wizi,utapeli,udanganyifu (ufisadi): Afrika tumo

e)Mikosi mbalimbali :Afrika tumo

Swali :Tumelaaniwa??????

Jibu: Hapana
, ila tumeacha kufikiri kwa kutumia fikra tunduizi na tunatumia fikra mfu. Kwa kifupi tunatumia majibu rahisi kwenye maswali magumu.

Mfano mzuri ni hapo juu, ukitumia fikra tunduizi kujibu maswali ya hapo juu utagundua kuwa yote ambayo umeyataja yana sababu na chanzo chake na vilevile yana majibu na suluhisho yake.

Bara la ulaya baada ya kupitia katika zama za giza hatimaye walipata mwamko(Renaissance) kwani waliamua kuacha watu wa dini, waganga na washirikina wawaamulie na kuwatatulia matatizo yao.

Badala yake waliamua kutafuta kiini cha tatizo husika na majibu yake kwa kina kupitia fikra tunduizi. Mara baada ya huu mwamko, kilichotokea ni historia mpaka leo!!!!!!!!!!!!

Renaissance | Definition, Meaning, History, Artists, Art, & ...​


Encyclopedia Britannica
https://www.britannica.com › ... › Philosophical Issues



28 Mar 2023 — Renaissance, (French: “Rebirth”) period in European civilization immediately following the Middle Ages and conventionally held to have been ...

Nb 1: Tuache kujibu majibu rahisi kwenye maswali magumu:

Mfano 1: Kwanini wewe ni masikini????


Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya umasikini kwenye ukoo wenu.

Mfano 2: Kwa nini wewe hujaolewa???

Jibu : Umelaaniwa. Kuna laana ya ndoa kwenye ukoo wenu au familia yenu.

Nb 2: Kila tatizo lina chanzo chake na suluhisho lake.

Nb 3: Kufikiri kwa kutumia fikra tunduizi ni njia sahihi ya kukabiliana na matatizo mbalimbali.

Nb 4: Kazi kuu ya kichwa ni kufikri licha ya kuwa na kazi nyingine ya kubebea masikio!!!!!!!!!!

Ni mtazamo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 
Ukitoka au Kuzaliwa ktk familia ambayo tangu Babu wa mababu Hadi wazazi na kaka na dada zako kiukoo hayupo aliyevuka darasa la nne, utaipata vp hiyo unayoita Elimu?
Unakubaliana na mimi au unakataa? Elimu ndio mwisho hicho kinachoitwa pepo, hata hao unawaona kwa Mwamposa wa pepo tokaa,pepo tokaaa, ni elimu tu ndio shida yao hakuna cha pepo wala nini.
 
Safi sana mkuu
 
Unaelezea nin shuhuda za uongo hapa unafikria nan anakuelewa na hizo porojo za kutunga😂😂😂.

unaelezea vip uislamu wakati hujui kitu?
Usiingie udini hapa, HOJA ni ingine kabisa.

It's all about faith in God, na jinsi Gani mtu anaweza kujikuta ktk mkwamo Fulani maishani chanzo kikiwa ni kurithi.
 
Pepo la vifo mfululizo!
Hili acha kabisaaa
 
Usiingie udini hapa, HOJA ni ingine kabisa.

It's all about faith in God, na jinsi Gani mtu anaweza kujikuta ktk mkwamo Fulani maishani chanzo kikiwa ni kurithi.
Kwa nn utaje waislamu eti wanaamini waganga ..Tena usirudie tena .!


Sitaki kubishana .
 
Unakubaliana na mimi au unakataa? Elimu ndio mwisho hicho kinachoitwa pepo, hata hao unawaona kwa Mwamposa wa pepo tokaa,pepo tokaaa, ni elimu tu ndio shida yao hakuna cha pepo wala nini.
Kama unapinga hakuna shetani,mapepo,majini basi wewe ni mchawi.

Unawadanganya watu humu wapuuze Imani katika Mungu Ili uwamalizie.
 
Kwa nn utaje waislamu eti wanaamini waganga ..Tena usirudie tena .!


Sitaki kubishana .
Jikite kwenye HOJA.

UKWELI uko pale pale wapo wengi wanaoingia miskitini, makanisani, na wengine hawaendi Kanisani Wala msikitini wanaoenda Kwa Waganga na wengine kufuga majini.

Wote hao ni kundi moja, wanatakiwa wamtegemee Mungu mmoja na wa pekee.

Mungu yule aliyekuwa akiwatembelea Adam na Hawa Bustani ya edeni na kuongea nao na kutatua changamoto zao zote.

Na Mungu huyo Hadi Leo Bado huongea na Wana wake, na kutatua changamoto zote.

Amen
 
sema hivyo usiseme waislamu wanaamini waganga karekebishe na siku nyingine usirudie.!
 
sema hivyo usiseme waislamu wanaamini waganga karekebishe na siku nyingine usirudie.!
Acha ibaki hivyo hivyo maana waislamu ni Wakristo na Wakristo ni waislamu sababu Aliyewaumba na kuwapa PUMZI wote ni Mungu mmoja.

Dini ya Kweli ni kuwajali maskini na wajane, kuwapenda WANADAMU wote bila ubaguzi sababu Edeni hapakuwa na Uislamu au Hindu au HEKALU,

Edeni palikuwa na WANADAMU na IMANI juu ya Mungu mmoja wa pekee.

Amen
 
Acha ibaki hivyo hivyo maana waislamu ni Wakristo na Wakristo ni waislamu sababu Aliyewaumba na kuwapa PUMZI wote ni Mungu mmoja.

Amen
Mimi na wewe na wengine sote sio wakamalifu hakuna wakumshutymu mwenzio wala kusema hutu yupo hivi .!

Narudia dini zote zimeoinga ushirikina ila ni watu wa pande zote wanafanya mambo ya ushirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…