Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kinachowaponza wengi ni tamaa na kupenda short cut.. Yaani mtu humfahamu vizuri tayari ushamparamia.. Iwe hiyo moja basi.. Unanogewa na kuendelea halafu taratibu kuna vitu unaanza kuviona ambavyo si vya kawaida sana lakini unapuuzia
Kuna ndoto unaoteshwa lakini unapuuzia
Marafiki wanakuonya lakini unadhani wanakuonea gere
Ndugu wanakuhadharisha lakini unawaona hawapendi maendeleo yako

Haya mambo huwa hayaji kwa bahati mbaya, huwa na background
Nilikuwa na manzi mmoja mkoa x huyu manzi nilimuelewa kweli na yeye pia alinielewa (tulipendana) , na background yake yeye ni mtoto wa pasta , shida zikaanza sasa, niliota zaidi ya 5 times kuonywa vikali kuachana na huyu manzi , kwa kuoneshwa live matendo yake machafu nyuma ya pazia ( Nilikuwa vizuri kiroho )

So , kwa kumalizia ni kwamba unaweza kufanya uchunguzi na ukaona pale ni sahihi , ila ukajuta vilivyo na pia kuna sehemu nyengine unaweza kuona sio sahihi kwa macho ila hapo ndio penyewe , tunakosea kwa sababu tupo mbani na yule ayajuaye ya sirini MUNGU aliye hai.
 
Nilikuwa na manzi mmoja mkoa x huyu manzi nilimuelewa kweli na yeye pia alinielewa (tulipendana) , na background yake yeye ni mtoto wa pasta , shida zikaanza sasa, niliota zaidi ya 5 times kuonywa vikali kuachana na huyu manzi , kwa kuoneshwa live matendo yake machafu nyuma ya pazia ( Nilikuwa vizuri kiroho )

So , kwa kumalizia ni kwamba unaweza kufanya uchunguzi na ukaona pale ni sahihi , ila ukajuta vilivyo na pia kuna sehemu nyengine unaweza kuona sio sahihi kwa macho ila hapo ndio penyewe , tunakosea kwa sababu tupo mbani na yule ayajuaye ya sirini MUNGU aliye hai.
Ungesema ung'ang'anie ungeisoma number vibaya mno
 
Ulimwengu wa Roho/Spiritual realm ndio chanzo au asili ya mabo yote tunayoona yakidhihirika mwilini.Iwe ni mazuri(baraka) au mabaya(laana) kwenye maisha ya mtu au watu chanzo chake ni rohoni.
Kwa nini ninasema hayo? Lazima mtu ujiulize chanzo cha haya yanayonitokea ni nini?na lini nitapata ukombozi kamilifu toka kwenye tatizo au matatizo yanayonikumba?
-Kuelewa chanzo na uhalisi wa kitu kinakupa urahisi wa kulitatua tatizo kwa ukamilifu na kwa uhalali ili kumaliza madhara yaliyojitokeza na kuzuia mengine ambayo yangetokea kutokana na roho au tabia fulani.Lakini pia hukupa uhalali wa kutafuta,kupata na kudai baraka zako au za uzao wako unazopaswa kuzipata katika maisha yenu.
Asili ya ulimwengu wa Roho;
-Uhalali/legitimacy.
Mambo yote yanayotokea kwenye maisha ya mtu au watu yana uhalali kwa aliyekusudiwa.Angalia familia,ukoo au boma lenu linaandamwa na nini?Panakuwa na mtiririko rasmi wa mambo mazuri au mabaya yanayowatokea watu jamii moja.Kuna nini kinakupa uhalali wa kupata hayo mema(utajiri,afya njema,elimu bora,familia bora yenye ustawi na maelewano na maisha marefu)au mabaya(magonjwa,faraka na ibu za ndoa,magomvi,umasikini ulitopea na kushindwa kielimu).Uhalali wa mambo mazuri unatokana na kutenda mazuri kwa Mungu au kuwa mwaminifu kwa shetani pia.Vile vile uhalali wa mambo mabaya hutokana na kukiuka miiko na mapatano ya maagano yaliyowekwa awali,kurithi jina,laana za familia,kukataliwa au kujikataa mwenyewe na kuabudu ushirikina.
 
-Siri/secret operating
Ulimwengu wa roho unaendesha mambo yake kwa SIRI NA MAFUMBO sana.Mwenye uwezo wa kutambua hayo ndiye anayeshinda kabisa kwenye ulimwengu wa damu na nyama.Ni muhimu kujua siri ya baraka zako au matatizo unayokumbana nayo.Wakati mwingine unaweza kujiona upo sahihi ukichunguza mwenendo wako;la hasha kumbe matatizo au tatizo lako limeletwa na mtu au watu waliopita katika maisha yako.Kuwa makini sana na mwenza(mume au mke),marafiki,majirani na ndugu.Wanaweza kuwa anguko au inuko lako kutokana na roho walizobeba.CHUMA HUNOA CHUMA.
Mfano Soma 2Samweli 21:1-9 n Yoshua 9 yote kuna funzo utalipata.

Madhara yanaweza kukupata hata kama wewe hukutenda mabaya kama wazazi wako walikuwa kama Sauli.Kuna nguvu katika maagano.Maagano yana viapo,matamko na madhara yanayoendana na kukiuka maagan😵le wako unayechukulia poa maagano unayofanya na wengine hakika utalipa kwa njia moja ama nyingine.Iwe katika ndoa au kazini tunza kiapo chako.Ukikiuka tu kuna madhara utayapata mwenyewe au uzao wako.
Jitahidi kujua siri ya tatizo lako na si kukimbilia kwa wasaidizi wa kiroho wa uongo watakuokuengezea mzigo wa matatizo.Mwombe Mungu wa kweli akujulishe siri ya matatizo yako.Lakini kwa wale wenye kumbukumbu za kifamilia fatilia ujue umepataje hayo mema isije kuwa umeyapata kwa kuwatenda wengine mabaya ikawa chanzo cha shida kwa uzao wako baadaye
 
-Ni ulimwengu wa mbadilishano/Trade oeiented.
Maisha ya mwanadamu katika kila kitu kina mbadilishano.Naamanisha utatenda hili upate lile.Hakuna kinachokuja bure.Na kila upande mwema au mbaya huvutia kwake kwa sera nzuri lakini zenye masharti ya mficho ndani yake.Tumeumbiwa free will katika kufanya maamuzi,amua leo unataka mema au mabaya?Amua nani unayetaka kumtumikia?Mungu ama shetani maana wote ni roho.

Maamuzi yako ndiyo yatakayoainisha ni nini kikupate baadaye.Na usije ukajidanganya huko utakapochagua kuenenda ndipo utapata malipo yake.Umeamua kupata vitu kwa uhalali pasipo dhuluma wala manung'uniko hakika utapata mema yadumuyo.Lakini unatafuta kwa dhuluma,ushirikina,kutumia mwili wako isivyo halali au kwa ushawishi wa pesa ama zawadi ndiyo yapo mafanikio ya muda mfupi yenye kilio kwako au kwa wengine.Unatoa nini upate nini?Kama ulivyosema kaka unaburudisha mwili leo lkn unazoa roho au mapepo yanaweza kukudhuru mwenyewe afya ya mwili na akili pia na uchumi.

Je unatumia nyezo gani katika mbadilishano?
(Moyo wako,pesa,kuiba nyota za watu,uchawi,kumwaga dammu za watu nk).
Jiulize mwisho wa hayo yote unayoyafanya yanakupa amani ya moyo na ungependa utendewe hivyo kupata mafanikio au kutatua shida zako?
Ninachoamini dhambi husameheka lakini madhara yake je?Vipi kwa wengine wasiojua baba au mama alitoa nini apate nini?
 
La msingi ni kusimama katika haki na kujichunguza mara kwa mara kwa mara tunavyoenenda ili tusiache vilio kwa vizazi vyetu.UTAVUNA ULICHOPANDA HAKIKA.Kama sio wmewe basi uzao wako.Lakini MAVUNO mabaya ya wazazi wetu yasizuie kuotesha fikira,mawazo na mitazamo mipya kama mbegu bora zinayoweza kuzaa matunda mema katika jamii zetu.
 
Post no 286 - 289 credit kwako: Chimodoi Asante kwa michango iliyoshiba maarifa[emoji1545]...Nimekuwa kama kijumbe tu[emoji1545][emoji818]
 
Kuna familia zina pepo la elimu kikomo ni la saba ama form 4
Kwa nini uone form 4 au la saba ni laana ,na usiseme kuna family wana mapepo ya kusoma hadi wanakufa maskini , boss wangu mimi kaishia darasa la sita,ila ana mawe balaa,dreva wake ni mtu mwenye degree,ana wafanyakazi 18 wasomi
 
Kwa nini uone form 4 au la saba ni laana ,na usiseme kuna family wana mapepo ya kusoma hadi wanakufa maskini , boss wangu mimi kaishia darasa la sita,ila ana mawe balaa,dreva wake ni mtu mwenye degree,ana wafanyakazi 18 wasomi
Kuna familia zina pepo la elimu kikomo ni la saba ama form 4!
Nimezungumzia pepo sijazungumzia laana! Je unaweza kuyatofautisha hayo mawili?
 
Kumradhi mkuu unaweza kuelezea angalau kwa muhtasari unaposema ‘pepo’ unamaanisha nini hasa?
 
Kuna familia zina pepo la elimu kikomo ni la saba ama form 4!
Nimezungumzia pepo sijazungumzia laana! Je unaweza kuyatofautisha hayo mawili?
Tusaidie tofaut kat ya pepo vs laana?
Kwa akili yangu ii ndogo pepo ni kiumbe cha shetani na laana ni matamko mabaya kwa mtu/koo..
 
Tusaidie tofaut kat ya pepo vs laana?
Kwa akili yangu ii ndogo pepo ni kiumbe cha shetani na laana ni matamko mabaya kwa mtu/koo..
Laana ni roho hasi inayotokana na maagano ama kunenewa vibaya ama malipizi kutokana na matendo mabaya ya mtu
Pepo ni roho ya mambo ambayo yanamhusu hata mwenye nafanikio mfano
Pepo la ngono, mchukulie mfalme Suleiman aliyebarikiwa utajiri na hekima lakini akapewa bakshish ya pepo la ngono
Kuna familia zimefanikiwa kwenye mambo ya biashara lakini kwenye elimu ni zero na kuna familia zimefanikiwa sana kwenye elimu lakini kwenye maisha ni sifuri
 
Haya ndio mambo na izo ndio njia ambazo tulipaswa kuyatufutia ufumbuzi kwenye ngazi za familia zetu, koo zetu na taifa ili kutibu na kufuta msululu wa matatizo yanayotuandama.

Sasa unakuta matendo ya kifisadi, rushwa, ubinafsi uliokithiri, chuki, visasi, malezi ya ovyo, mmonyoko mkubwa wa maadili kuanzia ngazi ya familia, tawala mbovu kwenye serikali zetu, mwisho wa siku matokeo yake ni ukosefu wa ajira kwa wengi, umaskini wa kutisha, mimba zisizotarajiwa, watoto wasio eleweka sababu ya ukosefu wa malezi nk. Sasa badala ya kutafuta mizizi na kutibu vyanzo vya matatizo hayo kuanzia ngazi ya familia zetu tunabakia tunafundishana kuwa eti ni mapepo na laana.

Na wahanga wakubwa wa haya mambo ni mabinti na wanawake ambao wamegeuka wateja wakubwa wa manabii mitume na waganga wa kienyeji waliomua kutumia ujinga wetu kuwa fursa kwako. INASIKITISHA SANA maana kwa hali hii mpaka Yesu anarudi ni kamwe hatuwezi kupata suluhu ya matatizo yanayoziandama familia zetu sababu tutabakia kupambana na mapepo na laana huku tukiacha "cause" ya matatizo yetu ikiendelea kuigwa na kurithiwa kizazi mpaka kizazi.
Aisee umesema vizuri sana.
 
Kwenye ukoo wangu tunasumbuliwa na umasikini mkubwa, tunajitahidi kupambana lakini hatuna mafanikio. Mkuu Mshana Jr hebu tusaidie juu ya hili.
Umasikini ni kama vazi chafu, ukiendelea kulivaa kwa kisingizio kuwa ni vazi lako umelizoea utaendelea kunuka na kuwa mchafu hadi siku utakapoamua kulivua na kuvaa vazi jipya.

Kimsingi umasikini huwa unakaa katika tabia na matendo yetu ya kila siku ambayo yapo kinyume na mifumo ya utafutaji na utunzaji wa mali.

Ukosefu wa maarifa ya matumizi sahihi ya muda, rasilimali watu ngazi ya familia na utengenezaji wa ramani ya muendelezo wa usimamizi wa kilichotafutwa inapelekea kuzaa umasikini ambao kila ambaye ataukubali basi utamvaa kama waliotangulia.

Ukiona familia yako wameukumbatia umasikini na wapo nao comfortable usione tatizo kujitenga nao na kupata sehemu ya tofauti ya kuanzisha Maisha nje yao.
 
Kumradhi mkuu unaweza kuelezea angalau kwa muhtasari unaposema ‘pepo’ unamaanisha nini hasa?
Pepo ni neno linalotokana na Kiyunani daimon, ambayo inamaanisha 'fikra' au 'roho' isiyojumlishwa. Fikra au roho hii pia inaweza kueleweka kama nguvu, lakini sio kama mtu aliye na mapenzi au mhusika.

Kwa sababu ya ukweli kwamba Injili zinasimulia hadithi tofauti juu ya kutoa pepo kutendwa na Yesu, imani imeenea kuwa pepo siku zote ni nguvu hasi au za kishetani, au ni shetani mwenyewe. Walakini, haya hayapaswi kuchanganywa na mfano wa shetani.

Mapepo, Ujuzi, au Roho zinaweza kuwa nzuri au mbaya. Katika eneo la imani za kiroho, inaaminika kwamba pepo, kama nguvu isiyo ya kibinafsi, hufanya kupitia watu katika mfumo wa milki, na kwa hivyo, inaweza kukuchochea wewe na uumbaji na uharibifu, mzuri na mbaya. Sasa, katika visa vyote viwili, "pepo" lazima aachiliwe ili mtu aliye na uwezo tena atumie mapenzi na uhuru wake.
 
Back
Top Bottom