Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Hawa wapo wengi na ni matokeo ya malezi mabovu tu. Mara nyingi watoto wanaolelewa na wazazi wa upande m'moja especially kuelelewa na mama tu au kulelewa na baba ambaye anamuachia bibi upande wa baba aleee mtoto anadekezwa anaharibika.
 
Kwahiyo according to u the strongest soul ni za wale waliookoka ...... African stil you night
 
Kwahiyo according to u the strongest soul ni za wale waliookoka ...... African stil you night
If you are not born again,

Lazima una LAANA za kurithi kutokana na dhambi za watangulizi, pia jua lazima una demons.

Ukiona uko salama, jua unasaidiwa na waombao katika Kweli ya Mungu.

Bt jua ulinzi wako ni hafifu, ukishambuliwa yatakupata.

Ukiishi Duniani jua Kuna Mungu au Shetani. Kama haamini any of the two, basi wewe ni WA Shetani Kwa dhambi ya Adam na Hawa ulorithi.
 
Ila Mshana Jr mimi niseme jambo moja tu kuwa hayo ni matokeo ya kirithi tabia. Unajua tabia zinaambukiza kama magonjwa mengine.

Watoto huwa wanatazama waliowakuta Duniani wanaishi kwa mfumo gani kisha nao wanaukopi na kuishi vile vile. A
Haya ndio mambo na izo ndio njia ambazo tulipaswa kuyatufutia ufumbuzi kwenye ngazi za familia zetu, koo zetu na taifa ili kutibu na kufuta msululu wa matatizo yanayotuandama.

Sasa unakuta matendo ya kifisadi, rushwa, ubinafsi uliokithiri, chuki, visasi, malezi ya ovyo, mmonyoko mkubwa wa maadili kuanzia ngazi ya familia, tawala mbovu kwenye serikali zetu, mwisho wa siku matokeo yake ni ukosefu wa ajira kwa wengi, umaskini wa kutisha, mimba zisizotarajiwa, watoto wasio eleweka sababu ya ukosefu wa malezi nk. Sasa badala ya kutafuta mizizi na kutibu vyanzo vya matatizo hayo kuanzia ngazi ya familia zetu tunabakia tunafundishana kuwa eti ni mapepo na laana.

Na wahanga wakubwa wa haya mambo ni mabinti na wanawake ambao wamegeuka wateja wakubwa wa manabii mitume na waganga wa kienyeji waliomua kutumia ujinga wetu kuwa fursa kwako. INASIKITISHA SANA maana kwa hali hii mpaka Yesu anarudi ni kamwe hatuwezi kupata suluhu ya matatizo yanayoziandama familia zetu sababu tutabakia kupambana na mapepo na laana huku tukiacha "cause" ya matatizo yetu ikiendelea kuigwa na kurithiwa kizazi mpaka kizazi.
 
Umeongea sana ila vingi ni vya kiimani ambapo kwa upande mwingine ni poroja ..

kwanza waislamu hawaamini waganga kumbuka dhambi ambao haisameheki kutokana na uislamu ni shirk ambao miongoni ni waganga ,kuabudu miungu mingi yaani shirk ni pana na mengi yapo nikupa kwa kifupi.


kingine baadhi ya mifano sijui mtu kujulishwa kwamba mume sijui lini atakuja ni uongo na ni nguvu za giza za kwenu moja kwa moja ni shirki...

kwenda kumkana dhambi mbele ya binadamu mwenzio ni shirk mweny kuombwa msamaha ni Mungu pekee so hapo sawa umeenda kwa mganga aliyevaa suti.


Kingine hata watu waaliokoka kibao wapo wanaenda kwa waganga na wala usibishe sina hakika kama ukristo unakubali ushirika ila hata uislamu haukubali kwa kuonyesha hatari yake ni kwamba dhamba ambayo haisameheki ni shirki.

Pia tambua baadhi ya mambo huwezi kujua eti mtu fulani atakufa siku fulani hapa labda ramli ambayo ni shirki ..

Kingine sisi waislamu tunaamini katika mambo sio kama useme mpaka upewe ufunuo hiyo kitu hakuna na hakipo ni nguvu za giza na ushuhuda wa uongo ..Ndo maana watu wanaomba kupata mke mwema hata kuwa na mwisho mwema hapa duniani ..


Mengine yapo sawa nimekuelewesha tu hamna ubishani.!!
 
Zemanda kuna vitu vikubwa sana umeandika hapa na vingine vinaumiza sana! Wanasema maji hufuata mkondo .. Kuna jamaa yangu ni school mate kwasasa nimeshajitenga naye kabisa.. Kwenye familia yao wana hizi tabia za kitapeli tapeli japo si kivile sana.. Sasa huyu jamaa yangu akenda kuoa familia ambayo karibia mabinti wote waliolewa na matapeli wa mjini.. Mmojawapo ni tapeli tajiri mpaka sasa lakini anaishi kama ndezi
 
Mimi magonjwa kama kisukari ,hiv,ulevi umalaya,pressure cancer,hayo trendi yake ni kubwa mno,kama ndugu yako mmja kapata jiandae
 
Kufanya ngono hovyo hovyo wengi wanadhani hatari ni kwenye ukimwi tu. Kuna magonjwa zaidi ya ukimwi na pia mikosi kama ulivyosema. BTW pepo la ngono kama alilonalo mzabzab halimo kwenye list.
BTW pepo la ngono kama alilonalo mzabzab halimo kwenye list.[emoji23] likoje hilo
 
Huwezi kunielewesha bila kujua au kuthibitisha UKWELI au uongo ktk nilichoandika.

Mfano, footballer anawezaje kumuelewesha fundi ujenzi jinsi ya kujenga magorofa?
 
Kwenye ukoo wangu tunasumbuliwa na umasikini mkubwa, tunajitahidi kupambana lakini hatuna mafanikio. Mkuu Mshana Jr hebu tusaidie juu ya hili.
EMMYGUY ndugu yangu hayo mambo ni very complicated na yana mizizi mirefu sana.. Ninachoweza kukwambia ni kutumia tu ile tiba yetu ya munyu ili walau kupata ulinzi na kuzuia mambo kuharibika zaidi huku ukipambana kupata suluhu ya kudumu
 
Hapo hakuna cha nini wala nini ni elimu tu ndio hakuna, kama kuna elimu ya kutosha hayo yotee aliyosema jamaa hayawezi kupata nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…