Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Nimekuelewa mkuu.

Nilichotaka kusema ni hizo nguvu hasi, sio kwamba zipo kwenye makundi mfano kundi la ngono, kundi la ulevi, kundi la uvivu, kundi la umasikini nk. Ila ni kundi moja tu la malaika waasi basi na ambao walishavunjwa vujwa na kumalizwa nguvu na Yesu mwenyewe, hivyo hawana tena ubavu wala nguvu zozote juu ya binadamu kama kabla ya Yesu kuwashinda. Hivyo tukiendelea kuwatupia lawama hawa malaika waasi kwamba ndio wanaoendesha hizo nguvu hasi kwa kuwaona kama wao ndio chanzo cha kila dhambi na matatizo yote yanayomkabili binadamu ma familia zetu basi Yesu hakuna alichokifanya na ni kama hakuwahi kuja kabisa duniani maana shetani na malaika zake bado wanatamba.
Asante kwa ufafanuzi mzuri[emoji1752][emoji1545]
 
Je wewe ndo unayeweka masharti ya second chance au ni aliyetuumba ndo huweka masharti?

Usiwe na inda wala ila ndani ya moyo unapokuwa unaangalia haya mambo. Usiwalaumu wahanga bali muombe Mungu yasikukute
Mkuu sio second chance tuu.
Chances zipo tena na tena na lazima zitaendelea kuwepo mpaka pumzi yetu ya mwisho, cha msingi ni hakuna kukata tamaa.

Mkuu usiseme hayajanokuta maana hatufahamiani, inawezekana yamenikuta mengi na magumu sana kuliko yako. Mkuu Jaribu kumuelewa Mungu na dini vinataka nini,
 
Pepo la pesa au cheo ni baya sana katika jamii, anaejua huo mchezo atawamaliza wote huku akijifurahisha kwenye viti virefu baa. Ila mwisho nae ataondoka.
 
Hiki ndicho walichokuwa wanakifanya mababu zetu zamani.. Unaweza kukataliwa ndoa kwasababu ya background ya familia
Pamoja na hiyo hao mababu zetu walizaa vilema, albino, wakawa maskini, wakawa wajinga mpaka wakauza nchi kwa wakoloni kwa vipande vya nguo.

Maisha yapo katika nyanja zote. Hakuna maisha plain yasiyo na mitikisiko. Huwezi kimbia changamoto za mseto wa maisha ya dunia.

Faida na Hasara maishani ziko upande mmoja na vyote huja pamoja sema kinachozidi kingine nguvu kwa wakati huo ndicho kinachoonekana na kuhesabiwa kuwa kipo.(kila penye faida pana hasara na penye hasra pana faida)

Maisha hayana kanuni ya pamoja ili wote tufanikiwe kwa kanuni moja na wakati mmoja.
Pamoja na mapambano ya juhudi,
1.Wengine unatakiwa uibe,unyanganye,uuwe ili ufanikiwe

2. Wengine utapeli na kudhulumu
4. Wengine ufanye ibada sana nuumba za ibada

Na kila kitu huja kwa majira na nyakati zake( huzuni/furaha, hasara/faida, kufanikiwa/kushndwa, utajiri/umaskin.)
 
Chumvi inahusiana nini na mfumo wa maisha?! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
1. Katika hali ya kawaida binadamu na wanyama wengine wanahitaji chumvi kama chakula. Kumbuka chakula ni Uhai.
2. Kiroho chumvi inatakasa na inaondosha au kupingana na nguvu hasi/ovu.(wengine huita nguvu za giza).
3. Katika mfumo wa maisha kuna mambo au mapito mengi. Katika mapito hayo, yapo mambo mazuri, mepesi, magumu au wakati mwingine changamoto zisizoeleweka chanzo chake ni nini e.g. nuksi, mabalaa, mikosi n.k.. Ili kukabiliana na mambo hayo chumvi hutumika kama mojawapo ya kupata suluhisho. Hapo imani yako ni muhimu. i.e. kama huamini kwamba kwa kutumia chumvi unaweza kupata suluhisho, basi we achana nayo komaa tu na hali yako.
4. Zingatia kwamba Mungu hakuiumba chumvi kwa bahati mbaya. Kama wewe ni Mkristo soma habari za nabii Elisha na jinsi Mungu alivyomwonesha atumie chumvi katika maji kama suluhisho la changamoto lililokuwepo katika mji wa Yeriko la watu kuzaa watoto mfu, vilema, mimba kuharibika n.k. kutokana na matumizi ya maji kutoka katika chemchemu iliyokuwa katika eneo lao. ( 2 Wafalme 2:19 -21).
Mwisho: Kwa wewe kutokuona au kukubali au kuamini kwamba kuna uhusiano wa chumvi na mfumo wa maisha, hakutaiondolea chumvi kuwa ni yenye kuvuta heri katika mustakabali wa mfumo wa maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Asante.
 
Ndio uko sahihi kabisa, sasa inategemea ni pepo la aina gani
Kwa Wakristo ni Malaika mlinzi. Huyo ni malaika anayekulinda katika hatari zote za Roho na za mwili siku zote. Ipo sala kwa RC inayosaliwa hv: "Sala kwa malaika mlinzi ... Malaika mlinzi wangu unilinde katika hatari zote....."
 
Hilo sio pepo ni upumbavu wa serikali ya kijani na raia wasiokuwa na maamuzi na serikali yao. Wewe unaona ni mapepo sababu unatazama hili tatizo la kukosa ajira kwenye individual level.

Ungelitazama katika level ya taifa ungeelewa kuwa haimake sense idadi ya wahitimu wasomi kuongezeka kila mwaka huku nafasi za kazi na taasisi zikiwa zile zile na watu hawastaafu wanang'ang'ania kubakia serikalini.

This means kuna mfumo ambao unakinzana na mahitaji ya uhalisia. Sasa hapo mapepo yanafanyaje huo upepo wao.
Nanukuu" Ungelitazama katika level ya taifa ungeelewa kuwa haimake sense idadi ya wahitimu wasomi kuongezeka kila mwaka huku nafasi za kazi na taasisi zikiwa zile zile na watu hawastaafu wanang'ang'ania kubakia serikalini.
Mkuu, hebu jaribu kupata mizania linganifu kwamba wahitimu Wasomi ni wengi na wanaongezeka kila mwaka (increasing at an increased rate) na nafasi za kazi ni zile zile(Constant). Hapo utaona ni lazima kuwepo na watakaokosa nafasi katika nafasi zilizopo.
Kwa mujibu wa Taratibu za Utumishi wa umma ni lazima kustaafu(ukifikisha 60yrs)au mtumishi anaweza kustaafishwa kwa manufaa ya umma au mtumishi mwenyewe anaweza kuomba kustaafu kabla ya kufikisha umri wa 60yrs. Katika umri wa 60 yrs mtumishi anatakiwa kwa mujibu wa Sheria kustaafu - Hilo sio ombi na wala huwezi kung'ang'ania.
Ni mfumo upi unaokinzana na mahitaji ya uhalisia? Kama nafasi za ajira zipo 30 na waombaji wenye vigezo wapo 100 utafanyaje? kiUhalisia ni kwamba lazima 70 wakose. Mkuu, hili halina cha siasa - lipo wazi. Kumbuka vijana (wahitimu) ni wengi lakini nafasi zilizopo za kuajiriwa esp.Serikalini ni chache.
 
Ila kuna pepo la kutengenezwa, ili mtu awe na nafanikio kimaisha, anatengeneza pepo la kutesa ndugu zake ili yeye apete. Ni katika ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom