Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Asante kwa mchango wako kaka mkubwa
 
Asante kwa mchango wako kaka mkubwa
Asante mkuu. Naona watu wanajadili jambo hili kwa ushabiki tu wakati hata leo ukienda hapo makao makuu ya NASA unaonyeshwa tu kitengo hicho kinachohangaika na kuchunguza kama kuna asteroid inayotulenga huko...na nini cha kufanya.

Tatizo hata hivyo universe ni kubwa na telescope zao zinaweza kutazama upande mmoja tu kwa wakati. Na maasteroid mengine hasa yale madogo madogo huwa hayaonekani katika makamera yao. Ndiyo maana wanajaribu kuhangaika kuona cha kufanya kama vu bin vu bonge la asteroid hili hapa linakuja moja kwa moja kutugonga....
 
Nimekukubali mzee.. Ukweli ni kwamba watu wapo serious na haya maisha, na hii dunia yetu.
Hakuna pengine pa kukimbilia. Kama asteroid ikija huko imeponyoka kutoka kwenye asteroid belt angalau Homo Sapiens tuwe na la kufanya na siyo kuangamia kibudu tu kama walivyoangamia akina dinosaur.

Tuwaache hawa jamaa wafanye mambo yao na sisi tubakie na ujuaji wetu usio na kichwa wala miguu...

Fikiria mwaka huu bajeti ya NASA ni dola bilioni 23.3. Hii si karibia bajeti yetu nzima kabisa? (Sina uhakika). Halafu utasikia mbongo anasema hawa jamaa wanataka kutupiga. Kuwapiga hela zenu za tozo ama? Au mnazopewa kila siku kama mikopo na misaada?
 
Deep Space Network.. Carlifornia, Madrid and Australia.. Walinishangaza sana wale jamaa wanavyomonitor anga kama wanavyomonitor ndege pale radar za airport..
Ukiachilia mbali kama execution yake itawezekana au lah, lkn ebu fikiria tu the thinking ya kwenda kuidiverge asteroid huko iliko millions of kilometres.. Halafu mpuuzi mmoja ambaye hata uwezo wa milo miwili kwa siku hana na ana miaka 40+ anakuja na hoja nyepesi za kubeza..

Nakumbuka wanasema hizo projects zimehamasishwa zaidi na kilichotokea Russia i think soon before or soon after WW1. Alfajiri vioo vya majengo ya mji mzima vilikuwa vinapigwa na punje ndogo ndogo za kokoto; wakarealize ilikuwa ni jiwe limesagwasagwa wakati linaingia anga la chini la dunia.
Wakaona lazima tuwe tunamonitor space tujue whats going on.
Baada ya kuweza kumonitor, next step ni tunafanyaje sasa kuzuia maafa?😴😴😴
 
Mkuu huyo aliyeitengeneza dunia alikuwa wapi wakati dinosaurs wakisambaratishwa na kile kimondo?
Mkuu hii dunia hauishi peke yako wewe unajali kuhusu wewe sasa hivi na unaona chini ya miguu yako wenzako wanaona miaka 1000 mbele juu ya survival ya race yao na vizazi vyao au leo kungekuwa hakuna simu, magari wala umeme kama wangekuwa na akili kama zako.

Yaani kijiwe kimoja saizi ya mpira ukilinganisha na ukubwa wa dunia ndio kinaweza kushikilia sayari zote seriously?
Trust me bila hawa jamaa wewe usingejua kabisa kwamba unaishi juu ya jiwe kubwa linaloelea kwenye empty space wala usingejua uwepo wa gravity wala uwepo wa sayari so cha kufanya ni kuachia wataalamu na wawaanzilishi wa elimu uliyosoma kufanya wanachokijua.
Wewe endelea kupambaba na tozo na bei za vifurushi.

Hapa ni sawa na mwanafunzi kumwambia mwalimu jinsi ya kufundisha au mgonjwa kumwambia daktari jinsi ya kutibu.
 
Dunia kuzunguka kote huko lakini bado ipo kwenye hatari ya kugongwa...
 
Wewe hayo maswali unayojiuliza leo na kushindwa kujibu wenzako walishajiuliza miaka 200 nyuma na kupata majibu.

Ukiona hivyo basi tambua wewe siyo Albert Einstein, Nikola Tesla wala Isaac Newton hivyo hayo maswali achana nayo na undelee kutafuta ugali sababu hicho ndio pekee waafrika wanaweza fanya kwa usahihi bila kukosa majibu.
 
hawana kitu hao bado watoto sana, kama tu dawa ya covid, ukimwi na vijigonjwa vingine kama hivyo imewashinda wataweza kubadili nini au kufanya lipi la ajabu ktk dunia hii?

kwa kifupi hao wa.she.nzi ni wazee wa kiki na misifa tuu, hawana jipya.
 
Hayo maandiko yameandikwa na haohao unaoona wanayapinga.
Hivi hujui kama dini zililetwa afrika na wakoloni au ukristo na uislamu ulianzishwa na babu zako wa kiafrika?
Je ulishawahi kuona mwafrika mweusi kwenye vitabu vyako vya dini zaidi ya watu weupe?
 
hawana kitu hao bado watoto sana, kama tu dawa ya covid, ukimwi na vijigonjwa vingine kama hivyo imewashinda wataweza kubadili nini au kufanya lipi la ajabu ktk dunia hii?

kwa kifupi hao wa.she.nzi ni wazee wa kiki na misifa tuu, hawana jipya.
Hiyo simu unayotumia unajua ilipotengezwa?

Au uliitengeneza wewe mkuu?
Kama uliitengeneza wewe sema ndio ili nikuulize maswali juu ya huo uvumbuzi wako wa simu.
 
Hiyo wanayofanya ni experiment na sio kwamba hilo jiwe linakuja straight duniani.
Hilo jiwe lipo kwenye orbit yake halina madhara yoyote na dunia.
 
Hao wazungu waliokulisha haya maneno waambie waache ujinga
 
Hilo jiwe lije tu tena lianzie Tanzania maana maisha yamekuwa magumu, kila kitu bei
 
wishfull thinking
 
Hivi unafahamu kwamba annual budget ya NASA ni 22,000,000,000 dollars?
Hiyo ni 22 US billion dollars sawasawa na trilion 45 za kitanzania.
Wewe unazo trilion 45 kwa ajili ya kupata majibu unayoyataka? kama huna kaa kimya.
Na hili andiko halijaandikwa na NASA bali limeandikwa na mtu mmoja mwenye uelewa hafifu na haya mambo hivyo bila shaka hawezi kujua chochote kuhusu jinsi gani NASA wamefanya mpaka kuja na majibu.
Usitumie google bali jifunze kutumia WIKIPEDIA, kule kuna majibu yote kama utakuwa na kichwa cha kuelewa kilichoandikwa.

Otherwise you're manchild asking childish questions.
 
Sababu nimepewa akili na hakuna aliyejibu maswali hayo si wakina Eistein wala kina Tesla.

Huu udhaifu wa kutokuhoji wameshaujua Wanasayansi ndiyo maana wanafanya wanayo yataka sababu wanajua watu hawana muda huo.

Soma habari za kina Albert Einstein na Albert Michelson katika issue ya "How Einstein Kept the Stationary Earth Moving and Took Physics Away From Empiricism to the Fantasies of Imagination". Ujue ni kwa namna gani Einstein alivyo kilaza, kwahiyo suala la kuhoji hatuwezi kuacha sababu uhalisia upo na tunaishi nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…