Kuna sababu gani za wanawake kutoa namba kwa wanaume kisha kuingia mitini (ku-ghost)?

Kuna sababu gani za wanawake kutoa namba kwa wanaume kisha kuingia mitini (ku-ghost)?

Hilo suala la kutoumiza ego mimi ninalipinga kwa sababu atajisikia vibaya wakati huo tu ila baada ya saa moja atakuwa ameshakusahau na amesahau kila kitu ana focus na mawindo mengine, ila ukimpa namba ukam-ghost atakuwa anateseka kwa wiki au miezi akiwa na matumaini hewa ya kitapeli.
Hii ni tabia ya Kiswahili ya kijinga sana.
Jamani Yoda umetapeliwa nini? 😂

Usiassume kuwa ambavyo ungepotezea wewe basi mwingine atapotezea vile vile. Ni survival skill ambayo wanawake tumejifunza since kudeal na wanaume sio kitendo salama.

Siku mkituhakikishia usalama, tutaanza kuwanyima namba macho makavu kabisa.
 
Wanawake sisi tumeumbiwa huruma lakini haimaanishi ndio tumkubali kila mwanaume..!!

Kuna muda unamuonea huruma mwanaume atajisikiaje nikimnyima namba?
Hivyo tunatoa kisha tunapotezea..!!

Unakuta mmekutana kikazi au kibiashara lakini yeye akaingiza feelings zake..!!
Ili usimkwaze unampa namba lakini unajua kabisa simuhitaji..!!
Sahihi!
 
Wanawake ambao huwa wanatoa namba za simu kwa uchangamfu mkubwa tu baada ya kuombwa na wanaume kisha wakishaachana wanawapotezea (ghost) au kujifanya matawi huwa ni wapuuzi wakubwa sana.

Kama huna mpango wa kuwasiliana na mwanaume hakuna haja ya kutoa namba ya simu.
Hutakiwi kumtafuta siku hiyohiuo akikupa namba, kaa kama siku mbili. Ukija kuanza kumcheki punguza kujieleza sana, usitume text kama hajajibu uliyomtumia mwanzo. Kiufupi acha kujifanya una muda mwingi wa kumtafuta pia.

Kupotezewa muda mwingine mnapataka wenyewe
 
Jamani Yoda umetapeliwa nini? 😂

Usiassume kuwa ambavyo ungepotezea wewe basi mwingine atapotezea vile vile. Ni survival skill ambayo wanawake tumejifunza since kudeal na wanaume sio kitendo salama.

Siku mkituhakikishia usalama, tutaanza kuwanyima namba macho makavu kabisa.
Acheni visingizio vya ajabu ajabu kusingizia mnatoa namba under duress kwa usalama wenu, huu ni utapeli tu unaofanyika na wanawake wengi wa mjini. Mtu mmekutana kwenye public bus, SGR, ndege, Bar, sherehe au mitikasi ya biashara hata hujui anapoishi na wengi wao wala hamtakuja kuwahi kuonana tena utamdhuru kivipi hadi atishike alazimike kutoa namba!

Kumbuka hawa sio watu unakutana nao uchochoroni au sehemu tight ukiwa na silaha au nafasi ya kufanya chochote hadi walazimike kutoa namba kwa usalama wao.
 
Sio visingizio ni moja ya sababu.

Zoea kudeal na wanawake wa kila aina.
 
Sio visingizio ni moja ya sababu.

Zoea kudeal na wanawake wa kila aina.
Mimi nafikiri Jamii yetu ya Kitanzania hasa mijini ina wanawake wengi wajinga wajinga sana, hiyo ndio aina kubwa zaidi ya wanawake ninaowaona, badala ya kuwavumilia tu bora waambiwe wabadilike.
 
Back
Top Bottom