Kuna Sauti inanijia kwamba huenda wabunge 19 wa CHADEMA wana baraka za Mwenyekiti kwa makubaliano maalumu kutotoboa siri

..Again, anayeteua wabunge wa viti maalum wa Chadema siyo Katibu Mkuu wa chama, bali ni kamati kuu ambayo bado haijakaa kufanyia uamuzi suala hilo.

Kwanini kamati haikai tangu uchaguzi umekwisha October mpaka leo February? Bunge liwe linawasubiri nyinyi tu? Hampo serious hata kidogo tatizo hamtaki ushauri kuwa mwenyekiti wenu ni kirusi hatari. Muda utaongea
 
Lakini mkuu unafikiri hao akina silinde au halima tuliwadhania kama watakuja kusaliti mapambano????
chadema wanajiona wao pekee ni wamiliki wa mbunge wakati mbunge ni mali ya mwananchi. Mwananchi anaamini pale anapomuona mbunge wake akizungumzia changamoto za jimbo bungeni

Kipindi cha mafuriko ya mwaka jana wabunge wao walisusia bunge kwa maagizo ya chama na huko kilimanjaro, kagera, morogoro nk mito, maziwa yalitapika maji wananchi hawakuwa na wa kuwasemea bungeni wakati wa kujadili bajeti ya miundombinu.

Ulitegemea Rwakatare asiingie bungeni wakati bukoba ilikuwa inazama.
Silinde asiingie bungeni wakati wa kujadili bajeti ya kilimo ukizingatia jimbo lake ni wakulima kweli kweli
Lijualikali jimboni mafuriko kila kona.

Hawa tuwaite wasaliti wa chama au wapiga kura wao.?

Haya ndiyo mambo yaliyochangia chadema kuporomoka
 
Kwanini kamati haikai tangu uchaguzi umekwisha October mpaka leo February? Bunge liwe linawasubiri nyinyi tu? Hampo serious hata kidogo tatizo hamtaki ushauri kuwa mwenyekiti wenu ni kirusi hatari. Muda utaongea

..siyo kweli kwamba Kamati Kuu ya Cdm haijawahi kukaa tangu Oct 2020.

..Kamati Kuu ilishakaa na maamuzi iliyochukua ni kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake.
 
Kuna Kisauti kinanjia Kuhusu Mbowe kubariki Viti Maalumu hapo awali kwa makubaliano ya kuwa siri na kujifanya hana habari.

Hii yaweza kuwa kwa maslahi mapana ya Chama (Ustawi na kutofutika).

Ni mawazo yangu ila tuwaze nje ya Box.

Britannica
Athari za kuparamia viporo vya kande iliyochacha halafumnajiwa na sauti za ajabu ajabu
 
..KATIBA yetu ndivyo inavyoelekeza, Chadema hawajajiamulia wanavyotaka wao.

..Kama kuna kipengele cha Katiba kinachowakwaza basi suluhisho ni kukibadilisha, na siyo kukipuuza kwa kujichukulia maamuzi.
 
..Again, anayeteua wabunge wa viti maalum wa Chadema siyo Katibu Mkuu wa chama, bali ni kamati kuu ambayo bado haijakaa kufanyia uamuzi suala hilo.

..siyo kweli kwamba Kamati Kuu ya Cdm haijawahi kukaa tangu Oct 2020.

..Kamati Kuu ilishakaa na maamuzi iliyochukua ni kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake.

cdm mmekuwa watu wa kutabirika kirahisi sana, tulishawaonya hizi siasa za harakati hamkusikia na bado manendelea nazo. Msijidanganye kwenye mitandao hilo kundi linaungwa na wananchi wengi kuliko mnavyodhani
 
..tatizo ni kwamba Halima na wenzake wameingia bungeni kinyume cha sheria.

..na ni bahati mbaya kwamba Spika wa Bunge anashiriki ktk uvunjaji huo wa sheria.
 
Unadhani kupambana na serikali ya kidikteta iliyo tayari kwa lolote ni rahisi sana? Kabla hujaiona "njaa" pekee, tafuta taarifa za wapinzani wanaopambana na dola kila kukicha hata walio ndani ya CCM halafu upime kama ni hicho unachoita "wachumia tumbo" ndicho tatizo kubwa pekee. Kama unatarajia walio upinzani wawe tayari kujitoa mhanga hata kwa uhai wao basi jiulize kama wewe binafsi ndio msimamo wako thabiti.

Huwezi kuhukumu udhaifu wa upinzani kwa kuona watu binfasi aina za kina Silinde, Lijualikali, Mdee, etc. Angalia pia waliosimama kidete kupambana kama kina Mbowe, Msigwa, Heche, Sugu, Mnyika, Lissu, nk. katika mazingira magumu sana. Usipoona juhudi na ujasiri wa hawa mbele ya dola iliyopania kuua upinzani ni bora uachane na mjadala kuhusu upinzani Tanzania. Ni kama umeshaamua kuungana na Serikali kuponda juhudi zote zinazofanywa na upande huo.
 
We ulikuwa kwenye hiyo kikao ya makubaliano au unaongea pumba tu
 
Bongo bana nchi ya ajabu sometimes na ni kutokana na watu hasa. Hii nchi kuendelea ni ngumu sana kutokana na akili za watu ziko nyuma. Hivi kweli swala kama hili linalohitaji intelijensia ya hali ya juu kulivumbua kama yanayosadikika ni kweli mtu aseme amesikia sauti tumboni mwake hhhhhhhhh serikali muda mwingine tunaionea tu. Hii sio topic ya kuchangia bali ni kijiwe I'm done.
 
Mbona hili tunasema kila siku?

Ni vile tu Mbowe ana wafuasi mbumbumbu, lakini wangekuwa wanajielewa wangeshaagutuka zamani.

Yaani nimecheka kwa nguvu, eti Mbowe ana wafuasi mbumbumbu, halafu kwenye uchaguzi wa ccm Magufuli anapata kura 100% bila hata kura moja kuharibika! Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Mbona chadema wanachukua ruzuku wakati hawatambui matokeo yote?
Chadema ina wenyewe, ndio sababu unaona akina Mdee kwa kupitia viti maalum wako bungeni.Hatuoni Chadema kwenda mahakamani kupinga uwakilishi wa wabunge hao.
 
Hata mwenyekiti kuendelea kubaki madarakani for more than 20 yrs ni mipango, nchi hii ni zaidi ya tuijuavyo. Alikuja slaa akiwa serious yakamkuta, alikuja Tundu Lissu akiwa serious yakamkuta... Lakini mwenyekiti yupo ana survive tu.
Ishu kubwa ya kile chama, wanachama wake hawatofautiani akili na wale wa kijani, hawataki kuwaza nje ya box. Wao kila kitu ni 'tupo pamoja kamanda' wanasiasa wananufaika sana na akili ndogo za watanzania.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Yaani nimecheka kwa nguvu, eti Mbowe ana wafuasi mbumbumbu, halafu kwenye uchaguzi wa ccm Magufuli anapata kura 100% bila hata kura moja kuharibika! Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
Haya mambo wewe huwezi kuelewa maana ni moja ya wafuasi ambao Mbowe anajivunia sana kuwa nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…