Kuna sehemu yenye joto zaidi ya Ifakara Tanzania?

 
Joto la eneo hili hufikia hadi nyuzi joto 40 C, kumbuka hapa Dar halijawahi kuvuka 34 na watu ndio wanapiga kelele hivi

Je, kuna zaidi ya Ifakara kwa joto Tanzania?
Tatizo umesahau concept ya humidity ya geography, Dar inaweza kuwa 33 °C na moshi 40°C , ila Dar ni kisanga kwa sababu ya humidity.
 
Asee asikwambie mtu hakuna sehemu yenye joto kama pale kwa chini kwenye exsozi

Watu wa dar es laam
Nyumba zao zimebanana sana na pia ni kuna asili ya jangwa pia watu ni wengi
 
Kuna mwezi nilienda ifakara nikajisema sasa huu ukijani wote unafaida gani kama joto ndo hivi....nadhani ifakara itakuwa ni bondeni
Ifakara kuna baridi kali sana kwenye season zake.

Ukienda sehemu ukikuta lodge zina heater ujuwe hilo eneo ni la ukanda wa baridi.
 
Wakuu naomba mwongozo kidogo, wakati unaelekea iringa na mbeya ukifika mlima Kitonga huwa kuna kupanda, lakini sasa sijawahi kuona mahali pengine mnenda kuteremka!
Ni kwamba ile mikoa ipo juu?
Morogoro na dar zipo bondeni labda?
Ndio maana ya nyanda za juu, elevation kabla haujaanza kupanda kitonga ni kama 600m abs wakati ukimaliza mlima ni kama 1200 abs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…