hoja yako ina msisimko lakini haina mashiko hebu tuiangalie kwa ukaribu. Rwanda inaingilia Congo kwa njia za kificho, na mara nyingi inakosolewa kimataifa. Tanzania, kwa heshima yake, haiwezi kutumia mbinu za "kuvizia" kama Rwanda. Sisi tuna historia ya kuheshimu sheria za kimataifa, na hatutaki kujifananisha na taifa linalotuhumiwa kufadhili waasi ili kufyonza rasilimali kwa njia za kifisadi.
Kuhusu "wafuga vitambi," tunaweza kuwa nao, lakini uamuzi wa kupeleka jeshi Congo si suala la kula madini tu. Tukifanya hivyo bila mipango madhubuti, tunaweza kuishia kuonekana kama wavamizi badala ya waokozi. Kujenga msingi wa kijeshi Congo ni rahisi kusema, lakini ni ghali kwa vitendo, hasa bila ushirikiano wa kweli wa Congo na jamii ya kimataifa.
Tanzania ina fursa ya kusaidia kwa mkataba, lakini sio kwa njia za "Rwanda style." Tunahitaji mipango thabiti, si haraka za kuchota madini huku tukihatarisha amani yetu wenyewe. Tukishindwa, hatutakula madini; tutakula aibu.