Asijichanganye kukutana na mimi ataacha ndala kwa maswali ntakayo muulizaWakuu, kuna jambo nimekuwa nikilitafakari sana.
Katika maisha haya tunahangaika kutafuta pesa, heshima, mali, nafasi na kutambulika. Tunajenga nyumba, tunanunua magari, tunatafuta followers na tunataka watu wajue tumefanikiwa.
Lakini kuna siku kila mmoja wetu ataondoka hapa duniani akiwa hana chochote alichokusanya.
Utakutana na Mungu ukiwa peke yako.
Hakutakuwa na marafiki wa kukusifia, pesa za kukusaidia, cheo cha kukulinda wala mali za kukufuata.
Kilichobaki ni matendo yako.
Ulimsaidia nani ulipokuwa na uwezo?
Ulimsamehe nani?
Ulimuumiza nani bila sababu?
Ulimnyanyasa nani kwa sababu ulikuwa na uwezo?
Na pale ulipokuwa huna kitu, uliwezaje kubaki na moyo wa kumtegemea Mungu?
Nadhani wakati mwingine tunahitaji kupunguza mbio za dunia na kujitazama ndani.
Maisha ni mafupi sana. Leo tunazungumza, kesho mtu anaulizia ulikuwa wapi.
Tafuteni dunia, lakini msimsahau Mungu. Tafuteni mafanikio, lakini msipoteze utu. Na mkipewa uwezo, tumieni kuwainua wengine.
Mwisho wa safari, tunarudi pale tulikotoka.
Mungu atupe mwisho mwema, moyo safi na maisha yenye maana. Ameen.
Kwa nini aliruhusu ubatili utokeeUbatili aliuleta mwanadamu kupitia dhambi mkuu
Falsafa ya uthibitishoNi kweli kwamba hisia au uzoefu wa mtu pekee hauwezi kuwa ushahidi wa kutosha kuthibitisha uwepo wa Mungu. Lakini kwa upande mwingine, kutokuwepo kwa ushahidi unaokuridhisha wewe hakumaanishi moja kwa moja kwamba Mungu hayupo. Hoja ya msingi ni kutofautisha kati ya imani, madai na ushahidi—kila upande una haki ya kuuliza ushahidi na kuhoji hoja za upande mwingine.
Burden of proof ni kwa mdai, nakubaliana. Lakini kushindwa kwako kuiona au kuikubali evidence hakubadilishi “haijathibitishwa kwako” kuwa “Mungu hayupo.” Kutokuwepo kwa ushahidi si ushahidi wa kutokuwepo.Falsafa ya uthibitisho
(Burden of proof philosophy) inamtaka anayeanza kudai kitu kipo ndio mwenye mzigo wa kuthibitisha madai hayo.
Ndio maana polisi wakidai una madawa ya kulevya, Wao wanaodai ndio wenye mzigo wa kuthibitisha madai hayo, na sio wewe mtuhumiwa.
Vivyo hivyo, nyie mnaodai Mungu yupo ndio wenye mzigo wa kuthibitisha kwamba yupo, kwa sababu madai ya kwamba Mungu yupo ni madai yenu. Na yalianzia kwenu nyie waamini Mungu.
Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo, ni kwamba madai yako ni ya uongo, na huyo Mungu unayedai yupo, hayupo.
Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.
Chochote kinachodaiwa bila uthibitisho kinaweza kutupiliwa mbali bila uthibitisho.
Hivyo, huwezi kutaka uthibitisho wa kwamba Mungu hayupo, wakati wewe mwenyewe unayedai yupo huwezi kuthibitisha kwamba yupo.
Mungu angekuwa ameumba mwanadamu mkamilifu, mwanadamu asingeweza kubadilika kuwa muasi na mtenda dhambi.MUNGU alimuumba mwanadamu mkamilifu aliye huru na maamuzi ya kufikiri... na hakuumba roboti la kumtii tu kwa shurti.
Sasa thibitisha Mungu yupo.Burden of proof ni kwa mdai, nakubaliana. Lakini kushindwa kwako kuiona au kuikubali evidence hakubadilishi “haijathibitishwa kwako” kuwa “Mungu hayupo.” Kutokuwepo kwa ushahidi si ushahidi wa kutokuwepo.
Mungu si kitu cha maabara ukampime kama kemikali. Imani inaegemea dalili, mantiki na ushahidi unaoutafsiri wewe. Kama huamini, ni sawa—lakini kutokuwepo kwa ushahidi unaokuridhisha si sawa moja kwa moja na kuthibitisha kwamba Mungu hayupo.Sasa thibitisha Mungu yupo.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.Mungu si kitu cha maabara ukampime kama kemikali. Imani inaegemea dalili, mantiki na ushahidi unaoutafsiri wewe.
Kama kutokuwepo kwa ushahidi sio ushahidi wa kutokuwepo.Kama huamini, ni sawa—lakini kutokuwepo kwa ushahidi unaokuridhisha si sawa moja kwa moja na kuthibitisha kwamba Mungu hayupo.
Asante kwa ujumbe mzuri. Barikiwa sanaWakuu, kuna jambo nimekuwa nikilitafakari sana.
Katika maisha haya tunahangaika kutafuta pesa, heshima, mali, nafasi na kutambulika. Tunajenga nyumba, tunanunua magari, tunatafuta followers na tunataka watu wajue tumefanikiwa.
Lakini kuna siku kila mmoja wetu ataondoka hapa duniani akiwa hana chochote alichokusanya.
Utakutana na Mungu ukiwa peke yako.
Hakutakuwa na marafiki wa kukusifia, pesa za kukusaidia, cheo cha kukulinda wala mali za kukufuata.
Kilichobaki ni matendo yako.
Ulimsaidia nani ulipokuwa na uwezo?
Ulimsamehe nani?
Ulimuumiza nani bila sababu?
Ulimnyanyasa nani kwa sababu ulikuwa na uwezo?
Na pale ulipokuwa huna kitu, uliwezaje kubaki na moyo wa kumtegemea Mungu?
Nadhani wakati mwingine tunahitaji kupunguza mbio za dunia na kujitazama ndani.
Maisha ni mafupi sana. Leo tunazungumza, kesho mtu anaulizia ulikuwa wapi.
Tafuteni dunia, lakini msimsahau Mungu. Tafuteni mafanikio, lakini msipoteze utu. Na mkipewa uwezo, tumieni kuwainua wengine.
Mwisho wa safari, tunarudi pale tulikotoka.
Mungu atupe mwisho mwema, moyo safi na maisha yenye maana. Ameen.
Ni kweli, mtu anaweza kuamini hata kitu cha uongo. Lakini hilo halithibitishi kwamba kila kitu kisichoonekana ni uongo. Ndiyo maana tunatofautisha kati ya imani, ushahidi na hitimisho.Kuamini unaweza kuamini hata uongo.
Unaweza kuwa na imani ya kitu cha uongo.
Sasa unathibitishaje kwamba imani yako ya huyo "Mungu" ni ukweli na sio uongo?
Hapo ndipo tunapotumia ushahidi na mantiki. Huwezi kusema “hakipo” kwa uhakika kwa sababu tu hujakiona, lakini pia huwezi kusema “kipo” kwa sababu tu huwezi kuthibitisha hakipo. Madai makubwa yanahitaji ushahidi unaoyaunga mkono.Kama kutokuwepo kwa ushahidi sio ushahidi wa kutokuwepo.
Sasa, Tutajuaje kwamba kitu hakipo kwa sababu ni kweli hakipo au kipo ila tu umekosekana uthibitisho wa kuthibitisha kipo?
Tutajuaje kwamba kitu hakipo kwasababu ni kweli hakipo, Au kipo ila tu, umekosekana uthibitisho wa kuthibitisha kipo?Ni kweli, mtu anaweza kuamini hata kitu cha uongo. Lakini hilo halithibitishi kwamba kila kitu kisichoonekana ni uongo. Ndiyo maana tunatofautisha kati ya imani, ushahidi na hitimisho.
Huwezi kujua kwa 100% kila kitu hakipo. Ndiyo maana tunasema: mzigo wa kuthibitisha dai uko kwa anayesema kitu kipo. Kama hakuna ushahidi wa kutosha, jibu sahihi ni “sijui”, si kulazimisha kusema kipo wala hakipo.Tutajuaje kwamba kitu hakipo kwasababu ni kweli hakipo, Au kipo ila tu, umekosekana uthibitisho wa kuthibitisha kipo?
Kwa sababu harazimishi umtii kwa shurti, anatuacha tuchague kwa upendo wetu!!!Kwa nini aliruhusu ubatili utokee
Kitu kinaweza kuwepo na kisionekane.Hapo ndipo tunapotumia ushahidi na mantiki. Huwezi kusema “hakipo” kwa uhakika kwa sababu tu hujakiona.
Extraordinary claims require Extraordinary evidences.lakini pia huwezi kusema “kipo” kwa sababu tu huwezi kuthibitisha hakipo. Madai makubwa yanahitaji ushahidi unaoyaunga mkono.
Kwa nini alimruhusu shetani dunianiKwa sababu harazimishi umtii kwa shurti, anatuacha tuchague kwa upendo wetu!!!
Wewe ulijuaje kwa 100% Mungu yupo?Huwezi kujua kwa 100% kila kitu hakipo. Ndiyo maana tunasema: mzigo wa kuthibitisha dai uko kwa anayesema kitu kipo. Kama hakuna ushahidi wa kutosha, jibu sahihi ni “sijui”, si kulazimisha kusema kipo wala hakipo.
Kama ambavyo umasikini sio sifa na utajiri pia sio sifa.Fedha,Magari na Majumba ni vitu vya kupita tu,
Ila hakikisha kua vinapitia na kwako kabla mauti hayajakukuta,
Hatukuumbwa ili tuteseke wala kuteseka sio sifa,
Masikini hua wanafarijika sana wakikumbuka kua hata tajiri nae atakufa,
Kwa sababu MUNGU ni upendo... na alimuacha aoneshe utawala wake jinsi ulivyo baada ya kudai. Utawala wa MUNGU sio wa hakiKwa nini alimruhusu shetani duniani