Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

Unaposema "kutokujua sababu ya Mungu kuruhusu uovu" ume conclude Mungu yupo.

Wakati hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo kwanza ndiyo uweze kuongelea sababu za Mungu, kwa sababu, kama Mungu hayupo, suala zima la sababu za Mungu halipo. Mungu ambaye hayupo hawezi kuwa na sababu.

Kimantiki, uwepo wa maovu unapingana moja kwa moja na uwepo wa Mungu huyo, kwa sababu, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, na upendo wote, ana kila ujuzi, kila uwezo na kila upendo wa kuumba ulimwengu usiowezekana kuwa na maovu.

Sasa kwa nini aumbe ulimwengu ambao maovu yanawezekana kuwepo?

Hapo uwepo wa maovu ni direct contradiction ya uwepo wa huyo Mungu.

Na kama kuna sababu ya yeye kuumba ulimwengu unaowezekana ki
uwa na maovu, itaje tuijadili.

Kusema tu hatujui sababu za Mungu kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na maovu si hoja ya utetezi kuonesha Mungu yupo.

Kwa sababu inawezekana hatujui sababu za Mungu kuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na maovu kwa sababu Mungu hayupo na hajaumba ulimwengu.
 
Hoja yako ina nguvu, lakini “uwepo wa uovu” si uthibitisho wa moja kwa moja kwamba Mungu hayupo.

Unachohitaji kuonyesha ni kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kabisa kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu uovu.

Ukithibitisha hilo, hapo contradiction yako inakuwa nzito zaidi. Lakini kusema “kuna uovu, kwa hiyo Mungu hayupo” bado ni hitimisho linalohitaji hoja ya ziada.
 
Ukifikiria Hivi kuna Kiwango Kikubwa cha Uelewa Unakuwa Umefikia.

Yesu hakujenga, Hakukusanya Mali zake binafsi wala Hakuwa na Tamaa za Mali za Dunia hii maana Alipita Kiwango Kikubwa cha Hekima na Uelewa kuliko Binadamu yeyote yule.

Kuna Mtu anaua ili apate mali ambayo ataiacha , Kuna Mtu anashinda kwa Waganga kutafuta Cheo kazini , Kuna Watu wanazini na Kila Mwanamke hadi wake za Watu ili Wabaki na Heshima Fulani waliyoingia nayo Mikataba ya Giza...haya Yote Mbele za Mungu Utajibu
 
Hilo najua kwamba nimetokana na wazazi wangu na watoto wangu watatokana na mimi na mama yao
Unajua au hujui unaweza kuzaliwa na changamoto kutokana na uzembe wa mzazi wakati wa ujauzito kama kuzaliwa njiti n.k na wewe hujafanya chochote?
 
Kweli kabisa. Hekima ya kweli si kujua namna ya kupata mali tu, bali kujua thamani ya maisha na mwisho wake. Mali, cheo na sifa vinaisha; matendo ndiyo hubaki. Ndiyo maana kila mtu atawajibika kwa alichochagua mbele za Mungu. 🙏✍️
 
Inawezekana mungu mwema mwenye nguvu zote akaruhusu uovu na mateso ?
 

Kwahiyo Ukiwa na Majumba na Magari ndio Hatoteseka. Hujui Ili Binadamu asiteseke anahitaji MAJI NA CHAKULA tu.

Hakuna Ambaye aliyekosa Fedha , Magari na Majumba Akateseka . ila Wapo waliokosa Chakula na Maji wakateseka

Kichaa, Ombaomba , Na Wale Wahazabe kule Porini Hawana hata Fedha wala Magari ila Wana CHAKULA NA MAJI na Kuna Uwezekano wanaishi Kwa FURAHA kuliko Wewe
 
Inawezekana mungu mwema mwenye nguvu zote akaruhusu uovu na mateso ?
Ndiyo, inawezekana—kwa mtazamo wa imani, uwepo wa uovu haukanushi moja kwa moja uwepo wa Mungu.

Hoja kubwa ni kwa nini Mungu mwenye uwezo wote anaruhusu uovu, na hapo ndipo mijadala ya imani, uhuru wa kuchagua na kusudi la maisha inapokuja.
 
Umewaza parefu mkuu 🙏🏽 🙏🏽
Dunia si mali yetu hakika tunapita njia tu,,, 🚶
 
Tunaosema Mungu yupo Yuko wengi Sana.
Mungu yupo.
Mungu yupo
Mungu yupo...
Sasa hii inaitwa "popularity fallacy"

Kwa kilatini argumentum ad populum.

The popularity fallacy, occurs when someone claims that an idea or product is true simply because a large number of people believe in or use it.

Yani mtu anakubali na kuamini Mungu yupo, simply because majority ya watu wanaamini hivyo. Na yeye anaunga tela.

Lakini in reality, majority sio kipimo cha kuhitimisha kitu kipo. Kwa sababu hata kundi kubwa la watu, linaweza kuamini uongo vilevile.
 
Kwani wewe unaongelea mateso gani hapa?
Umetaja vitu ambavyo ni vya lazima ili binadamu aishi,
Umewahi kusikia mtu kakosa matibabu kisa hana hela?

Upo serious kweli kua masikini na matajiri wanateseka sawa au unataka tu kujifariji?
 
Mwisho wa safari, tunarudi pale tulikotoka.

Mungu atupe mwisho mwema, moyo safi na maisha yenye maana. Amee
n.
 
Unajua au hujui unaweza kuzaliwa na changamoto kutokana na uzembe wa mzazi wakati wa ujauzito kama kuzaliwa njiti n.k na wewe hujafanya chochote?
hakuna uzembe wala nini
ndomaana mzazi mmoja anaeza kuzaa tasa na mwingie ana uwezo wa kuzaa
 
Umewaza parefu mkuu 🙏🏽 🙏🏽
Dunia si mali yetu hakika tunapita njia tu,,, 🚶
Kweli kabisa mkuu 🙏🏽 Dunia ni kituo, si makazi ya milele. Tunapita tu, muhimu tuache alama njema kabla safari haijaisha. 🤝🏽
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…