Bwana Tony Cipriano
JF-Expert Member
- Nov 17, 2022
- 4,401
- 9,555
dah siku hiyo ole wangu mimi mlevi
Mimi nimemjibu aliyesema hakuna Mungu. Usikomenti bila kujua hili jibu linahusu swali gani.Kwa MUNGU haangalii wingi.
Wakati wa nuhu wa 8 pekee waliokoka, kwa sodoma na gomora ni luthu na binti zake.
MUNGU anahukumu kwa haki na sio kwa wingi mkuu kadhi
KivipiMungu ni ROHO!
Hoja yako ina nguvu kama tukikubali kwamba Mungu mwenye uwezo na upendo wote hana sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Lakini hapo ndipo mjadala ulipo: kuwepo kwa uovu hakuthibitishi moja kwa moja kutokuwepo kwa Mungu; kunahitaji kwanza kuthibitisha kwamba hakuna sababu yenye mantiki ambayo Mungu angeweza kuwa nayo ya kuuruhusu. Hivyo umeonyesha tatizo la uovu, si uthibitisho wa mwisho kwamba Mungu hayupo.Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kimantiki hatakiwi kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu ulimwengu unaoweza kuwa na uovu.
Kwa nini?
Kwa sababu, tunapata maswali ya kuchunguza yanayotuonesha hivyo.
Kimantiki, sababu hii ya Mungu huyo kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu inaweza kuwa ndani ya uwezo wake au nje ya uwezo wake Mungu.
1. Je, sababu hiyo ipo nje ya uwezo wake Mungu?, kwamba hawezi kuibadilisha inambidi aumbe ulimwengu unaoruhusu maovu tu, analazimika, hata kama hakutaka? Yani ni kama kuna logic fulani, tuseme kama ya kimahesabu, ambayo inamlazimisha Mungu akitaka kuumba ulimwengu tu, basi lazima akubali maovu yaweze kuwapo katika ulimwengu huo, Mungu hawezi kuepuka hilo?
Kama ni hivyo, basi huyo si Mungu muweza yote, kwa sababu kuna hii sababu ambayo iko nje ya uwezo wake, imemlazimisha aumbe ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya hata kama hakutaka.
Au
2. Sababu hii ya kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya ipo ndani ya uwezo wake Mungu, angeweza kuibadilisha tu, kuiondoa tu, aumbe ulimwengu usioruhusu maovu, yeye ni Mungu muweza yote, lakini kakataa kuibadilisha tu, kaamua kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu?
Kama ni hivyo, basi huyu si Mungu mwenye upendo wote, kwa sababu maovu yanaumiza wengi, wakati Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na maovu na hakuna kiumbe chake kitakachoumizwa na maovu. Mungu mwenye upendo wote kimantiki hatakiwi kuruhusu ulimwengu unaoruhusu maovu kama anaweza kuumba ulimwengu usioruhusu maovu.
Either way, sababu ikiwa ndani ya uwezo wake, au nje ya uwezo wake, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu unaoruhusu maovu, contradiction hii ina mutual exclusivity kwamba;
1. Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu unaoruhusu maovu haupo,
2. Ama ulimwengu unaoruhusu maovu upo na Mungu huyo hayupo.
Ulimwengu unaoruhusu maovu upo. Ndiyo huu tunaoishi.
Hivyo,
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Hana mwili...Kivipi
YESU anaweza kukuokoa mkuu Bwana Tony Ciprianodah siku hiyo ole wangu mimi mlevi
Umeshindwa kuelewa, au huna kabisa uwezo wa kuelewa, au unabisha kwa ligi tu.Hoja yako ina nguvu kama tukikubali kwamba Mungu mwenye uwezo na upendo wote hana sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Lakini hapo ndipo mjadala ulipo: kuwepo kwa uovu hakuthibitishi moja kwa moja kutokuwepo kwa Mungu; kunahitaji kwanza kuthibitisha kwamba hakuna sababu yenye mantiki ambayo Mungu angeweza kuwa nayo ya kuuruhusu. Hivyo umeonyesha tatizo la uovu, si uthibitisho wa mwisho kwamba Mungu hayupo.
Kivip, ana nini?Hana mwili...
Sawa mkuu nimependa uvumilivu wako, Big up🫡
Nimekuelewa vizuri. Lakini tofauti iko kwenye hatua moja: contradiction unayoonyesha inategemea premise kwamba Mungu mwenye sifa hizo hawezi kabisa kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Hilo ndilo linalohitaji kuthibitishwa, si kuchukuliwa kama hitimisho.Umeshindwa kuelewa, au huna kabisa uwezo wa kuelewa, au unabisha kwa ligi tu.
Uovu kuwapo ulimwenguni una contradict sifa za Mungu. Hii ni contradiction ya core characteristic za Mungu si suala superficial tu.
Nimeeleza kirefu kwamba nimekuonesha kuwa sababu yoyote ambayo Mungu angeweza kuwa nayo ya kuuruhusu uovu ina contradict sifa zake za uungu, ujuzi wa yote, uweza wa yote na upendo wote.
Ngoja niweke mjadala huu katika Euclidean geometry labda utaeleweka zaidi.
Yani katika Euclidean geometry ukishakubali na kuthibitisha hili ni duara, kukubali na kuthibitisha tu kuwa hili ni duara kumesha contradict uwezekano wa hilo duara kuwa pembetatu, kwa sababu sifa za duara zina contradict sifa za pembetatu.
Duara lina nyuzi 360, pembetatu ina nyuzi 180.
Duara halina pembe, pembetatu ina pembe tatu.
Sasa, wewe unachosema hapo ni kwamba, sifa za duara ku contradict duara hilo hilo kuwa pembetatu kwa wakati huohuo si uthibitisho kwamba hakuna duara ambalo hapo hapo ni pembetatu.
Ni kweli, hakuna mwanadamu aliye na uhakika wa moja kwa moja kuhusu yatakayotokea baada ya kifo. Ndiyo maana tunaita suala hili imani, si jambo tuliloliona kwa macho.Umejuaje tutakutana na Mungu?🤔
Unajua hayo masuala ni 50/50
Who knows? Labda after death ndiyo the end, the end of you and your existence.