Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Sawa,Ndiyo, kwa muktadha wa huyo Mungu unayemjadili, nakubali hizo ni definitive characteristics—yaani sifa zinazomfafanua huyo Mungu.
Lakini kukubali definition yake si kukubali kwamba Mungu huyo hayupo.
Hapo bado tunahitaji hoja ya hatua inayofuata.
Kama hizo ni definitive and definitional characteristics, kwamba bila hizo kuwapo Mungu huyo hayupo, tukigundua kuwa hizo characteristics haziwezi kuwapo, haziwezekaniki, zina contradictions zinazozifanya zisiweze kusimama, ni za kufikirika na kusemekana tu kama mtu anavyoweza kusema "pembetatu duara" lakini kiuhalisia katika Euclidean geometry hiyo pembetatu duara haiwezekani kuwapo, huyo Mungu ataweza kuwapo?
Definitional characteriatics za Mungu zikiwa contradicted na kuonekana haziwezekani kuwapo, Mungu huyo wa hizo definigmtional characteristics anaweza kuwapo bado?
Yani kwa nfano mimi nimezaliwa mwaka 2000 AD. Na kabla ya hapo sijawahi kuwapo.
Halafu definitional characteristic ya Mungu ni kwamba hakuzaliwa na kauumba ulimwengu mabilioni ya miaka nyuma huko.
Sasa hapo mimi nikikwambia kuwa mimi, niliyezaliwa mwaka 2000, ambaye sijawahi kuwapo huko nyuma kabla ya mwaka 2000 AD, ndiye Mungu niliyeuumba ulimwengu, utakubali kuwa mimi ndiye Mungu niliyeuumba ulimwengu? Utasema kuwa huwezi kujua namna ambayo inawezekana nimezaliwa mwaka 2000 AD, lakini pengine nimeweza kuuumba ulimwengu huu mabilioni ya miaka iliyopita, kwamba hii contradiction ya timeline haithibitishi kwamba mimi si Mungu niliyeuumba ulimwengu huu?