Nimekuelewa vizuri. Lakini tofauti iko kwenye hatua moja: contradiction unayoonyesha inategemea premise kwamba Mungu mwenye sifa hizo hawezi kabisa kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Hilo ndilo linalohitaji kuthibitishwa, si kuchukuliwa kama hitimisho.
Kwa hiyo hoja yako inaonyesha changamoto kubwa kwa dhana ya Mungu huyo, lakini bado si contradiction ya kimantiki mpaka premise hiyo ithibitishwe. Hapo ndipo tunatofautiana.
Ni hivi.
Mungu, kidhana na kimantiki, ana characteristics fulani. Bila hizi characteristics anakuwa si Mungu.
Kama vile katika Euclidean geometry, pembe tatu ni lazima iwe na pembe tatu (ndiyo maana ikaitwa pembetatu), ni lazima iwe na nyuzi 180.
Umbo likikosa sifa hizi, hilo si pembetatu.
Kwa muktadha wetu hapa, kwa kuanzia, kidhana na kimantiki, Mungu ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.
Yeyote atakayekosa sifa hizo si Mungu.
Ukiweza ku contradict sifa yoyote kati ya hizo, ukaonesha haziwezekaniki, utakayebaki naye si Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Ulimwengu wenye kuruhusu uovu kuweza kuwapo tu, ume contradict sifa hizi za Mungu kuwapo, nimeeleza hapo juu.
Kwa mantiki ya mutual exclusivity nimeeleza maana ya ulimwengu huu kuwapo kuwa ni
1. Ama suala la ulimwengu kuweza kuwa na ubaya lipo nje ya uwezo wa Mungu. Kwamba Mungu hakuwa na jinsi, katika kuumba ulimwengu alilazimika kuuumba ulimwengu ukiwa na uwezo wa kuwa na ubaya. Hii ina contradict sifa ya uweza yote ya Mungu. Mungu muweza yote halazimiki kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya. Hivyo ukisema alilazimika, huyo si Mungu muweza yote.
2. Ama suala la ulimwengu kuweza kuwa na mabaya lipo ndani ya uwezo wa Mungu, Mungu muweza yote aliweza kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya, ila hakutaka tu. Kama ni hivyo, hili nalo lina contradict sifa ya Mungu ya kuwa na upendo wote. Kuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usioweza kuwa na mabaya halafu kuumba ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya ni ukatili kwa viumbe wengi watakaoumizwa na mabaya hayo, ukatili huu una contradict sifa ya Mungu mwenye upendo wote.
Mungu mwenye upendo wote si mkatili, na mkatili hawezi kuwa Mungu mwenye upendo wote.
Ukisema vyovyote, kwamba sababu za Mungu kuumba ulimwengu unaoruhusu kuwa na mabaya zilikuwa ndani ya uwezo wa Mungu au nje ya uwezo wa Mungu, ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya una contradict sifa za Mungu kwa namna ya msingi kabisa, una contradict sifa za Mungu kwa namna inayomfanya Mungu huyo asiweze kuwapo.
Hii ni aina ya contradiction ya definitive characteristics. Si superficial, ni fundamental.
Hii ni contradiction ya aina ya "pembetatu haiwezi kuwa duara hapohapo katika Euclidean geometry, kwa sababu sifa zinalolifanya umbo kuwa pembetatu zinalikataza umbo hilo kuwa duara".
Kwa hivyo umbo ama ni pembetatu, ama ni duara, hatuwezi kuwa na pembetatu ambayo pia ni duara kwa wakati mmoja.
The two are mutually exclusive.
Kama vile ambavyo, ama tunaweza kuwa na ulimwengu unaoweza kuwa na maovu bila ya kuwa na Mungu, ama tunaweza kuwa na Mungu bila ya kuwa na ulimwengu unaoruhusu maovu.
Hatuwezi kuwa na Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, halafu wakati huo huo tukawa na ulimwengu unaoruhusu maovu.
The two are mutually exclusive.
Ulimwengu unaoruhusu maovu tunao, ndio huu tunaoishi.
Hivyo, Mungu hayupo.