Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

Sikudai namjua Mungu kwa 100% kwa maana ya kumwona au kujua kila kitu kumhusu. Ninasema naamini Mungu yupo kutokana na sababu na ushahidi ninaouona. Kutokujua kila kitu kuhusu kitu hakumaanishi kitu hicho hakipo.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa unathibitishaje imani yako kuhusu Mungu huyo ni ukweli na si uongo?

Unathibitisha vipi kwamba imani yako ya kwamba "Mungu yupo" ni imani ya kweli na si uongo?
 
Mwisho wa safari, tunarudi pale tulikotoka.

Mungu atupe mwisho mwema, moyo safi na maisha yenye maana. Amee
n.
Ameen mkuu 🙏🏽 Hakika mwisho wa safari kila mmoja atarudi alikotoka.

Cha msingi ni kuishi kwa wema, unyenyekevu na kuacha alama njema. Mungu atupe mwisho mwema sote. 🤲🏽
 
Wingi ni kipimo cha kukubalika kwa Jambo. Tukiwa wengi tukamchagua Mungu tukawashinda ambao hamkumchagua Mungu, tunaoshinda tutawaongoza walioshindwa ujue.
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa unathibitishaje imani yako kuhusu Mungu huyo ni ukweli na si uongo?

Unathibitisha vipi kwamba imani yako ya kwamba "Mungu yupo" ni imani ya kweli na si uongo?
Wewe unathibishaje kwamba hayupo wakati waliomuona waliandika kuthibitisha?
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa unathibitishaje imani yako kuhusu Mungu huyo ni ukweli na si uongo?

Unathibitisha vipi kwamba imani yako ya kwamba "Mungu yupo" ni imani ya kweli na si uongo?
Hoja yako ni ya msingi mkuu. Imani peke yake si uthibitisho; ndiyo maana mtu anaweza kuamini kitu cha kweli au cha uongo. Kwa upande wa Mungu, mtu hutazama ushahidi, mantiki na uzoefu kisha hufanya hitimisho lake. Lakini kusema “siwezi kuthibitisha” hakumaanishi moja kwa moja “hakipo.” Hapo ndipo mjadala ulipo.
 
Wingi ni kipimo cha kukubalika kwa Jambo. Tukiwa wengi tukamchagua Mungu tukawashinda ambao hamkumchagua Mungu, tunaoshinda tutawaongoza walioshindwa ujue.
Kwa MUNGU haangalii wingi.

Wakati wa nuhu wa 8 pekee waliokoka, kwa sodoma na gomora ni luthu na binti zake.

MUNGU anahukumu kwa haki na sio kwa wingi mkuu kadhi
 
Ndiyo, inawezekana—kwa mtazamo wa imani, uwepo wa uovu haukanushi moja kwa moja uwepo wa Mungu.

Hoja kubwa ni kwa nini Mungu mwenye uwezo wote anaruhusu uovu, na hapo ndipo mijadala ya imani, uhuru wa kuchagua na kusudi la maisha inapokuja.
Siongelei mtazamo wa imani, mtazamo wa imani unaweza kuamini chochote, unaweza kuamini hata mungu amekutuma uue watu ili uende mbinguni. Mimi nazungumzia katika mantiki(logic) inawezekana mungu mwema na mwenye nguvu akaruhusu uwepo wa uovu na mateso??
iulize tena AI tuone majibu yake.
 
Wewe unathibishaje kwamba hayupo wakati waliomuona waliandika kuthibitisha?
Kisichokuwepo hakithibitishiki.

Kwa sababu hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.

Maandiko yaliyo andikwa kwamba ni ya Mungu ni mengi sana.

Wengi waliandika na wakadai ni maandiko ya Mungu.

Kuna andiko la Biblia, Quran, Torah, The Vedas, Tripitaka, The Kojik, The Guru Granth Sahib na mengineyo mengi.

Sasa Mungu gani anakuwa na Maandiko mengi yanayo tofautiana na kupingana yenyewe kwa yenyewe katika kuelezea uwepo wake?
 
Sasa kama umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo, na hapohapo unakataa kwamba hayupo, sasa unasimama upande upi?
 
Katika muktadha wa mantiki, uwezekano wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na uovu, ni contradiction.

Hii contradiction ni sawa na kusema kwamba, katika Euclidean geometry, unaweza kuwa na pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.

Characteristics za pembetatu, kimantiki, zina contradict uwezekano wa pembetatu jiyo hiyo kuwa duara.

Pembetatu ina nyuzi 180, duara lina nyuzi 360.

Pembetatu ina pembe tatu, duara halina pembe.

Hivyo, in Euclidean geometry, hakuna oembetatu ambayo pia ni duara.

Vivyo hivyo, characteristics za Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, zina contradict Mungu huyo kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu.

Kusema kuwa hatujui sababu za Mungu kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu ni sawa na kusema inawezekana kuna pembetatu ambayo ni duara katika Euclidean geometry, ila hatujaijua tu.

Hatuhitaji kujua pembetatu zote ili kujua katika Euclidean geometry hakuna pembetatu ambayo ni duara pia, tukizijua core characteristics za pembetatu na za duara tu, tunaweza kujua kuwa katika Euclidean geometry, pembetatu haiwezi kuwa duara.

Vivyo hivyo, hatuhitaji kujua sababu zote za Mungu ili kujua kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya ni contradiction, na contradiction hii kuiondoa kuna mutual exclusivity.

Maana yake ama Mungu huyo yupo na ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya haupo, ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo na Mungu huyo hayupo.

Ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo.

Mungu huyo hayupo.
 
Mungu wa Ibrahim (Wa Wakristo na Waislamu) hayupo. Mantiki tu inakataa uwepo wake kabla hata hatujaongelea ushahidi wowote wa uwepo wake.
 
Hapo ndipo mjadala wa mantiki ulipo. Kama Mungu ni mwema kabisa, anajua yote na ana uwezo wote, swali la msingi ni: kwa nini aruhusu uovu na mateso wakati angeweza kuyazuia? Hilo ndilo tunalopaswa kulijadili kimantiki, si kwa kudhani tu jibu kutokana na imani.
 
Hoja yako ina nguvu, lakini kuna hatua moja muhimu: contradiction haijathibitishwa mpaka ionyeshwe kwamba Mungu mwenye sifa hizo hawezi kuwa na sababu yoyote ya kimantiki ya kuruhusu uovu. Kusema “hatuijui sababu” si uthibitisho kwamba sababu hiyo haiwezi kuwepo. Kwa hiyo problem of evil ni challenge kubwa kwa dhana hiyo ya Mungu, lakini si contradiction ya moja kwa moja kama “pembetatu ni duara” bila premise hiyo kuthibitishwa.
 
Mungu wa Ibrahim (Wa Wakristo na Waislamu) hayupo. Mantiki tu inakataa uwepo wake kabla hata hatujaongelea ushahidi wowote wa uwepo wake.
Mantiki inaweza kuhoji kama sifa tunazopewa za Mungu zinaendana, lakini kusema “mantiki imethibitisha Mungu hayupo” ni hitimisho kubwa zaidi.

Hoja ya uovu ni changamoto kwa dhana ya Mungu mwenye uwezo, ujuzi na upendo wote, lakini bado inahitaji premises zake kuthibitishwa.
 
Sasa kama umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo, na hapohapo unakataa kwamba hayupo, sasa unasimama upande upi?
Msimamo wangu ni huu: naamini Mungu yupo, lakini siwezi kudai kwamba nimeuthibitisha uwepo Wake kwa kipimo cha maabara. Imani yangu ina sababu na hoja ninazoziona zina maana, huku nikikubali kwamba maswali ya kimantiki bado yanaweza kujadiliwa. Kuamini si sawa na kudai nimejua kila kitu.
 
Mungu huyo characteristic zake zinafanya asiumbe ulimwengu unaoruhusu maovu.

Kwa sababu, ana uwezo wote wa kuumba ulimwengu anaoutaka.

Ana ujuzi wote wa kuumba ukimwengu anaoutaka.

Ana upendo wote wa kuzuia ulimwengu wenye maovu usiwepo.

Hivyo, ulimwengu unaoweza kuwa na maovu kuwapo ni direct contradiction ya kuwapo Mungu huyo.

Kuna mutual exclusivity kati ya kuwapo Mungu huyo na kuwapo ulimwengu unaoruhusu maovu.

Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu huo haupo, ama ulimwengu huo upo na Mungu huyo hayupo.

Ulimwengu huo upo.

Hivyo.

Mungu huyo hayupo.

Kusema Mungu huyo yupo ni sawasawa na kusema kuna pembetatu ambayo hapohapo muda huohuo ni duara pia katika Euclidean geometry.
 
Hoja yako inakuwa contradiction ikiwa premise hii ni kweli: kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuwa na sababu yoyote ya kimantiki ya kuruhusu uovu.

Lakini hilo ndilo hasa linalohitaji kuthibitishwa. Kwa mfano, kuwepo kwa uovu hakujithibitishi moja kwa moja kuwa Mungu hana sababu ya kuuruhusu.

Hivyo hoja yako ni challenge nzito kwa imani, lakini si contradiction ya kimantiki iliyothibitishwa kama “pembetatu ni duara.”
 
Comment ndefu an....🤔
 
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kimantiki hatakiwi kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu ulimwengu unaoweza kuwa na uovu.

Kwa nini?

Kwa sababu, tunapata maswali ya kuchunguza yanayotuonesha hivyo.

Kimantiki, sababu hii ya Mungu huyo kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu inaweza kuwa ndani ya uwezo wake au nje ya uwezo wake Mungu.

1. Je, sababu hiyo ipo nje ya uwezo wake Mungu?, kwamba hawezi kuibadilisha inambidi aumbe ulimwengu unaoruhusu maovu tu, analazimika, hata kama hakutaka? Yani ni kama kuna logic fulani, tuseme kama ya kimahesabu, ambayo inamlazimisha Mungu akitaka kuumba ulimwengu tu, basi lazima akubali maovu yaweze kuwapo katika ulimwengu huo, Mungu hawezi kuepuka hilo?

Kama ni hivyo, basi huyo si Mungu muweza yote, kwa sababu kuna hii sababu ambayo iko nje ya uwezo wake, imemlazimisha aumbe ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya hata kama hakutaka.

Au

2. Sababu hii ya kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya ipo ndani ya uwezo wake Mungu, angeweza kuibadilisha tu, kuiondoa tu, aumbe ulimwengu usioruhusu maovu, yeye ni Mungu muweza yote, lakini kakataa kuibadilisha tu, kaamua kuumba ulimwengu unaoruhusu maovu?

Kama ni hivyo, basi huyu si Mungu mwenye upendo wote, kwa sababu maovu yanaumiza wengi, wakati Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na maovu na hakuna kiumbe chake kitakachoumizwa na maovu. Mungu mwenye upendo wote kimantiki hatakiwi kuruhusu ulimwengu unaoruhusu maovu kama anaweza kuumba ulimwengu usioruhusu maovu.

Either way, sababu ikiwa ndani ya uwezo wake, au nje ya uwezo wake, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu unaoruhusu maovu, contradiction hii ina mutual exclusivity kwamba;

1. Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu unaoruhusu maovu haupo,

2. Ama ulimwengu unaoruhusu maovu upo na Mungu huyo hayupo.

Ulimwengu unaoruhusu maovu upo. Ndiyo huu tunaoishi.

Hivyo,

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…