#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

Hawako serious sasa stivu nyerere ataelemisha nini!? Kuna mtu wa maana anaweza msikiliza yule maamuma
 
Kwasababu tumekubalina ni hiyari, ukichanja tuliza mshono, kama hutaki kuchanja endelea na maisha yako.....mambo ya mmoja kumtishia mwingine kwa msimamo wake nao ni ujinga......kila mtu abaki na anachokiamini basi, akifa athari ni kwa familia yake wewe inakuhusu nn?
 
Mi nimechanja lakini kitoto changu kichanga sitaki kichanjwe! Kuna nesi hapa amenivuta sikio niwe makini.

Naona hakuna muitikio wa chanjo kwa watu wazima wanaamua kuipunguzia kwa vitoto huko leba
Nesi mwenyewe ana elimu gani?
Hao form failure?
 
Kwanza ufahamu kuwa ukipata chanjo baada ya kupata Corona haitakusaidia. So usishangae sana mtu kupata chanjo na kufa. Na chanjo inachukua wiki zaidi ya mbili kujenga kinga dhidi ya corona.

Pia nikwambie tu. Corona imeonyesha kuwa mortality rate ni kama 3%. Hivyo kama katika watu mia walioumwa, ni watatu tu wanakufa. Hivyo huwezi kusema njia za 2020 zinafanya kazi bila utafiti wa kina wa kisayansi. Je kuna waliotumia njia za 2020 na wakafa?
mzee unavyo jitahidi kutetea. Kwani covid yenyewe ukipata hata kwa takwimu za sasa ni asilimia ngapi wanakua kwenye siriaz illness? Toka inaanza ni % ndogo sana ambayo inakua kwenye risk kubwa kwaiyo hiyo 3% unayo isema ni ipi isije kua ndio hiyo hiyo tu ambayo ni sawa na bure
 
Hongera Mkuu kwa Kuchanja. Sasa tusubiri kati ya proposing side au opposing side Nani ataibuka kidedea. Yetu macho
 
Ni vigumu sana kuwaokoa watu ambao ni mind controlled...hili zoezi la microchopping world wide linakwenda kuleta catastrophy kwa wote waliojipeleka kupata Jab..
Hii ni agenda ya kina Bill Gates na Gates pia anatumika, the Hidden Master mwenye kutoa utajiri kwa wanaomcha ndo mwenye true agenda.
Uko sahihi 100% mkuu. The world is so asleep - wawe wazungu au waafrika - wamelala fofofo. Lakini tutaendelea kusema hakika wapo watakaosikia
 
Nakwambia hivi si ajabu hilo maana watu hawajaanza kufa leo kwa ujinga, huko hospitali kuna watu wamelazwa kwa maradhi ambayo sababu ni ujinga tu. Tunasumbuliwa na maradhi mengi sana na husababisha vifo vingi ila yote hayo sababu ni ujinga tu, kama tungejielewa hayo maradhi tusingapata na tungeepusha vifo.

Sasa mimi nakushangaa wewe unaona ujinga kwenye corona tu!
Acha ubishi fuatilia death mortality rate kwa nchi masikini na nchi zilizoendelea ndo utaelewa kuwa ujinga unaua.
 
Naona kama wewe ndiye huyo steve Nyerere maana unavyopigia debe hiyo sindano utadhani unakufa kesho.!
 
Acha ubishi fuatilia death mortality rate kwa nchi masikini na nchi zilizoendelea ndo utaelewa kuwa ujinga unaua.
Ujinga upi unaokusudia wewe ili tuchambue tuweze kujua kama hao nchi zilizoendelea kweli hawafi sana kwa ujinga?
 
Mi nimechanja lakini kitoto changu kichanga sitaki kichanjwe! Kuna nesi hapa amenivuta sikio niwe makini.

Naona hakuna muitikio wa chanjo kwa watu wazima wanaamua kuipunguzia kwa vitoto huko leba
Sasa nesi anakuvuta sikio ni kuwa amekupenda ama?

Uwe na uelewa basi, sio kila mwenye kipaza sauti ndiye mjuzi wa maongezi.
 
Corona ipo toka mwaka jana hapa nchini na kulikuwa hakuna chanjo wala nini sasa ajabu anakuja mtu sasa hivi na kutaka nione chanjo ndio kitu pekee cha kunifanya niweze kuendelea kuishi kwamba bila chanjo sina uhakika wa kuishi.
 
Kwasababu tumekubalina ni hiyari, ukichanja tuliza mshono, kama hutaki kuchanja endelea na maisha yako.....mambo ya mmoja kumtishia mwingine kwa msimamo wake nao ni ujinga......kila mtu abaki na anachokiamini basi, akifa athari ni kwa familia yake wewe inakuhusu nn?
Nani kakuambia kuchanja hiari?
 
Tumekuwa na Tatizo Kuu la kutaka Kusikia Unachokitaka au Kuona na Kifanywe Unachokitaka Mhusika na sio Uhalisia. Wewe ukitaka kukubali kubali, usipotaka acha. Juzi nipo ofisini, kuna jirani yangu hakuwa amefungua ofisi yake, nikampigia kumuuliza kama atakuja akaniambia hana uhakika sababu walikuwa kwenye mazishi ya jirani yao.

Picha nzima ikapatikana jana, kumbe aliyefariki aliwahi kuchanjwa! Baada ya muda maradhi yakawa yanapishana pishana hayamkauki, Jumanne hali ikawa tata akaaga dunia. Hapo Jeshi la Wokovu tena Kurasini nikakutana na same stori ukiachana na za huku mtaani kwetu. Wewe endelea kubisha, hakuna wa kubishana na wewe.
Wanaopigia debe chanjo naona ni watu wenye akili fupi sana.
 
Back
Top Bottom