Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

Kuna siri gani kati ya Wachaga na Mwisho wa Mwaka?

Kaka k ni nani mdau? Ulimaanisha mimi?
Mimi ni mchagga bila kuchanganya kabila. Wazazi wote wachagga.

hua tunaenda kupata baraka za wazazi na kuangalia familia zetu , pia huwa tunaenda kufanya tathmin km kwa mwaka unaofuta kuna haja ya kuongeza jengo lingine! Mi nitaondoka tar 20, tukutane tukapate kitoch na album
 
Infact Mimi nitaondoka hapa Dar kwa Meridian ifikapo tarehe 20 December 2011.
 
Heheh asante.
Mbege itanikoma leo. . .

Na tukiondoka watu huwa wanafurahia sana maana hata Foleni inapungua kwa zaidi ya 50% Maana wengi wetu huwa tunakamata ESCUDO na RAV4 zet haooooooooooo Mgombani! Karibu Lizzy kwetu Maana shughuli ya Kuandaa Mbege tayari iko kwenye Maandalizi
 
Na tukiondoka watu huwa wanafurahia sana maana hata Foleni inapungua kwa zaidi ya 50% Maana wengi wetu huwa tunakamata ESCUDO na RAV4 zet haooooooooooo Mgombani! Karibu Lizzy kwetu Maana shughuli ya Kuandaa Mbege tayari iko kwenye Maandalizi
Heheheh. . . wanapata nafuu.

Mhh kama ukiniambia kutakua na mbege + mbusi ntakuja Mashati kula mwaka mpya.
 
nilishangaa ephraim kibonde badala ya kwenda likizo kwao anaenda kwa mkewe moshi halafu bila aibu anajitapa redioni.
 
ulikuwa unazimwaga tu...full kuzungusha raundi au?
:flame:

Hahahahahaa...yaani Rejao ukipanda migombani na ukaacha kuwapa chakula masela akoo!! huonekani jombaa.... sa kitu minilikua nafanya nikujaza wese full tank kwenye gari zangu na kuwazungusha machalii wangu sehemu mbalimbali kukata maji kwa kiwango cha lami hee!! kuja kustuka Account haina hata uwezo wakununua lita 500 za mafuta dah!! isinge kua kibubu cha ma mrembo wangu kusoma poa kwajina la Mungu ningehaibikia hapo aisee....
 
Kuna jamaa (Mchaga)juzi alitoa angalizo maeneo ya Ken Garden (Arusha)wakati anapata moja baridi....

Nanukuu "Hawa jamaa wa CCM wanadhani sisi Wachaga ni wajinga?
Eti wamepanga uchaguzi wa Madiwani kurudiwa tarehe 22 DEC, kwa kudhani kwamba wachaga wote hatutakuwepo mjini....Kwa tarifa yao, kipindi hiki tunatanguliza mbuzi kuanzia tarehe 15 Dec, na ni lazima turudi Arusha tarehe 21 Dec kupiga kura.....Tafadhali nawaombeni sana, mkishapiga kura msiondoke mpaka kura zihesabiwe na majibu yapatikane ...
Kazi ikikamilika,wote tutaelekea uchagani kuendelea na mbuzi wetu"
 
Mi nimetanguliza mbuzi m1,nataka beberu wa kunukia,mbuzi huyo ntamchinja trh 26/12 ni kwa ajili ya jina la mwanangu wa kiume ambaye atachukua jina la babu yangu mimi(siyo babu yake) kumbuka trh 25 ntakuwa nishapata maji,trh 26 supu kisusio kama kawa, karibuni sana!
 
2: Ni kwanini kila mwaka mwezi huu desemba, unakuta wachagga wanapeleka magodoro nyumbani(vijijini), yale mwanzo walopeleka huwa yanakuwa yameenda wapi?
Nisaidieni majibu tafadhali.[/QUOTE]

Kila baada ya miezi 9 huwa kunakuwa na ugeni kwa baadhi ya familia (watoto),hasa kwa wale wake wanaobaki kijijini .......Nadhani jibu la godoro jipya utakuwa umelipata.............
 
Back
Top Bottom