The hammer
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,397
- 1,786
Acha uongo. Mbona husemi kuhusu MAKAFARA ya kumwaga damu ya mbuzi ama kondoo?!!!
Hakuna kafara yoyote inayofanyika...nikuambie tu,hakuna kabila lolote hapa Tanzania lililotawanyika hapa Tanzania kama Wachagga na Wapare,utaenda Mkoa gani au kijiji gani chenye maendeleo kidogo tu uwakose either Mchagga au Mpare?
So kwa muktadha huo wamejiwekea utaratibu mzuri tu kuwa wawe wanakutana kama ndugu once a year ambayo December ndo yenye siku kuu kubwa mbili za kusherekea na kijumuika pamoja kama ndugu jamaa na marafiki kwa kupotezana mwaka mmoja au zaidi.
Makabila mengine ndugu wote wapo sehemu moja,kweli kutakuwa na haja gani ya kurudi kwao ukizingatia makazi ya kuweza kuhifadhi watu hata watano ni kitendawili?
Japo pia pamoja na kuwa Wachagga na Wapare wanaishi mbali na makwao lakini wamepajenga sana kwao mpaka vijijini kiasi kwamba nyumba zinaweza ku-accomodate watu zaidi tofauti na vijiji vya mikoa mingi hapa Tanzania...
Mfano usiopingika toka nikue,sijawahi kuona nyumba iliyoezekwa kwa nyasi kijijini kwetu toka miaka ya 1985 zaidi ya kuwa na nyumba zilizokuwa zimeezekwa kwa bati za madebe na nyingi zilizoezekwa kwa mtindo huo yalikuwa ni majiko na sehemu za mifugo japo chache pia zilikuwepo za kuishi zilizoezekwa kwa madebe,leo hii huzikuti kule hizo nyumba za mtindo huo.Hakuna nyumba za matope,na hakuna nyumba sijui ya vyumba viwili iliyojengwa kwa mtindo kama darasa na umeme kijijini hapo ulifika miaka ya 1968+ hivi...kwa maendeleo hayo na kwa ndugu,jamaa na marafiki kutawanyika kila mahali,kwanini.tusiwe na siku maalum za kuonana?
Lakini pia,katika makabila haya mawili,ni vigumu kumkuta kijana amekaa idle tu,hajui cha kufanya.Wengi wao wana shughuli za kujishughulisha hata kama anaingiza kidogo sana so anahitaji kupumzika mwisho wa mwaka na kusherekea siku kuu na ndugu zake,tofauti na jamii nyingi za makabila ya hapa Tz na huo ndo ukweli,wenye wivu mjinyonge ndo maana mna chuki sana na wana Kilimanjaro na Arusha pia kwa sasa nayo mmeanza kuichukia,na badoooo!!!!