Kuna siri gani kua ukimsimulia mtu mipango yako ghafla inafeli au kusuasua?

Kuna siri gani kua ukimsimulia mtu mipango yako ghafla inafeli au kusuasua?

nipo online

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,039
Reaction score
2,657
Nimesikia ama kuchunguza kua mara nyingi ukiropoka kwa watu mipango yako inaanza kusua sua na hatimae Kufeli mazima. Tafadhali wabobezi wa masuala ya kiroho naomba hapa ufafanuzi.

Kuna mstari fulan katika biblia kua "usimwage lulu kwenye nguruwe wasije wakazikanyaga na kukurarua" je huenda kukawa na uhusiano hapa? Karibuni.
 
Ukiwa na Jambo lako kaa kimya usitangazetangaze sana hakikisha haueleweki nasisitiza hakikisha hawakuelewi Ijumaa kwako ufanye iwe Jumapili na Jumanne iwe km Alhamisi mchana wakila Ugali wewe kula kashata na kahawa jioni karanga na chai ya ukwaju
 
Ni saikolojia tu.

Saikolojia inasema,ukimsimulia mtu mipango yako akili inajiseti na kuamini kwamba tayari mipango umeshaitekeleza,...hivyo motivation inapungua au kupotea kabisa.

Telling people our plans release dopamine, which can trick the brain into feeling good about our progress on a project, which we actually haven't started yet. This can then disincentivize us to continue, as we already got a good feeling and don't want to do the hard work.
 
Tafadhali mkuu, kwanini ukikiuka hii kanuni unachezea za uso?
Hio ndio ilivyo maana yake wewe huwezi kujisaliti mwenyewe ila mtu mwingine kukusaliti na kuvujisha data zako ni suala la kugusa tu sasa zikimfikia mbaya wako ndio hivyo na usichojua kumpa mtu taarifa zako ni sawa na kuwasha kiberi nyikani pori zima litaungua
 
Nimesikia ama kuchunguza kua mara nyingi ukiropoka kwa watu mipango yako inaanza kusua sua na hatimae Kufeli mazima. Tafadhali wabobezi wa masuala ya kiroho naomba hapa ufafanuzi.

Kuna mstari fulan katika biblia kua "usimwage lulu kwenye nguruwe wasije wakazikanyaga na kukurarua" je huenda kukawa na uhusiano hapa? Karibuni.
Monitoring spirit waits to hear the word of confession to know your heart or next plan to manipulate/block your helpers not to reach your destiny,nimeikopi mahali.
 
Hio ndio ilivyo maana yake wewe huwezi kujisaliti mwenyewe ila mtu mwingine kukusaliti na kuvujisha data zako ni suala la kugusa tu sasa zikimfikia mbaya wako ndio hivyo na usichojua kumpa mtu taarifa zako ni sawa na kuwasha kiberi nyikani pori zima litaungua
Ila wakuu haya mambo haya duh
 
Back
Top Bottom