Kuna siri gani ya mafanikio juu ya mtoto alielelewa na mzazi mmoja?

Kuna siri gani ya mafanikio juu ya mtoto alielelewa na mzazi mmoja?

Black BackUp

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
717
Reaction score
666
Habari wana JF,
Naomba nijikite katika hili hivi" kuna siri ipi ya mafanikio juu ya kijana alielelewa na mzazi mmoja hasa mama"? Nimeona watu mashughuli wengi , wana siasa, wafanya biashara wakubwa, wana muziki kama vile Diamond na wengine wengi wamepata mafanikio lakini wakitoa historia yao utasikia amelelewa na mzazi mmoja au Mlezi tu.

Zipo nafasi nyeti pia katika nchi hua wanafanikiwa kuzipata, kuaminiwa na kuzishikilia mfano katika nafasi za wateule wa Rais, sehemu kama Benki kuu na nafasi nyeti katika vyombo vya ulinzi na usalama. Naomba kujua hua kuna siri gani, malezi au kuna nguvu za kiroho hua zinakuja kuibuka katika kupambana na maisha?
 
Ngoja waje wanaosimanga single mothers
 
Hakuna ushahidi maalumu mpaka sasa ila utafiti unaonesha watoto wanao kua kwa kukosa malezi ya pande mbili za wazazi hujifunza mengi mapema na kuamini mafanikio halisi yanatokana na juhudi zao binafsi.

Siyo lazima walelewe upande mmoja wanaweza kuishi hata kwa ndugu au bibi na babu. Kuna madeko huwa wanayakosa kwa wazazi wao ambayo ndiyo huwakomaza.. Kiakili na kujiamini.
 
Back
Top Bottom