Kuna Taasisi za Serikali ukiajiriwa ni kama umejisajili kuwa maskini milele

Kuna Taasisi za Serikali ukiajiriwa ni kama umejisajili kuwa maskini milele

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,955
Wakuu kwema?

Ndio dunia inakabiliwa na tatizo la upungufu au ukosefu wa ajira ila kama watu tunaojihurumia ni vema kuchagua mwajiri bora na si bora mwajiri.

Kuna ofisi au taasisi zina watumishi maskini sana. Wanaomiliki nyumba za kisasa au magari ya kileo utakuta ni watu wa manunuzi, wahasibu na kiongozi mkuu wa centre husika tu. Wengine wote wanatia huruma.

Ukimwona mtumishi kajenga kibanda basi huyo kakopa na anaugulia maumivu kwa makato ya benki. Ukikosa ajira unakuwa tayari kuajiriwa hata na mchoma mihogo.

Kuna taasisi za serikali mmmhh, bora kwenda kulima viazi tu.
 
Kwa mfano taasisi zipi tupate picha halisi isije ukawa unazungumzia upigaji ambao umedhibitiwa kwa sasa?
 
Kwa mfano taasisi zipi tupate picha halisi isije ukawa unazungumzia upigaji ambao umedhibitiwa kwa sasa?
Halmashauri za majiji, manispaa na mini.
Bila kusahau wakala za serikali na taasisi zilizo chini ya serikali kuu.
Mfano : Kuna technician alikuwa analipwa 520k na taasisi Fulani. Kahamia taasisi nyingine sasa analipwa 1200k. Na posho karibu 800 k per month.
 
Basically, huwezi kuwa tajiri kwa kuajiriwa na kutegemea only one stream of income (salary) huku ukisubiri kustaafu na upate pension. Chances are very minimal unless uwe jizi sugu, tena jizi wa deals nene nene
Mtumishi inabidi aishi kwa uhuru.
Apate basic needs zake kwa wepesi.
Sasa mtu wa take home ya laki tatu, nne, tano huyu ataweza kumpa mwanae elimu bora na kupata fedha ya kufanya biashara. Kumbuka ukiajiriwa kwa tafsiri nyingne ni kwamba mahitaji yako muhimu utapewa na mwajiri wako.
 
We ndo umesema ukweli. Watu wa serikali wanaoweza kuwa na kipato either uwe mwizi wa mali ya umma tena mwizi mkubwaa kama alivokuwa lowasa n.k
 
Halmashauri za majiji, manispaa na mini.
Bila kusahau wakala za serikali na taasisi zilizo chini ya serikali kuu.
Mfano : Kuna technician alikuwa analipwa 520k na taasisi Fulani. Kahamia taasisi nyingine sasa analipwa 1200k. Na posho karibu 800 k per month.
Bila shaka hyo 520k ni ya Temesa,na hyo 1200000 ni kitu Kama Tanroads.
Kama sijakosea ni hvyo
 
Mtumishi inabidi aishi kwa uhuru.
Apate basic needs zake kwa wepesi.
Sasa mtu wa take home ya laki tatu, nne, tano huyu ataweza kumpa mwanae elimu bora na kupata fedha ya kufanya biashara. Kumbuka ukiajiriwa kwa tafsiri nyingne ni kwamba mahitaji yako muhimu utapewa na mwajiri wako.
Yes off course utajiri ni kitu kingine kabisa.
Hapa tunaongelea maisha standard tu/maisha bora yaani kuhusu chakula usiwaze,pa kulala usiwaze,kusafiri usiwaze,kusomesha watoto isiwe shida.
Sio kila mwezi baada ya kununua chakula tu unabaki na madeni.
 
Binadamu hataishi kwa mkate tu.. ni mwendo wa mtu kujiongeza nje ya kazi yake kujiingizia kipato.

Tabu ya wananchi wetu asilimia kubwa sanaaa ni kujaa uvivu na kukosa maarifa na fikra.
 
Back
Top Bottom