Bepari la bariadi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2016
- 420
- 671
Pasipo kumung'unya maneno Hali ya usalama wa raia na Mali zao imetikiswa kwa kipindi hiki, matukio ya ujambazi, unyang'anyi, ukwapuaji, na ukabaji yameendelea kushamiri sasa licha ya kuwepo na matamko mbali mbali kutoka kwa wenye dhamana na usalama wa raia.
Kama halijakukuta Basi fanya simple research kwa kuulizia watu maeneo yako ya kazi au kwenye Daladala au hata kijiweni tu uwaulize maoni yao kuhusu hali ya usalama mtaani kwao,kila kukicha utasikia hapa kama siyo pale.
Kuna huu ukwapuzi wa simu au bag na bodaboda unarudi nao kwa kasi. Tena hawa washenzi wanafunika plate number za pikipiki zao.
Polisi anzeni na hawa, wanaharibu Jina la bodaboda wengine walio raia Wema.
Lakini pia ile spirit na kasi ya kutokomeza ushenzi huu imeishia wapi? Je, nayo imezikwa na mwendazake? Watu hawana amani kabisa hasa jua linapozama.
Mama yetu, kwa hili nakuomba usilegeze sauti mama.
Punda haendi bila mijeredi na ukicheka na nyani utavuna mabua.