Watetezi wa Nyerere wanayo hoja. Kwamba, enzi hizo kweusi, angetumia nafasi yake ya Urais na Uenyekiti wake wa CCM Taifa. Muda huu tunavyojadili habari za Mwl Nyerere, watu wa kabila lake na watu wa dini yake ndio watu pekee ambao wangekuwa wamehodhi mifumo yote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Itoshe kusema, migodi ya dhahabu, mafuta na gesi na rasilimali zinginezo hazikuanza kuvunwa wakati wa Mwl Nyerere. Hoja yake kipindi hicho ilikuwa ni kuwa na subra hadi kuwepo Watanzania wenye sifa na uwezo wa kushiriki ipasavyo kwenye ugemaji wa rasilimali hizi. Ukiniuliza ikiwa alikuwa sawa, nitasema ndio.
Maana baada Azimio la Arusha lililotaifisha mali za mabepari, Watanzania waliopokea hizo mali hawakuweza kuziendeleza. Hivyo Mwl Nyerere aliona amefanya kosa na hakutaka kurudia kosa.
Fast forward, waliopokea kijiti cha uongozi kwa Mwl Nyerere, mbona hawatangulizi maslahi ya nchi kama alivyofanya mtangulizi wao? Tafakuri ya swali hili ndio linarejesha sifa kem kem kwa yule Mzee.
Wakosoaji wa Mwl Nyerere pia sioni kama wanatatizo. Maana lengo lao ni kuibua madhaifu ya kiuongozi ya Mwl ili viongozi waliopo na wajao wasirudie makosa yale yale. Pengine no muhimu kwa wakosoaji kujenga hoja za kimazingira na nyakati ili kuibua mjadala chanya kuhusu viongozi waliopita (Mwl Nyerere et Al) versus viongozi waliopokea kijiti. Lengo liwe kujenga badala ya kudogodesha.